Hivi inakuwaje mzazi anakua tegemezi Kwa mtoto ambaye amejitafuta Kwa jasho lake bila kumrithisha hata mbuzi mmoja

Kuwa oyaone, ndio utashagaa 9 kuitwa kenda...
Endelea kuona wazee wako hawastahili msaada wako kwa kuwa tu haujaridhi chochote toka kwao.
Na mtu huyo huyo utakuta yuko busy kusaidia watu baki na marafiki wakati wazazi wanaishi kwenye ufukara uliotopea.
 
Mimi nakuunga mkono mkuu, nliwahi muomba mzazi wangu mtaji na nilimletea business plan kabisa. Alikataa na kejeli juu kuwa sitoweza fanikiwa kibiashara. Baadae ikabidi nijiajiri tu huko nikawa napata visenti kidogo akaanza kunikejeli kwamba siwezi toboa kupitia "kujiajiri" na kwamba siwezi mfikia mali zake.

Cha ajabu nimejituma mambo yametiki, yeye alikua anatumia hela vibaya tu anatuma kwa marafiki zake mamilion ila mimi alininyima kabisa mtaji. Leo kafilisika, marafiki wote wamemkimbia ndio anakuja nimsaidie.

Kiukweli namsaidia napoweza tu ila mpaka leo huwa nashindwa kuelewa kwanini alikua anafanya vile. Kama aliniona sifai au kilaza basi ashikilie msimamo wake mpaka leo sio tena anakuja tunyang'any'ane visenti wakati yeye alitapanya mamilion.
 
Hakika wazazi nitawatunza Hadi siku ya mwisho. Wazazi wangu ni Moja ya familia yangu Tena Bado tu sijafanikiwa kuwa na Mali hakika wazazi wangu wangeona thamani kamili ya kuzaa mtoto.

Nawapenda sana wazazi wangu.

Huwa nawaombea kungekuwa na uwezo wa kuishi milele wangeishi milele hakika Ili waone faida ya kunizaa na kunikuza haijarishi sijarithishwa hata njiwa.

Potelea mbali Ile Hali ya baba kujikaza na asimwagie Nje jambo tosha la kushukuliwa daima .
 
Endelea kuwalea inaonekana hao walitimiza wajibu wao
 
Nyie alivyowazaa 6 akawatunzaa hakulalamikaa leo nyie 6 kumtunza mmoja kelele kibaooo kengeeee.
 
Mzazii akuzaeee..akusomesheee kesho umuombee mtajii akikunymaa ana rohooo mbayaaaa..! unataka akubebe mpaka linii??
 
Nyie si mnawaambiaga watoto kuwa "tafuta cha Kwako acha kutegemea urithi wa wazazi" na sisi tunawaambia na nyie wazazi wa hovyo "tafuteni vya kwenu, acheni kutegemea vya watoto"

Yaani unitelekeza alafu nikutunze, labda kama sio mimi George..
Na unakuta hilo ni jina la babu yako au mjomba wa baba yako alafu unajitia kujua pumbavu kabisa
 
Ban imeisha lini? tuanzishe vita ingine
kwani bado kuna Ban.. mzazi anapokea kiinua mgongo chake unamletea bajeti ya biasharaaaa..!! kapiga madusco unataka akupee helaaa...muombe akikataa usimchukiee
 
ACHA UPUMBAVU WE MPUMBAVU! UCHOYO WA KIPUMBAVU NA GIZA MBELE LIMEKUJAA. UMEJAALIWA KUPATA PESA NA UNA UWEZO SAIDIA WAZAZI WAKO HATA KAMA HAWAKUKUSAIDIA KUFIKA ULIPOFIKA.

MZAZI NI MZAZI TU NA NI MUNGU WAKO WA HAPA DUNIANI. HAKUNA KITU KINALETA FARAJA NA RAHA MOYONI KAMA KUMGHARAMIA MZAZI WAKO NA KUMPA ATAKACHO (YAANI KUHAKIKISHA ANAKULA VIZURI, ANAVAA VIZURI ATAKACHO, ANATIBIWA VYEMA NA HATA SAFARI UNAMPELEKA MZAZI WAKO KUSAFISHA MACHO)

UNABARIKIWA MARADUFU KWA FURAHA YAKE NA MBIGU ZINAFUNGUKA RIZQ INAZIDI KUNYESHA KWAKO.

ENDELEA KUDANGANYWA NA HUYO KIMADA WAKO WA KIRANGI SIJUI KIMBURU, CHA MOTO UTAKIONA.

FALA!
 
Kwa maana hiyo unataka kusema ww ukiwa mzazi ; mtoto akililia wembe utampa? Mtoto wako anayetambaa akiufuata moto utamwacha afanye kama atakavyo? Unatakiwa ujifunze kufanya maamuzi kwa mambo makubwa kutokana na uzoefu unaopatikana katika mambo madogo. Kwa akili ya kawaida huwezi kuridhia kumpa mtoto m5 hata kama unajua ni haki yake huku ukijua fika kwamba kwa hizo m5 ndo umempa mwanao Umauti kwa mikono yako mwenyewe wewe mzazi. Asikudanganye mtu. Huo sio upendo.
 
1. Mzazi anaforce kuhudumiwa na mwanae
2. Mwanae hataki kumhudumia mzazi

The buttom line of all the 2 problem is poverty. Ukiwa na pesa kama za lugumi unahudumia mpaka watoto wa mtaanu walio letwa duniani na watu wazima wawili walioamua kupeana utamu bila kinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…