Babe la mji
JF-Expert Member
- Dec 14, 2019
- 983
- 2,058
- Thread starter
-
- #41
Unakumbuka wabunge wa upinzani walishawahi kusema Tena mala nyingi kwamba tunahitaji Rais dikiteta kwa maana eti Jk ni Zaifu?Katika viongozi ambao wamerudisha nyuma maendeleo ya nchi hii, kuleta ubaguzi na mifarakano katika jamii ni Magufuli! Afadhali alivyopotea kwa sababu angeipeleka nchi kubaya sana na hata kusababisha vita vya sisi wenyewe!
Kikwete angeendelea walau kwa miaka mitano mbele tungekuwa tumeshaondoka kwenye kundi la nchi maskini na uchumi ungepata kwa mwendo wa swala kama sio mwendo wa duma.
Nchi mbalimbali za Afrika wangekuja kwetu kujifunza jinsi ya kukuza uchumi kwa kasi. Tatizo la Watanzania wengi ni sadists hivyo hatupendi mafanikio ya wengi na tunapenda kuona watu wakiwa na maisha ya chini kuliko sisi ili watunyenyekee.
Pia hata sisi wenyewe pia tukifanikiwa hujiona miunguwatu na kuwa limbukeni.
Lakini mliomba wenyewe kwa MUNGU kwamba mnahitaji Rais dikiteta na maombia yakajibiwa vizuri Sana na hatimae akaja JPM.Ben na Azory wangekuwa hai, Lissu asingepata hayo majeraha..
Sabaya asingekuwa na mashtaka leo hii - Tanzania daima na Mwanahalisi yangekuwepo mtaani.
Bunge lingering 50% kwa CCM na Upinzani...
Unawalazimisha watu kuchangia huu upuuzi ulioandika hapa?Pasko Mayala,Mshana Jr,Tindo, Gentacimine,Mrangi nk mnakalibishwa Sana kuchangia.
Ulitaak aende Kenya na bajaji?. Shirika la ndege linazo nane na ni kazi ya Hayati Magufuli. Hakuna anayeumbwa na Mungu amfurahishe kila mtu, wenye kuthamini alichokifanya tutaendelea kukumbuka utumishi wake.Mkapa,Kikwete na wengineo walikuwa wanatumia usafiri gani kuzunguka dunia kama Samiah asingeenda Kenya????
Kweli kabisa.
Nani alihitaji Rais muuaji bwana shee..unaua hadi vijana wadogo wanakupa vi challenge vya hapa na pale kweli?Lakini mliomba wenyewe kwa MUNGU kwamba mnahitaji Rais dikiteta na maombia yakajibiwa vizuri Sana na hatimae akaja JPM.
Madhara yake yanalazimisha watu kusemaTumpumshe mzee wa watu. Si busara kumsema marehemu maana hawezi kujitetea. Tugange yajayo
NB. HAKUNA BINADAMU MKAMILIFU
JPM alikuwa ni kiongozi mwenye kufanana sana na mahitaji ya nchi yetu. Uonevu ulikuwa umezidi na watu wakijiona ni miungu watu.
Kulikuwa na umafia wa hali ya juu, mitandao ya unyanganyi wa mali za watu ukiongozwa na wafanyakazi wa serikali, hatukuogopana kiasi cha kuoneana huku tukijua yule anayeonewa hana uwezo wa kumfanya chochote muoneaji.
Reli mara ya mwisho kufika Moshi ilikuwa 1995 JPM mwaka jana kaifufua hiyo safari Wachagga wameenda krismasi wakitandika pombe kwenye mabehewa. Hivi sasa kuna wataalam wa masuala ya masuala ya reli 120 wamesomeshwa pale NIT ili wakati SGR ikianza kazi tuwe tayari na wataalam wazalendo.
Ndege hizi kama sio uwezo wa kufuatilia aliokuwa nao RIP zisingenunuliwa. Twiga asingeonekana angani, Mama Samia asingesafiri kwenda Kenya na Uganda akijinafasi.
Hayati alikuwa na udhaifu wake wa hasira na maamuzi yenye kuumiza wengi. Ukitaka tajiri aishi kama shetani maana yake unamuua na njaa mfanyakazi wake. Manji alienda zake Canada, Mo Dewji anaweza kwenda zake South Africa, Bakhresa anaweza kuishi Dubai au New York, tatizo ni yule dereva wake, tatizo ni yule mfanyakazi wa kampuni yake anayesomesha na kulea familia.
Hayati alikuwa na matatizo ya kiafya ambayo ni makubwa, ilikuwa ni vigumu kwake kuwa na amani ya kiakili ikiwa ndani ya moyo kumewekwa kitu cha kumsaidia kupumua. Alikuwa ni mkiwa anayeishi miongoni mwa watu wengi kwa wakati mmoja.
Mungu natumaini amemsamehe madhambi yake kwa kuweza kupata sakramenti ya mwisho siku aliyoaga dunia
Kweli kabisa.Sijawahi kuikubali style ya uongozi wa mwendazake
Nalog off
Nimekuuliza hao wengine walitumia bajaji,baiskeli,ungo,gari,treni au meli kuzunguka ulimwengu kabla ya Magufuli kutawala????Ulitaak aende Kenya na bajaji?. Shirika la ndege linazo nane na ni kazi ya Hayati Magufuli. Hakuna anayeumbwa na Mungu amfurahishe kila mtu, wenye kuthamini alichokifanya tutaendelea kukumbuka utumishi wake.
Kama unachukiwa na wengi pia ni tatizoUlitaak aende Kenya na bajaji?. Shirika la ndege linazo nane na ni kazi ya Hayati Magufuli. Hakuna anayeumbwa na Mungu amfurahishe kila mtu, wenye kuthamini alichokifanya tutaendelea kukumbuka utumishi wake.
Kwa hiyo na wewe unataka ubabe uwe kama mwarabu.Uarabuni kuna ubabe lakini hatuwafikii kwa maendeleo
Nimeongelea kufufuliwa kwa shirika la ndege lililokuwa limekufa. Wao kusafiri na ndege hakumaanishi kwamba shirika lilikuwa lipo vizuri.Mkapa,Kikwete na wengineo walikuwa wanatumia usafiri gani kuzunguka dunia kama Samiah asingeenda Kenya????
Kweli kabisa.
Nimekuuliza hao wengine walitumia bajaji,baiskeli,ungo,gari,treni au meli kuzunguka ulimwengu kabla ya Magufuli kutawala????
Trump alichukiwa na wengi na bado kaongoza Marekani kwa miaka minne.Kama unachukiwa na wengi pia ni tatizo
We acha hizo! Kikwete! Umesahau yaliyokuwa yakifanyika nchi hii? Au unaangalia watu walivyoiba na kujenga magorofa ndo unadhani zingekuwa mali ya serikali? Nchi ilikuwa inakusanya bilioni 800 kwa mwezi yaani trioni 9 kwa mwaka. Hiyo ingekuondoaje kwenyeskini?Kikwete angeendelea walau kwa miaka mitano mbele tungekuwa tumeshaondoka kwenye kundi la nchi maskini na uchumi ungepata kwa mwendo wa swala kama sio mwendo wa duma.
Nchi mbalimbali za Afrika wangekuja kwetu kujifunza jinsi ya kukuza uchumi kwa kasi. Tatizo la Watanzania wengi ni sadists hivyo hatupendi mafanikio ya wengi na tunapenda kuona watu wakiwa na maisha ya chini kuliko sisi ili watunyenyekee.
Pia hata sisi wenyewe pia tukifanikiwa hujiona miunguwatu na kuwa limbukeni.
Kiranga,ni kweli najichanganya lakini ni kutokana na hali ilivokuwa kwa kipindi hicho ndo Mana naonekana kama vile najichanganya.Yani unakubali tulikuwa tunahitaji rais dikteta, halafu unasema JPM aliharibu democracy.
Mbona kama unajipinga mwenyewe?
Kwa
Kwa hiyo na wewe unataka ubabe uwe kama mwarabu.
Hayo yote yameangukia kwenye swala la Uchumi na Democracy.Upo sahihi kwa mtazamo wako Wala sikupingi lakini nazani yote ni kwa Sababu kipindi anachukua nchi presure ilikua kubwa ukiizingatia upinzani ulikua mkubwa Sana .Kuitoa nchi kwenye mazoea na kuiweka sawa ilifkia kipindi akawa anajihami na Katika kujihami ikapelekea kuumiza watu.
Hata na Mimi nikili kaniumiza kiuchumi pakubwa Sana lakini nshamsamehe na bado nakili Kuna vitu kafanya kwa faida ya Nchi
Takwimu za nadharia kumfurahisha mwendazake je hayo makusanyo ya mwendazake yalifanya nini miaka mitano watu bila ajira,maisha ya shida,biashara kuyumba,wafanyakazi kutopandishwa madaraja,huoni kuwa mwendazake ni mwizi namba one Tanzania.We acha hizo! Kikwete! Umesahau yaliyokuwa yakifanyika nchi hii? Au unaangalia watu walivyoiba na kujenga magorofa ndunadhani zingekuwa mali ya serikali? Nchi ilikuwa inakusanya bilioni 800 kwa mwezi yaani trioni 9 kwa mwaka. Hiyo ingekuondoaje kwenyeskini?
Huyo hakuwa rais.
King Bill :Naheshimu Sana mawazo yako pia naomba nikuulize lakini punguza kwanza jazba .Unazani hata Lowasa kama angekua Rais he asingekua dikiteta kwa hali ya kisisa ilivokuwa? Maana presure ya kisiasa ilikua juu Sana kwa kipindi hicho,naomba mawazo yako kwa kuangalia Hali ilivokuwa mwaka 2015.Unawalazimisha watu kuchangia huu upuuzi ulioandika hapa?
Magu alikuwa raisi mbovu kuliko maraisi wote waliokwisha tawala nchi hii.
Huwezi kutawala nchi kama familia yako!