Kiranga:Ni kweli huwezi upo sahihi lkini napenda kukufahaimisha tu ujie Mimi sio kwamba natetea yaliyofanyika ambayo hayakua mazuri .Mimi nimeweka hii mada iwe kama funzo kwa yaliyotekea ili tujifinze na tusiludie Hilo hayo makosa kama taifa .Inabidi tuipiganie KATIBA MPYA kama kweli tunahitaji tusonge mbele.
Katiba mpya ni muhimu.
Lakini je, katiba mpya watu wataitumia?
Maana ya sasa hivi inawapa uhuru watu kufanya mikutano ya kisiasa popote nchini. Rais kaivunja kasema uchumi kwanza.Mikutano inayoruhusiwa na katiba anaibana.
Sasa, katiba mpya ikija halafu rais akaivunja watu watafanya nini?
A law that is unenforceable is as good as none.
Wananchi wa Tanzania wanaelewa kwamba maneno yaliyo katika katiba hayachomoki kutoka katika katiba na kuwawekea adabu watawala?
Wananchibwa Tanzania wanaelewa kwamba watu ndio wanaowashurutisha watawala kubadilika?
Mimi pia naitaka katiba mpya, don't get me wrong.
Lakini, napata wasiwasi kidogo ninapoona ya sasa inavunjwa na watu hawafanyi kitu.
Tukipata mpya ikavunjwa watu watafanya nini cha tofauti?
Tusije kuwa kama mtu anayelalamika gari alilopewa ni mkweche, anataka Ferrari gari ya thamani na mwendokasi sana. Halafu akapewa Ferrari, tukaja k8mugundua kwamba huyu bwana tatizo lake si gari kuwa bovu.
Tatizo lale yeye mwenyewe hajui kuendesha gari lolote lile!