Hivi ingekuwaje 2015 kama tusingempata Hayati Magufuli kwa nchi ilipokuwa imefikia?


Bora kiduchu chenye faida ktk nchi nzima kuliko kingi kisicho na faida kwa nchi nzima, bali kina faida sehemu ndogo tu ya nchi (Chato).

Takwimu za nadharia kumfurahisha mwendazake je hayo makusanyo ya mwendazake yalifanya nini miaka mitano watu bila ajira,maisha ya shida,biashara kuyumba,wafanyakazi kutopandishwa madaraja,huoni kuwa mwendazake ni mwizi namba one Tanzania.

WALOLA VUNZYA tuko pamoja.
 
Wengine wanajiuliza, “hivi ingekuwaje kama Mungu asingemchukuwa mja wake?!”
 
Magufuli ndiye Raisi aliyekuza uchumi kwa rate kiduchu sana ukilinganisha na watangulizi wake. Obvious, graph ya ukuaji wa uchumi ilikuwa ikishuka siku hadi siku.
Thanks for termination of his regime.
 
Kwanini uumize watu wengine kwa insecurities zako binafsi, Tena yeye aliyejiona mzalendo badala atendee ushaur wa wapinzani akawa anawatesa,naona katutudisha nchi yetu hatua nyingi nyuma.

hatua zipi nyuma?
 
Tatizo jamaa hakuwa na uelewa kabisa juu ya wapi Dunia ilipo kwa sasa kiasi akaanza kuifanya nchi nzima kuwa against Dunia
 
Sasa kama umeishasema alichemka kwenye uchumi alikuwa wanini huyo? Make hata hiyo 2015 unayosema tuliangalia zaidi kuwa uchumi uliharibika

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Sasa kipi kizuri, kuwa na uchumi wa kati watu waendwlee kufa na njaa au kuwa na uchumi wa kawaida watu wale bata!!!
 
Kwa mawazo yako jamii yetu ya kitanzania badi ipo gizani na haijui haki zake basi bado shida ipo ,lakini kwa ushauli wangu ni kwamba ,
Nchi yetu inabidi ije na mkakati madhubuti wa kuondoa umasikini .

Umasikini ndo chanzo Cha yote haya.Umaskini ukitokomezwa watu watajua haki zao na hatamae viongozi wasiofaa watawajibishwa na jamii .
 
Huwezi kumaliza umasikini kabla watu hawajajua haki zao.

Watu wanajua haki zao kwanza, halafu ndiyo wanaondoa umasikini.

Kama hujui haki zako, utadhulumiwa tu kila siku, na hivyo huwezi kumaliza umasikini.
 
Huwezi kumaliza umasikini kabla watu hawajajua haki zao.

Watu wanajua haki zao kwanza, halafu ndiyo wanaondoa umasikini.

Kama hujui haki zako, utadhulumiwa tu kila siku, na hivyo huwezi kumaliza umasikini.
Sawa Kiranga ,Sasa kwa maoni yako nini kifanyike ili tuwe kama nchi nyingine za kupigiwa mfano
 
Sawa Kiranga ,Sasa kwa maoni yako nini kifanyike ili tuwe kama nchi nyingine za kupigiwa mfano
Kuna mambo ya kufanya pande zote mbili, pande za wananchi na za watawala.

Wananchi inawabidi waji assert, kujielimisha na kudai haki zao.

Watawala wanatakiwa kufungua mifumo na kufanya ushirikishwaji wa umma zaidi kuruhusu wananchi kuchangia moja kwa moja zaidi maendeleo ya nchi.

Mambo ni mengi sana na unaweza kuandika kitabu usikimalize, lakini hili ndilo kubwa kabisa.
 
Sasa kama mtu ameua uchumi na demokrasia,tumkumbuke kwa lipi?..
 
Useme tu ingekuwaje kama mara tu baada JK angeingia SSH?
 
Una ushahidi wa hivi vitu ulivyoandika. Au nawwe umemezeshwa cassette ukiplay inapiga nyimbo zilizorekodiwa.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama aliharibu demokrasia na uchumi kipi kinachofaa kumpa sifa ?
 
Itoshe kusema akili yako kuna sehemu imeganda. Mtu kakaa miaka 10 hali ilikua vile. Halafu unasema angeongezewa miaka 5 mingine nchi ingeondoka kwenye umasikini?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kipi ?
 
Hiyo demokrasia na uchumi ndivyo city muhimu kuliko hayo yote aliyoyafanya wakati watu wameuliwa wengine wameptea wengine wameokotwa kwenye viroba na kuzikwa bila uchunguzi kufanyika sisi tunamshukuru mungu kwa kumuondsha mapema ingawa alimpa muda kidogo na inshallah amuadhibu kama anavyostahiki amin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…