Hivi kama wewe ni mzazi/ mlezi unachukua hatua au maamuzi gani endapo mtoto wako anakataa kwenda shule?

Hivi kama wewe ni mzazi/ mlezi unachukua hatua au maamuzi gani endapo mtoto wako anakataa kwenda shule?

Dasizo

Senior Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
173
Reaction score
413
Wana JF naombeni ushauri wenu.

Kuna kijana wangu atakataa kwenda shule, yupo kidato cha kwanza . Nimfanye nini maana kama kupiga nimepiga na kumshauri lakini haambiliki😭😭
 
Anataka akae nyumban tu
Mdadisi kama kuna ukatili aliokutana nao shuleni mf. ulawiti, uonevu n.k. Pia, cheki kama ana makundi mabovu.

Fatilia afya yake labda kagundua ana maambukizi ya ugonjwa fulani hatari so haoni haja ya kujiandalia kesho yake kwakuwa anaamini haipo.

Ukijiridhisha hayo yote hayapo na umeshamshauri vya kutosha ila hasikii basi punguza utulivu wake hapo nyumbani.

Hakikisha kila unavyoondoka anaachiwa majukumu hadi aone kushinda nyumbani kugumu. Kufyeka, kulisha mifugo, kuchimba shimo la taka, kupeleka mizigo kwa watu n.k. na ukirudi fatilia kama ametekeleza.
 
Mdadisi kama kuna ukatili aliokutana nao shuleni kama ulawiti, uonevu n.k. Pia cheki kama ana makundi mabovu, afya yake labda kagundua ana maambukizi ya ugonjwa fulani hatari so haoni haja ya kujiandalia kesho yake coz anaamini haipo.

Ukijiridhisha hayo yote hayapo na umeshamshauri vya kutosha ila hasikii basi punguza utulivu wake hapo nyumbani.

Hakikisha kila unavyoondoka anaachiwa majukumu hadi aone kushinda nyumbani kugumu. Kufyeka, kulisha mifugo, kuchimba shimo la taka, kupeleka mizigo kwa watu n.k. na ukirudi fatilia kama ametekeleza.
.......ushauri mujarabu kabisa huu, aufanyie kazi haraka mleta mada......
 
Wana JF naombeni ushauri wenu
Kuna kijana wangu atakataa kwenda shule, yupo kidato cha kwanza . Nimfanye nini maana kama kupiga nimepiga na kumshauri lakini ambiliki😭😭
Pole sana, mpeleke magereza huko, akae hata siku 3, umkabidhi kwa wale wanaitwa Kikosi Maalum cha Magereza, au kamata kwa lazima peleka shule za JWTZ, nasema anyooshwe.
 
Wana JF naombeni ushauri wenu
Kuna kijana wangu atakataa kwenda shule, yupo kidato cha kwanza . Nimfanye nini maana kama kupiga nimepiga na kumshauri lakini ambiliki😭😭
Mwambie achague fani gani anataka ndio umtafutie akafanye.ila ningemshauri achague umeme wa magari mana unalipa sana
 
Kama ni mvivu wa kusoma hata huko kwenye fani atakuwa mtegaji tu maana kuna kusoma pia

Kama ni mvivu wa kusoma hata huko kwenye fani atakuwa mtegaji tu maana kuna kusoma pia
sio veta.ampeleke gereji ya magari akajifunze umeme wa magari hyo fani inalipa sana tena ina pesa kuliko mtu anaefanya kazi ofisini. mimi nilikataa shule nikapelekwa gereji mpaka nimekuwa fundi mzuri tu. na nina vitega uchumi vingi nyumba3 hapa dar na nyumbani kwetu moshi nimejenga pia. nimewafundisha vjana wengi na nimewatoa na wana maisha mazuri tu nafamilia zao
 
Hongera mchaga
 
Wana JF naombeni ushauri wenu.

Kuna kijana wangu atakataa kwenda shule, yupo kidato cha kwanza . Nimfanye nini maana kama kupiga nimepiga na kumshauri lakini haambiliki[emoji24][emoji24]
Ujue dalili ya mvua ni mawingu wazazi wengi wanashtukia mchezo kazi imeisha Yani kumuwashia taa kipofu ni kujiharibia mafuta ilibidi uanze kumshape toka mapema na umuondoe na makundi ila sahizi umechelewa utumie nguvu nyingi sana kumsaidia
 
Back
Top Bottom