Hivi Kariakoo ni kweli kuna Fremu za 3M-5M au ni kutishana tu?

Hivi Kariakoo ni kweli kuna Fremu za 3M-5M au ni kutishana tu?

Ina
Siyo kariakoo ya 2021
Inawezekana mkuu make mambo yanabadirika Ila sifa za namna hiyo kariakoo ishawah pitia ...kitu kingine ukiachilia mbal mdororo wa uchumi sa hv office za kisasa zipo karbia kila sehemu , Kias kwamba mtu sio lazima awe na office kariakoo , anaweza panga , mbezi beach , Moroco , upanga, mwenge , kijitonyama n.k office za kisasa na wateja wake akawapata mtandaoni na akawaelekeza alipo ....hii pia imepunguza popularity ya kariakoo Kwa Kias fulan
 
Kwa biashara ipi!!??
Zama hizi
Acheni kujipa moyo eti hali ni mbaya hapo k.koo kuna hadi frame ukitaka kumvua mtu kama Huna 95m kuendelea hupat frame na hiyo ni kilemba ...K.koo bado biashara ipo ...sema kitaa watu waliochoka wanatafutia pa kusuuza nafsi zao
Hao wanaokuambia eti biashara zinakufa kwa kasi wengi ni watu wa vijiweni nenda mwenyewe kafanye research
 
Wanasoma kwenye vitabu vya history.ila ukija kwenye ukweli wala haipo ivyo kabisa.sasa ivi watu wanapiga pesa Dodoma huko ila hapa Dar ni njaa tu
Sikatai na kweli nimeona maana Dodoma napafahamu vizuri, Ila mkuu mimi naona Dodoma watu wana i overate sanaa, bado sijaona mazingira ya dodoma kuizidi Dar kwa mzunguko wa pesa katika biashara,
Labda tutumie logic ya kua dodoma biashara ni dili kwa sasa sababu uhitaji ni mkubwa na wawekezaji bado ni wachache, na hasa uhitaji mkubwa ni pale mjini tuuu.

Dodoma wenyewe karibuni wote bidhaa wanachukulia Dar...
Dodoma kuishusha Dar kibiashara specifically ilala hilo sizani kama kizazi chetu hiki kitalishuhudia, japo sikatai ya kua Ikitoka Ilala & Temeke sasahivi inafuatia Dodoma Jiji..

Ila kimikoa kabisa, Hata hio nafasi ya pili Dodoma hashiki.
 
Wapi zimefungwa Acha ushabiki ...au usikute unapitaga k.koo saa 11 Asubuh sana hapo lazima ukute zote zimefungwa [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Mwenyewe hilo la fremu k.koo kufungwa kwa kukosa wateja sijwahi shuhudia..
Labda mbali huko, ila sio center pale mfn Aggre na Congo.

Pale Hata ukifunga ukaenda kula, watu wanaulizia hii haina mtu????

Hembu ngoja niulizee,
Naona watu wanataja sana Congo....
Hivi Congo inaizidi kweli Aggrey na Likoma huku kwa wauza electronics????

Ule mjazano pale kongo hasa kale ka uchochoro ka vumbi wanapopiga kelele mda wote kama wamemeza flash wanaoweka nguo kwenye vichanja naona wengi ni wapitaji kuelekea juu huku kwenye maduka mengi.
 
Achana na kkoo kabisa. Kkoo naweza kusema inalisha Zambia, malawi, Congo, Rwanda, Burundi kwa bidhaa. Achia mbali karibu mikoa yote ya Tanzania.
Yes uchumi umeyumba lkn si kwa kkoo. Hata kama kodi zimeshuka si kwa kiwango kikubwa sana. Ninachojua kuna mitaa kodi 5m ni kitu cha kawaida, mingine 3m mingine huko matakoni hata 500k unapata ila hakujachangamka hakuna biashara.
Muda kidogo Kuna kijana aliwahi kuniomba nimboost mtaji awe anauza vitu vya urembo wa wadada ktk vimeza pembeni ya barabara hiyo hiyo mitaa ya kkoo. mtaji alikuwa nao tayari, alihitaji eneo la kuweka meza. Eneo.tu la meza kuachiwa alitakiwa atoe 400k kwa eneo la kuweka kimeza tu.
Kkoo achana nako kabisa
 
Wakuu fremu bado ni ngumu kupata sehemu iliyochangamka asikudanganye mtu , hasa Kwa DSM , mbezi stand ya daladala Tu kupata Tu Banda la kukodi ni tena ndani humo kwenye vibanda ni 200k tena la kiboya Tu , goba pale center mpak 500k sembuse kariakoo.... Kariakoo mtu kukwachia Tu fremu si chini ya 35mil wanaita kumvua kilemba ....
Kukuachia kvp mkuu, fafanua.
 
Acheni kujipa moyo eti hali ni mbaya hapo k.koo kuna hadi frame ukitaka kumvua mtu kama Huna 95m kuendelea hupat frame na hiyo ni kilemba ...K.koo bado biashara ipo ...sema kitaa watu waliochoka wanatafutia pa kusuuza nafsi zao
Hao wanaokuambia eti biashara zinakufa kwa kasi wengi ni watu wa vijiweni nenda mwenyewe kafanye research
Unazungumzia mti mmoja, mm nazungumzia shamba la miti
 
Nina classmate wangu ambaye ni marafiki sanaa,

Baba yao alijenga mjengo wa kupangisha biashara k.koo,
Alishafariki, yule jamaa ile chain nzima ya ka family kao, kila katikati ya mwezi ana uhakika wa 5M..

No wonder aliacha shule, watu wakasema sana ikiwemo walimu anachezea maisha, ila njemba mpaka leo ni bata tuu, na hakuna mazingira ya hizo laana kumpata.

Kuna wazee waliwekeza banaaa,
Wengine bahati mbaya walipambana ila mambo tuu hayakua upande wao BIG up kwao pia.

Achana na hawa waliokua wamelala asaivi wanaong'ang'ania ukali kumbe stress za njaa na madeni, kwa kupenda kufoka mpaka koo limekauka, mda wote anaongea kama kapaliwa na ukoko,
Kidogo tuu anakutishia laana, Bahati nzuri hazishiki, wangetumaliza hawa wazee bila sababu, Anaweza aage anaenda kutafuta kumbe anawaachia msala wa madeni,
...Nimecheka ulivyomalizia mwisho vya kuwapiga Congo wazee wetu ,ambao hawakujenga frame kariakoo![emoji16]

Lakini Mkuu, kila MTU angejenga frame za kupangisha Kariakoo ni Mani angekuwa Mpangaji? [emoji16][emoji16]
 
Khaaaaaa......
Kuniachia kale kachumba nikupe 35M????
Halafu nianze tena kodi??? Mimi kama nimekufuata ukanitajia hivyo naweza nianguke kwa mshtuko.
mkuu kuna wakinga na waha wanalipa kariakoo kuna watu wana hela sana
 
Sikatai na kweli nimeona maana Dodoma napafahamu vizuri, Ila mkuu mimi naona Dodoma watu wana i overate sanaa, bado sijaona mazingira ya dodoma kuizidi Dar kwa mzunguko wa pesa katika biashara,
Labda tutumie logic ya kua dodoma biashara ni dili kwa sasa sababu uhitaji ni mkubwa na wawekezaji bado ni wachache, na hasa uhitaji mkubwa ni pale mjini tuuu.

Dodoma wenyewe karibuni wote bidhaa wanachukulia Dar...
Dodoma kuishusha Dar kibiashara specifically ilala hilo sizani kama kizazi chetu hiki kitalishuhudia, japo sikatai ya kua Ikitoka Ilala & Temeke sasahivi inafuatia Dodoma Jiji..

Ila kimikoa kabisa, Hata hio nafasi ya pili Dodoma hashiki.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]Nakazia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom