Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
Sikutaka kulizungumza hili suala kwa sababu wengi wnaachanganya hisia za kisiasa na uhalisia. Kisiasa biashara ya kkoo imeyumba na fremu hazina watu ILAAchana na kkoo kabisa. Kkoo naweza kusema inalisha Zambia, malawi, Congo, Rwanda, Burundi kwa bidhaa. Achia mbali karibu mikoa yote ya Tanzania.
Yes uchumi umeyumba lkn si kwa kkoo. Hata kama kodi zimeshuka si kwa kiwango kikubwa sana. Ninachojua kuna mitaa kodi 5m ni kitu cha kawaida, mingine 3m mingine huko matakoni hata 500k unapata ila hakujachangamka hakuna biashara.
Muda kidogo Kuna kijana aliwahi kuniomba nimboost mtaji awe anauza vitu vya urembo wa wadada ktk vimeza pembeni ya barabara hiyo hiyo mitaa ya kkoo. mtaji alikuwa nao tayari, alihitaji eneo la kuweka meza. Eneo.tu la meza kuachiwa alitakiwa atoe 400k kwa eneo la kuweka kimeza tu.
Kkoo achana nako kabisa
Huu uongo sijui kwa nini mnaupenda,kwanza unapaswa ufahamu hao wanaofanya biashara dodoma wengi wanachukia mzigo kkoo, pia unapaswa kufahamu hakuna mkoa ambao watu hawapigi pesa Ila inategemea tu unafanya biashara ganiWanasoma kwenye vitabu vya history.ila ukija kwenye ukweli wala haipo ivyo kabisa.sasa ivi watu wanapiga pesa Dodoma huko ila hapa Dar ni njaa tu
Umeongea vizuri sana!Sikutaka kulizungumza hili suala kwa sababu wengi wnaachanganya hisia za kisiasa na uhalisia. Kisiasa biashara ya kkoo imeyumba na fremu hazina watu ILA
Kiuhalisia Hali haipo hivyo Hadi leo hii mtaa wa aggrey watu wanagombea kutoa kilemba kwa mil 30 ili apate fremu ambayo Kodi yake ni mil 2.5
Kodi za milioni moja zipo, Ila zilizo ndani ya jengo au chini au zile za juu, Ila zinazotizama barabara Zina Bei kubwa Sana na watu wanazigombania kuliko kawaida.
Watu wanahisi tupo zama za kina Riziwani na baba yake pamoja na wale wahindi wa GSM kabla hawajabadili jina.Kama unataka fremu Kariakoo niambie, tukutane asubuhi nikupeleke kwa jamaa pasipo hata dalali wala kutoa hata mia ndugu. Mkuu usifanye utani na hali ya sasa ndugu ukafananisha na enzi za JAKAYA maana naona wengi mmekariri.
naona umeona ujekumtolea povu mzee wako hapa kidizainNina classmate wangu ambaye ni marafiki sanaa,
Baba yao alijenga mjengo wa kupangisha biashara k.koo,
Alishafariki, yule jamaa ile chain nzima ya ka family kao, kila katikati ya mwezi ana uhakika wa 5M..
No wonder aliacha shule, watu wakasema sana ikiwemo walimu anachezea maisha, ila njemba mpaka leo ni bata tuu na hakuna mazingira ya hizo laana kumpata.
Kuna wazee waliwekeza banaaa,
Wengine bahati mbaya walipambana ila mambo tuu hayakua upande wao BIG up kwao pia.
Achana na hawa waliokua wamelala asaivi wanaong'ang'ania ukali kumbe stress za njaa na madeni, kwa kupenda kufoka mpaka koo limekauka, muda wote anaongea kama kapaliwa na ukoko,
Kidogo tuu anakutishia laana, Bahati nzuri hazishiki, wangetumaliza hawa wazee bila sababu, Anaweza aage anaenda kutafuta kumbe anawaachia msala wa madeni,
mbona haieleweki, wengine wanasema pabaya wengine wanapiga hela mbona mixed signals ni nyingi?Wanasoma kwenye vitabu vya history.ila ukija kwenye ukweli wala haipo ivyo kabisa.sasa ivi watu wanapiga pesa Dodoma huko ila hapa Dar ni njaa tu
Sindio maana kuna wepesi wa kutoa hizo pesa maana uhakika wa kurudisha upo tena kwa kipindi kifupi tu π!Mkuu
Maisha ya kariakoo sio poa unalipa kodi 3.4M bado choo 5000 kwa mwezi 20000 kwa kajenjere na kuzoa taka bado kodi kama zote ila babaaa kunafaida sana kkooo kuliko mtaani ukipata mtaji kam50M mbn maisha mazuri ndani ya mwaka unadrive
Nasikia kuna baadhi wanauzia majumbani kwao na hasa kwa wateja wao wa siku nyingiKiukweli iliniuma sana manake kulikuwa na mamia ya unoccupied space. Picha niliyokuwa nimepata ni kwamba biashara nyingi zilikufa kwa sababu zamani haikuwa rahisi kuzipata.
Watu wanabisha tuu lakini kariakoo achana nako kabisa , watu wana pesa chafu balaa
Samahani bwana Dagger ...hizo 30m fremu inakuwa yako moja kwa moja au Kodi ya muda mfupi?Mm nna ushaidi k.koo lile jengo la infinix frame za pale barabarani wanapouza simu ..kuna mwamba alitoa 30m kupata frame ...
Mkuu Acha Tu Mimi nimejionea Kwa macho yangu hv , kinyerezi Tu kupata frem pale mwisho ni Laki tatu na jamaa anataka Kodi mwaka mzima na hapepesi macho na frem zpo aside kidog , goba Tu pale center ni 400k na hupati labda mtu umvue , frem zilizo waz ni za pembeni huko .... Sembuse kariakoo sehemu inyohudumia nchi nzima na baadhi ya nchi jirani .... Sometyme tunajifariji tuu Ila ukitaka ujue ingia mwenyewe .... Pale mbezi mwisho stendi kuna jamaa kaweka Banda ndani ndani anakodisha 250k na hapepesi macho , kupata Tu space mpak madalali wanasema zimeisha , mpak utumie nguvu kweli hata Kwa mtendaji ......Acheni kujipa moyo eti hali ni mbaya hapo k.koo kuna hadi frame ukitaka kumvua mtu kama Huna 95m kuendelea hupat frame na hiyo ni kilemba ...K.koo bado biashara ipo ...sema kitaa watu waliochoka wanatafutia pa kusuuza nafsi zao
Hao wanaokuambia eti biashara zinakufa kwa kasi wengi ni watu wa vijiweni nenda mwenyewe kafanye research
Acha kudanganya watu,Kuinunua tena [emoji3] jamaa anakuachia anaondoka na vitu vyake unabaki na frem tupu ndo hyo unampa mil 35 tena na Zaid kulingana na location .... Hapo unaanza kuelewana na mwenye frem sasa kuhusu Kodi na dalali hapo anahitaji chake , TRA nao ndani bila kusahau halmashauri , mlinzi n.k [emoji2957][emoji2957][emoji1787][emoji1787]
πππBaada ya wimbi la Wakinga sasa hivi k/koo kuna wimbi la Wasukuma hela sijui wameziltolea wapi
Yaani unalipa hiyo pesa mtu akupishe then ww unaendelea na mkataba wa pango kwa jina lako.Samahani bwana Dagger ...hizo 30m fremu inakuwa yako moja kwa moja au Kodi ya muda mfupi?
Mkuu nadanganya tena π mbna watu wameshuhudia wenyewe humu , vitu vingine unajarbu mwenyewe boss nenda aggrey au Kongo katafte frem alaf urudi hapaAcha kudanganya watu,