Hivi kumbe SportPesa ni wahuni kiasi hiki?

Hivi kumbe SportPesa ni wahuni kiasi hiki?

Acha kuwangia kazi na biashara za watu. Mbona unakuwa na kumbukumbu ya taarifa za bet yako!!!!

Nitakuwa wa mwisho kuamini hiki
Nasema from my experience. Sijadanganya mtu. Wameedit mkeka wangu.
 
Hawawezi wakafanya huo Ujinga..., ni sawasawa mlevi anayekuja kila siku kwako kunywa pombe alafu uanze kumpa maji badala ya Pombe huku ukijua kabisa yeye ndio anayekuweka hapo mjini kwa kuja kwake kwako na washikaji zake....

Risk ya kufanya hivyo cost yake ni maradufu kwa brand yao
 
IMG-20240929-WA0001.jpg
 
Mkuu, ujanja ujanja unaanzia hapo kwenye kutengeneza list ya betting. Wanacheza na saikolojia.

Unakuta mtu ana furaha kashinda elfu hamsini, unamuuliza how? Anasema mkeka umetiki, unamuuliza ulibet kiasi gani, anajibu 40,000/= ukapata kiasi gani, anajibu 50,000/= sasa umeshindaje 50,000/=? Umeshinda 10,000/= hii 40,000/= ni ya kwako.

Makampuni yanakupa hongera kwa kukurudishia pesa yako kama ushindi. Hawatenganishi ushindi halisi ulioupata na pesa uliyoweka. Wanaharibu tafsiri ya ushindi kwenye ubongo wako.
Sidhani kama kuna mtu anaweka mzigo halafu hajui hizo alizoweka zitamlipa kiasi gani iwapo atashinda. Au wewe kwa mawazo yako unafikiri mtu anaweka tu halafu anakuja kujua mbele kwa mbele?
 
hii na mimi nahisi ni kweli maana na mimi naonaga mkeka sometimes umebadilika bila hata kuelewa mazingira
 
Sidhani kama kuna mtu anaweka mzigo halafu hajui hizo alizoweka zitamlipa kiasi gani iwapo atashinda. Au wewe kwa mawazo yako unafikiri mtu anaweka tu halafu anakuja kujua mbele kwa mbele?
Twende taratibu, Wewe unadhani kwanini unaambiwa umeshinda 50,000 ilihali 40,000 ni ya kwako pamoja na kwamba unajua kuwa hujashinda 50,000 umeshinda 10,000? Kwanini unapewa hongera ya 50,000 na si 10,000?
 
Sasa kwann wanatoa options za kushare code
Kuna system za kudetect fraudent ama match fixing let say Mimi nimenunua game nikastake then nikaisambaza watu watakavyo stake kwenye Ile gemu Kuna sytesms zinawaonesha hii gemu imeuzwa hapa hakuna atakaye lipwa na aliyenunua atapata hasara na wakati mwingine wanafunguliwa mashataka. Lakini sio kushare code za mikeka kwa watu hiyo haina shida ukishare Tena wanafurahi
 
Twende taratibu, Wewe unadhani kwanini unaambiwa umeshinda 50,000 ilihali 40,000 ni ya kwako pamoja na kwamba unajua kuwa hujashinda 50,000 umeshinda 10,000? Kwanini unapewa hongera ya 50,000 na si 10,000?
Ukishinda hauhitaji kuambiwa, ni moja ya matokeo uliyotarajia. Kwani hadi uambiwe? Ukishinda mzigo unaingia kwenye account, uambiwe au usiambiwe, maana uliweka kiasi fulani ukitarajia utapata kiasi fulani na ukiwa unafahamu kabisa faida ni tofauti ya ulichoweka na ulichopata, hata kama haujaambiwa. Kwa nini usubiri kuambiwa wakati hesabu ipo wazi kabisa?
 
wajinga sana walininyima pesa ja jackpot wakasema tulishinda watu elfu 70 kila mmoja akapewa mia tano.
Sijawatumia tena nikakimbilia sportybet
Hahaaa hii balaa ila jamaaa ni wezi sana nilishawaona toka kitambo sana mtu mwenye akili timamu huwezi mkuta sportpesa
 
Watu tuna bet toka 2010 kuanzia M bet mpaka Piga bet karibu kampuni zote bongo tume pita na hatuja wahi kutana na hizo mambo za kubadilishiwa Chaguo hapo ni WEWE mwenyewe ulijichanganya
Kuna uwezekano alikuwa amepiga vyombo
 
Ukishinda hauhitaji kuambiwa, ni moja ya matokeo uliyotarajia. Kwani hadi uambiwe? Ukishinda mzigo unaingia kwenye account, uambiwe au usiambiwe, maana uliweka kiasi fulani ukitarajia utapata kiasi fulani na ukiwa unafahamu kabisa faida ni tofauti ya ulichoweka na ulichopata, hata kama haujaambiwa. Kwa nini usubiri kuambiwa wakati hesabu ipo wazi kabisa?
No, no. Usimfikirie mcheza kamari. Vaa viatu vya mchezesha kamari. Kwanini ameopt kumpa hongera ya ushindi mcheza kamari katika pesa yake aliyobeti na si ile aliyoshinda katika uhalisia? Unadhani sababu ni nini?
 
Mimi sio mchezesha kamari, bali mcheza kamari kwa hiyo navaa viatu vyangu. Nikiweka sh. elfu 40 huku nikijua nikishindwa itapotea yote na nikishinda nitapata sh. elfu 50, sihitaji mtu mwingine hadi atokee kuniambia kwa mchezo wa psychology maana mimi mwenyewe naelewa mapema
 
"Mbet" wameninyima pesa nilioshinda tarehe 30.9.2024...mpaka leo sioni meseji yakuthibitishwa hivi haya makampuni ndo yamefilisika? Ukiwapigia simu hawapokei.
 
Back
Top Bottom