Hivi kuna haja gani ya Kupost mambo yako, watoto, nguo mpya, Ujinga huo na ushamba

Hivi kuna haja gani ya Kupost mambo yako, watoto, nguo mpya, Ujinga huo na ushamba

Hapana , wala hakuna shida , kila mtu ana maisha yake na jinsi anvyopangilia tu namna ya kuishi hivyo sioni sababu ya mwingine kuingilia utaratibu wa mtu
Ni kawaida lakini si kawaida. Haya umepost una kula kitimoto sisi inatuhusu Nini na inatusaidia Nini?
Ukiombwa hata buku tu mtu akanunue dagaa hutoi
 
Maisha ni nini? Kila mtu ana namna yake ya kutafsiri maisha yake na mambo yanayompa furaha! Ukimuona mtu anapost nk ndo alipoona sehemu ya kupumzika na kufurahia maisha! Tuache kiherehere kwenye mipango ya watu na post zao! HAYATUHUSU
 
Wewe ni Sadist mkuu, Mimi sio mtumaji WA vitu mtamdaoni au sio Mtu ninae penda kupost personal life langu la mtandao ila wife huwa anafanya ivo na kids na Sina tatizo na ilo I have just to let them be, Haya mambo bana Sio hata ya kuwa complicated, Mimi huwa sijihusishi kabisa vitu kama birthday ila Birthday za madogo na wife na wazazi I must buy them something as presents na wanafurahi.
 
Mimi Huwa sielewi hasa huu ugonjwa wa kutafuta social validation, hasa wadada na wakaka wasiojielewa ndo Huwa Wana tabia hizi.

Unakuta kidada kimepewa trip ya kuenjoy nje ya nchi, Sasa buana akienda Kule Kila kitu anapost status ya wasap au insta, akiwa swimming pool, kwenye ndege, akiwa anakula chakula, akiwa beach. Sasa nashindwa kuelewa inamaana anachofanya afurahii yeye anachofurahia ni kupost kutuonesha kuwa anafurahia.

Wakati wengine muda wote ni kupost watoto wao , na familia mitandaoni, nafikiri si kila mtu aliyeko kwenye contact zako ni anafurahia hivo , tujifunze kukeep privacy, hayo mambo wanafanya mastaa na ni Kwa ajili ya branding au adverts.

Kila unachofanya unapost, Kila unapoenda sehemu nzuri, au unapokula msosi mzuri post, ukivaa nguo mpya kupost, kutwa kupost watoto wako na kuwasifia, weka mambo Yako private
1. Mtu apande ndege uumie
2. Akila chakula uumie
3. Avae nguo mpya uumie
Hizi ni dalili za;
1. Wewe mkuda unafuatilia ya watu
2. Una wivu kama angerusha vitu dhaifu ungefurahia
3. Unatska kuwapangia watu wapost unavyovitaka.

acheni watu waishi maisha yao
 
Kuna muda inabidi ukubali tu tumeishi sehemu tofauti na malezi tofauti, kama kwenu ilikuwa hata kutoka out na wazazi ni ngumu lazima ushangae mtu akitoka na familia na kuweka status
Wewe unajielewa
 
Bora umesema hili
Alf unakuta hela zinachezewa ovyo
Hapo unawaza hiyo hela ingekuwa kamtaji chako
 
Ila Kwa wanaume kufanya Ivo naonaga imekaa ki creepy creepy 🙄
Sielewag kwann mwanaume mtu mzima ujipost unalamba midomo huku unaimba nyimbo ya mboso mda mwingine aibu naona Mimi
Ningekuwa nauweza wa kumfikia ghafla
Ningemcharaza viboko
 
FB_IMG_1753266380389.jpg
 
Back
Top Bottom