Hivi kuna haja gani ya Kupost mambo yako, watoto, nguo mpya, Ujinga huo na ushamba

Hivi kuna haja gani ya Kupost mambo yako, watoto, nguo mpya, Ujinga huo na ushamba

Simu yake, bando lake, humlishi, humvishi na humhudumii kwa chochote, Sasa Mtu akijiposti mtandaoni wewe inakuuma nini?

Kama hujiposti ni wewe na huo ni uhuru wako.

Na wanao jiposti ni uhuru wao.

Huwezi kupangia watu maisha.
 
Ndio mkuu. Mimi kwenye mitandao ya kijamii sijawahi post hata nikiwa airport tu Wala familia yangu sijawahi post mitandaoni.

Hata wife nishampiga stop kunipost hata siku yangu ya kuzaliwa nishamwambia no na sisherekei.

Badala yake Huwa natoka hata 150-250k nagawaia wahitaji vitu mbalimbali na Bado si post.

Huo ni ulimbukeni na ujinga.
Jambo la kujiuliza unapo post Kwa mfano status Ina expired Kwa masaa24 lengo lako ni Nini Sasa?

Kwamba tujue Kila kitu kuhusu wewe ?
Una uhuru wa kutoposti chochote bila kuingiliwa pia wanaoposti wana uhuru wa kuposti chochote bila kuingiliwa.

Kila mtu ana namna yake ya kuishi.
 
Kama hujui basi ninyi wenye roho mbaya ndo walengwa wakuu, kumbe huwa mnaview ila kucomment hamcoment mnakuja kuripuka huku anonymously sio??

Kila mtu aishi ajuavyo, ukikereka na stutus zake mhide usione.

Kiranga huwa anasema watoto wake, nguo zake, nauli ya ndege yake, beach kalipia yeye wewe inakuuma nini yeye kufanya afanyayo??
 
unafikiri kwanini iliitwa Status/story?
 
Kama hujui basi ninyi wenye roho mbaya ndo walengwa wakuu, kumbe huwa mnaview ila kucomment hamcoment mnakuja kuripuka huku anonymously sio??

Kila mtu aishi ajuavyo, ukikereka na stutus zake mhide usione.

Kiranga huwa anasema watoto wake, nguo zake, nauli ya ndege yake, beach kalipia yeye wewe inakuuma nini yeye kufanya afanyayo??
Upo sahihi, nimeview status tatu nikasema ngoja niende Jamii Forum siwezi vumilia ujinga
 
inferiority complex, hujihisi duni ndani ya nafsi zao na uhisi wengine wanawachukulia kuwa duni. Ili kujipa thamani wasiokuwa nayo huona haja ya kuonyesha ulimwengu kuwa na wao wamo pia.

Ukichunguza kiundani wengi wenye tabia hizi ni wale waliokulia kwenye ufukara mkubwa.
kama ishu ni kujihisi duni, mbona Elon musk anajipost?
 
Mimi Huwa sielewi hasa huu ugonjwa wa kutafuta social validation, hasa wadada na wakaka wasiojielewa ndo Huwa Wana tabia hizi.

Unakuta kidada kimepewa trip ya kuenjoy nje ya nchi, Sasa buana akienda Kule Kila kitu anapost status ya wasap au insta, akiwa swimming pool, kwenye ndege, akiwa anakula chakula, akiwa beach. Sasa nashindwa kuelewa inamaana anachofanya afurahii yeye anachofurahia ni kupost kutuonesha kuwa anafurahia.

Wakati wengine muda wote ni kupost watoto wao , na familia mitandaoni, nafikiri si kila mtu aliyeko kwenye contact zako ni anafurahia hivo , tujifunze kukeep privacy, hayo mambo wanafanya mastaa na ni Kwa ajili ya branding au adverts.

Kila unachofanya unapost, Kila unapoenda sehemu nzuri, au unapokula msosi mzuri post, ukivaa nguo mpya kupost, kutwa kupost watoto wako na kuwasifia, weka mambo Yako private

Unaelewa maana ya Dunia kuwa kijiji?
Au upo Dunia ya Karne ya 18 huko?

Mtu kupost mambo yake wewe inakuumiza au kuvunja Sheria yoyote?

Kama haposti uchi, hatukani MTU, havunji maadili kwa nini uone shida?
 
Jamani si kuna watu ni content creators? Hata kwa wasapu status kama mtu anapost matangazo ya biashara ila mara moja anatupia maisha yake ili kuchangamsha asiwe too boring!

Do better mleta mada.
 
Back
Top Bottom