Hivi kuna mkoa unakosa maadili kama Dar?

Hivi kuna mkoa unakosa maadili kama Dar?

Hiyo mbona ndiyo sahihi au wewe ni ***** au basha ulitaka wanaume wabashiane ? Mbele mwanaume kati mwanamke nyuma mwanaume ndiyo standard...au wewe unapenda kupakatwa na kidume mwenzio nyuma ?mimi huwa naona fedhea sana mwanaume kukaa nyuma ya mwanaume mwenzie ...
Aiseee
 
Uko sahihi.
Kwa mfano usafiri wa boda kutoka kariakoo hadi Gongolamboto ukikodi ni elfu 10 ila mkiwa watatu mtachanga elfu 3 kila mmoja sasa bila kuchangia kwa mtindo huu ni raia wangapi wanamudu kutoa elfu 10 ya kulipia usafiri wa boda kila siku
Kwani daladala hakuna? You can't afford bodabodawa pande daladala. Mwanaume mzima anatoka Mbagala hadi Gomz huku nwanaume mwingine yuko nyuma yake anampumulia. Yaani afadhali apumuliwe kuliko kupanda daladala?!
 
Nimezunguka Tanzania nzima sijawahi kuona mwanamke na mwanaume wasiojuana wakibebwa mshikaki na bodaboda. Hiki kitu unakikuta Dar pekee.

Nikiwa nimesimama, nikaona boda anapiga debe Ubungooo...Ubungooo huku akiwa amepakia abiria wa kike. Nikaamini kabisa labda anatafutwa abiria mwingine wa kike. Aaagh wapi, akaja jamaa akapanda nyuma ya yule dada boda likaondoka. Nikabaki kushangaa tu. Kumbe ndio utaratibu wao

Watu wa Dar es Salaama wana shida sana kwenye maadili
Ndiyo maana kwa mtu ambaye anajielewa hapandi mishikaki ,ni bora apande boda peke yake au bajaji za kushea.
 
Huu mfano mbona sio Dar tu.Kama ni hivyo basi usukumani napo pazingatie.

Kuna siku nilikuwa Geita na shida ya kwenda Kakola.Nilienda parking ya magari ya Kakola(Nyankumbu) nikakuta gari hamna.

Boda akaja akaniuliza Kakola twende nikasema poa.Bei tukaelewana gafla akasema ngoja nipate abiria mwingine nikamwambia sina kulipa pesa unayotaka?gafla sikaja mama yuko serious kupanda nikamwambia jamaa hatakama ni haraka we tembea na huyo.

Hiyo ni ya kwangu.Ukitaka kujua utata wa hili ulizia wenyeji wa Kakola wakwambie boda zinazoenda Nyamishiga sijui Nyangalata huwa wanapakia vipi.Asee kuna watu wanaishi bhana dunia ina maajabu mengi.
Mimi nilishawahi panda boda maana gari zilikuwa hakuna kabisa kwenda Geita mjini ilikuwa inaenda mida ya saa kumi na moja usiku nilikodi boda kutoka Katoro hadi Nyankumbu baada ya kutoka pale stend ya katoro tumetembea kidogo akasimamisha mdada tukasimama akasema nae anaenda Geita mjini tukamchukuwa mie nikakaa nyuma niliienjoy ile safari yaan dada alikuwa mzuri hatari
 
Inasikitisha sababu umeshangaa kitu kidogo sana mpaka uituhumu Dar. Kuna vitu huko ukijionea si utasimulia ukoo? 😁😁😁

Mimi nlishangaa Iringa bajaji imebeba watu wa4[watatu nyuma, mmoja mbele na dereva], halafu ikawa inatafuta abiria mwingine.

Kumbe na seat ya dereva nayo inabeba abiria wawili na dereva anakuwa wa3😁😁😁
Nilipanda vi probox kutoka Tarime kwenda Nyamongo, pale mbele tulikuwa tumekaa watu 3, dere amekaa tako moja, stering ameishika kwa prmbeni(kama anacheza ps😁), halafu ngoma inalaza mshale hatari, yaani roho juu hadi ufike. Sasa kule nyuma balaa lake watu wameshonana hadi kwenye buti na mizigo umo umo.
 
Back
Top Bottom