Hivi kuna mkoa unakosa maadili kama Dar?

Aiseee
 
Uko sahihi.
Kwa mfano usafiri wa boda kutoka kariakoo hadi Gongolamboto ukikodi ni elfu 10 ila mkiwa watatu mtachanga elfu 3 kila mmoja sasa bila kuchangia kwa mtindo huu ni raia wangapi wanamudu kutoa elfu 10 ya kulipia usafiri wa boda kila siku
Kwani daladala hakuna? You can't afford bodabodawa pande daladala. Mwanaume mzima anatoka Mbagala hadi Gomz huku nwanaume mwingine yuko nyuma yake anampumulia. Yaani afadhali apumuliwe kuliko kupanda daladala?!
 
Ndiyo maana kwa mtu ambaye anajielewa hapandi mishikaki ,ni bora apande boda peke yake au bajaji za kushea.
 
Mimi nilishawahi panda boda maana gari zilikuwa hakuna kabisa kwenda Geita mjini ilikuwa inaenda mida ya saa kumi na moja usiku nilikodi boda kutoka Katoro hadi Nyankumbu baada ya kutoka pale stend ya katoro tumetembea kidogo akasimamisha mdada tukasimama akasema nae anaenda Geita mjini tukamchukuwa mie nikakaa nyuma niliienjoy ile safari yaan dada alikuwa mzuri hatari
 
Nilipanda vi probox kutoka Tarime kwenda Nyamongo, pale mbele tulikuwa tumekaa watu 3, dere amekaa tako moja, stering ameishika kwa prmbeni(kama anacheza ps😁), halafu ngoma inalaza mshale hatari, yaani roho juu hadi ufike. Sasa kule nyuma balaa lake watu wameshonana hadi kwenye buti na mizigo umo umo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…