Hivi kuna perfume ya kiume yenye kunukia vizuri kuliko hii?

Iyo pisi iliyokushobokea kisa Perfume nayo haijitambui.
 
Mtu kaingia ktk duka la perfume kaja kuwajaza humu😂.. Enewei Sauvage ni perfume yeboyebo.. hakuna kitu sipendi kama mnukio wangu uwe predictable kirahisi, yaan unapita sehem watu wanajua jamaa limejipigilia Sauvage hili.. hapana.
 
Hii nilipewa zawadi imesifiwa sana, halafu mimi sijaielewa kabisa.

Lakini cologne ina react tofauti na watu tofauti.
 

Sauvage ipo vizuri lakini ishakuwa yeboyebo sababu kila mwanaume hata asiye na uwezo anaweza nukia sababu ya uwepo wa fekero zake...

Kuna unyunyu kibao unaikimbiza hiyo makitu mfano ADG Profumo, LV Immagination etc
 
Mimi uwa ni deodorant mbele sinaga habari nyingi. Wazee wa Dola moja haituhusu
 
Haujipendi ?

Kama unajipenda, kwanini unajipenda unatumia vitu cheap cheap visivyo na ubora na vilivyopigwa marufuku ?
Unajibu ukiwa minnesota aù hapa hapa kwa waswahili wenzio hapa tunachopata original ni hewa tu yaliyabajua yote fak
 
Dah hizi habari za perfume zimenikumbusha tukio moja la ovyo sana:

Nipo mbezi mwisho nimepanda Costa naelekea bunju huko,
Kuna bibi mmoja kapanda pia na vifurushi vya mizigo mizigo mkononi kaja kaa pembeni yangu..... Sikumjari sana nikaendelea na mambo yangu, mara ghafla naanza kuhisi hewa maeneo yale inabadirika kwa kasi Sana. Ikabidi niache shughul zote nifanye ujasusi chapchap kujua what's wrong, baadae nikagundua yule bibi kajipulizia marashi ya maiti

Niliitambua hyo harufu sababu muda si mrefu Kuna msiba wa jamaa yangu ulitokea maeneo flani, tulipokuwa kwenye harakati za kumstiri harufu hiyohiyo ndio alipuliziwa kwa ukali sana.


Nikajua tu Bibi wa watu itakuwa alikutana na machinga wakamuuzia mzigo bei ndogo akaona kawapiga... Kumbe anauziwa perfume ya waliotangulia mbele za haki!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…