Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

Life is too short to hate, sina tatizo na Makonda lakini naanza kupatwa na mashaka what is the secret behind?

Nimesikiliza clouds leo mchana yule jamaa aliyesababishiwa ulemavu wa macho alikuwa studio za clouds, na ndugu Diamonds platnumz pia alikuwepo.

Diamond kama msanii amejikuna amemchangia yule cash millioni 2, lakini kilichonifanya niandike thread hii akaibuka Makonda na ahadi kwamba GSM watamnunulia nyumba huyu muhanga, atapewa bajaj 2 na bodaboda juu.

Hapa ndipo halmashauri yangu ya ubongo imeanza kugoma kuelewa kinachoendelea.

Numero uno; Ieleweke wazi mimi sipingi bwana huyu kupewa msaada lakini nikianza kuconnect dots ndio najiuliuza kunani Makonda na GSM.

Jengo la Bakwata ni GSM ndio watajenga mshenga kwa GSM ni Makonda.
Nyumba ya Muhanga itanunuliwa na GSM mshenga Makonda huyuhuyu, je Makonda anafahamu kuna watu mkoani kwake wLiopata majanga makubwa kuliko huyo aliyepoylteza uwezo wa kuona tena?

Kama kweli kuna wasamalia wema tuwaoneshe na wahitaji wengine kuliko mtu mmoja tu kuonekana ndio kama mgonjwa au muhanga wa Taifa.

Wapo wengi sana wanaohitaji faraja na kufutwa machozi.

Mwisho nawalaumu sana waandishi wetu wa investigation news kwa kutofuatilia kwa kina tukio hili ili umma ujuwe sababu halisi za scorpion kufanya ukatili huu kilikuwa ni kitendo cha kihalifu tu au revenge?

Kuna watu kwa ubaya waliowatendea wenzao ukija kuupata ukweli unaweza kuona hata mtu aliyemtoboa macho mwenzake bado ni adhabu ndogo.

Chonde chonde wanahabari wetu bahasha zitawauwa tafuteni mashirika ya kuwafadhili muandike kalamu zenu mukiwa huru.

Bado akili yangu inagoma tukio hili kuamini kama ni la kihalifu tu ati mkabaji hapana tunahitaji kujuwa ukweli.

Cc: Pasco Manyerere Jackton
I guess you're expert either in criminology or sociology of crime. Maana ulivyounganisha dots mpaka nimependa. All in all you raised important issues herein
 
Siku mkiamka kwenye usingizi ndiyo mtajua nini kinaendelea nyie endeleeni kuunga dots
 
Hizi ni hoja zisizo na mantiki kama zile za vijiwe vya kahawa kuanzia kichwa cha uzi hadi hitimisho ni blah...blah...blahh tu.
Ndio aina ya watanzania ,
Ndio sisi tunaotaka tuipite Kenya Na pia ndio sisi tunaolilia maisha bora huku tumekalia umbea kama wa mleta mada.
Mwanzoni story ilikuwa scorpion katili sana ,apigwe risasi ,mara nae atobolewe macho,mara vile ,
Sasa story imekuwa kisasi na habari za udaku wa GSM.
Ukiwaambia thibitisha basi kwa ushahidi usio na shaka wataanza mitusi.
AMA KWELI,UMASKINI HAKUNA ANAYEULIZA LAKINI UKITAJIRIKA ,
maskini Tanzania.
 
Ndio aina ya watanzania ,
Ndio sisi tunaotaka tuipite Kenya Na pia ndio sisi tunaolilia maisha bora huku tumekalia umbea kama wa mleta mada.
Mwanzoni story ilikuwa scorpion katili sana ,apigwe risasi ,mara nae atobolewe macho,mara vile ,
Sasa story imekuwa kisasi na habari za udaku wa GSM.
Ukiwaambia thibitisha basi kwa ushahidi usio na shaka wataanza mitusi.
AMA KWELI,UMASKINI HAKUNA ANAYEULIZA LAKINI UKITAJIRIKA ,
maskini Tanzania.
Hee hee povu hilo linakutoka umekula ugali wa unga wa omo nini! Unakuja na ile technic ya awamu ya Kikwete ya ''lete ushahidi''! Umeguswa sio! Na bado!
 
Mi nachoshukuru ni kuwa Makonda anafanya vyema sana...hatutakiwi kuhoji ilikuaje jamaa akatobolewa macho.

Ili linaweza kumtokea yeyote yule despite anything.

Kuhusu ili la gsm ni kweli jamaa wanajitolea sana kwenye jamii mpaka sasa wameshiriki kuokoa uhai wa watoto wengi wa nchi yetu waliokua wana tatizo la vichwa vikubwa.operation ambazo either wazazi wa kitanzania wa watoto hao ingewachukua muda kufanikisha zoezi hilo.

Kwa hili nawashukuru sana.
Haya mengine ya kuconnect Dots nawaachia great thinker wenzangu wadadavue.

Imani inanuzuia kumjadili yule anaetumia uwezo wake kusaidia maskini.

Ni Mungu pekee ndie ajuaye connection ya gsm na fedha zao.


Glory to GOD
Una mawazo ya kitumwa kweli kweli. Si mchezo!
 
Kuna taarifa nimezisikia kuhusu huyu jamaa, lakini acha nitulie maana alichotendwa ni unyama sana na si vizuri kujadili tetesi zilizojificha, na ukichukulia kwa sasa wenye haki miliki na taarifa za huyu ni Makonda na leo tena.
leo tena ndo nan?
 
Nimeliona bango la GSM njia ya street nikamkumbuka balozi mdogo wa china aliyepiga Picha akiwa kabeba bastola 3.
Gafla nikamkumbuka riz na malori,
Nikavuta ile picha ya paulo akimfunga riz gidamu ya viatu vyake.
Muda huohuo nikamkumbuka kaka JK hasa lile tabasamu,
Hamadi, nikamkumbuka Hosea na makontena bandarini....
Nimeagiza maji ya kunywa hapa bado natafakari...
 
Nimeliona bango la GSM njia ya street nikamkumbuka balozi mdogo wa china aliyepiga Picha akiwa kabeba bastola 3.
Hahaha..usinikumbushe nyakati za upigaji.

hakika tutamkumbuka mtawala yule kwa kuwatengenezea mazingira mazuri baadhi ya watz kuwa matajiri pasipo kuwa na kazi ya maana.
 
Hivi zile pikipiki kwa kila mjumbe wa mtaa kukopeshwa na makonda zilishatolewa??

GSM ndio waliokua watoe hizo pikipiki kama mkopo kwa wale wajumbe kwa jina la makonda marketing manager wao.
 
Hee hee povu hilo linakutoka umekula ugali wa unga wa omo nini! Unakuja na ile technic ya awamu ya Kikwete ya ''lete ushahidi''! Umeguswa sio! Na bado!
No data no right to say.
Vinginevyo unabaki kuwa umbea wa mama wa uswahilini.
Unajua umuhimu wa kuwa na ushahidi kwenye kabla ya kuropoka.
 
No data no right to say.
Vinginevyo unabaki kuwa umbea wa mama wa uswahilini.
Unajua umuhimu wa kuwa na ushahidi kwenye kabla ya kuropoka.
Data? Unaona mtu anakuchomolea mfukoni usibiri data? Mawe!
 
JISIEMU NDIO WALE NYUMBANI DUKANI SENTA wakwepa kodi kipindi cha mkwere
ENDI OFU ZE STORI
 
Katika vitu vitakuja kumuangusha nakonda ni uhusiano qake na wamiliki wa GSM. Wanatafuta kiki ya akupanda juu, wakifanikiwa unarusi mqendo ule ule wa HSC
 
Back
Top Bottom