Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

Ni vizuri kujiuliza umelifanyia nini taifa badala ya kuuliza kwanini fulani anasaidia mtu au watu. Hujachelewa maeneo bado yapo mengi yanahitaji msaada hebu nawe toa msaada badala ya kutumia kalamu yako katika taaluma ya uandishi kukosoa tu kila kitu. Hata kama ni kukosoa kuwa na positive thinking na si negative. Raisi alimsaidia bajaji mlemavu wa miguu sembuse Makonda kumsimamia kidete mwananchi wa mkoa wake kupata misaada baada ya kupewa upofu ndani ya dakika chache. Tutafakari tunayo taka kuandika kabla ya kuandika hata kama tumesomea kutoa habari lakini tujue hizo habari zinachanzo waandishi wenyewe tuzitafiti na sio kutupia kazi hiyo wengine
 
Hapo ndio Mohamed Ali (Jicho pevu) anahusika,angetoa kipindi Chake "Figisu Figisu za Scorpion"
 
GSM foundation,ni taasisi inayotoa misaada na huduma za jamii kwa watanzania mbali mbali
Anachofanya makonda ni kutumia fursa na nafasi yake ya ukuu wa mkoa kuhamasisha tu
Kwa taarifa GSM waligharamia matibabu ya moyo,GSM waligharamia kliniki ya bure kwa watu zaidi ya 30,000
GSM ndio waliowasaidia watu waliohamishiwa mabwe pande baada ya mafuriko ya jangwani,makonda hata ukuu wa wilaya alikua hajaupata
Heko makonda na GSM endeleeni kusaidia jamii
 
Yeah ,nakumbuka ile ishu ya magwepande miaka 6 iliyopita makonda akiwa bado form five,hawa jamaa walisaidia waathirika wa mafuriko,
so hakuna cha connection ya makonda na hawa GSM,wao kutoa ni moyo,ni kama yule mengi anaewalisha walemavu pilau kila mwaka
 
Binafsi nafurahi kuwa huyu mtu amepata msaada kwa maana kubwa analojiuliza baada ya kuwa kwenye hii hali mpya ni namna gani atakabili majukumu yake kama baba, mume, mwanaume, mkwe nk. Ila shida yangu na Makonda ni kuwa approach yake inamfanya aende kwenye makundi fulani kuomba. Kawaida kwenye kuomba fadhila huwa yanafuata malipo ambayo hufanywa na aliyepokea. Sasa siku GSM akienda omba naye favor kwa mkuu itakuwaje? atakataa kupata kulipa fashila? siku nyinigine akitaka sifa atenda kwa nani? La mwisho, ingekuwa watu wa chama fulani wamefanya anayofanya tungesikia maneno ya kuwa wanatumia tukio hilo kutafua ummarufu wa kisiasa kama ilivyokuwa case ya Bukoba.

Mkuu kwa hili la Makonda na kuwa na ukaribu na kampuni hii kiukweli kuna utata flan,ila kwa suala la makonda kutafta msahada kwa kijana huyu sio ishu ya kutafta umaalufu wa kisiasa maana kwa sasa ndo wameshika dora,na ni wajibu wa govn-kufanya lolote kwa ajili ya wananchi wake......hapa nadhani kaonyesha tofauti kati yake na kandoro+Makambaz!!.tusimlaum sana.
 
Acha wivu mtoa pst. Mbona GSM wamedhamini operation ya watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi Tanzania nzima na wala makonda hakuhusika. Watoto wengi wa maskini ambao hawakua na uwezo hata wa kwenda Dar sembuse India wameweza kupata huduma bure kabisa.
Siwezi kudebate na wewe uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana.

Baada ya kutokea storm kubwa Japan, Yakuza Mob ndio walikuwa wa kwanza kwa quick response kutowa misaada yote iliyohitajika kwa wananchi kabla hata ya serikali ya Japan haijatimiza wajibu wake kwa raia wake.

Sasa nikuulize swali kwa kitendo hiki kinawaondowa Yakuza kutoka kwenye kundi la kihalifu na mauwaji?

Poor IQ Son.
 
Nimeliona bango la GSM njia ya street nikamkumbuka balozi mdogo wa china aliyepiga Picha akiwa kabeba bastola 3.
Gafla nikamkumbuka riz na malori,
Nikavuta ile picha ya paulo akimfunga riz gidamu ya viatu vyake.
Muda huohuo nikamkumbuka kaka JK hasa lile tabasamu,
Hamadi, nikamkumbuka Hosea na makontena bandarini....
Nimeagiza maji ya kunywa hapa bado natafakari...
Tz na vimbwanga vyake....homeshoping center
 
Yeah ,nakumbuka ile ishu ya magwepande miaka 6 iliyopita makonda akiwa bado form five,hawa jamaa walisaidia waathirika wa mafuriko,
so hakuna cha connection ya makonda na hawa GSM,wao kutoa ni moyo,ni kama yule mengi anaewalisha walemavu pilau kila mwaka
Hivi yule Drug King pin wa Jamaica si aliwajengea nyumba kule Jamaica karibu mji mzima?

Je hii iliwazuia CIA kumtia mbaroni kwa sababu anasaidia masikini?

Unafahamu msaada walioutowa Yakuza kule Japan?

Hivi Panya road wakianza kuwafadhili wakulima wa nyanya na vitunguu pia mtaunga mkono wasitiwe mbaroni kwa sababu wakishatoka kukaba 10% wanawasaidia pembejeo wakulima wadogo?

Hivi kuna tajili nchi hii mwenye viwanda ambaye ana pesa kumshinda Bakhresa? Umeshawahi kusikia Bakhresa anatawanya pesa tu?

GSM wakifunga shughuli zao nchini na warudi kwa Yemen nchi haiwezi hata kutikisika wala kuyumba, ila Bakhresa leo akishut down operations zote completely ni lazima nchi itatikisika.

Ndio maana mtu kama Bakhresa haitaji middle Man Rais amekwenda mwenyewe na akajionea uwekezaji wa huyu mzee na akawaagiza mashetani wa Tanesco ndani ya miezi miwili wawe wamemuunganishia umeme, na anampa ardhi pia aongeze uwekezaji.

Wale ndio wafanyabiashara na wawekezaji wa kweli.

Wahalifu wote duniani hujificha nyuma ya hivi vitu mnaviita Foundation na Charity clubs.
 
Kuhusu Scorpion sitaki kumhukumu moja kwa moja maana ukweli wa mambo hayo wanayajua wenyewe yaani SCORPION na SAID,watu wamekazana kushadadia kuwa SCORPION ni katili kwa sababu tu hakuna maelezo yake ila yapo maelezo ya SAID tu ambayo anaeleza yale yanayomfavour yeye.

Connecting the dots na tukio la wale walimu wa Mbeya day,Mawaziri nao wakakurupuka kutoa matamko yasiyo na ukamilifu wa ushahidi sasa tunajionea namna leo waziri yuleyule anaanza kufikiri kutengua tamko lake.
 
Siwezi kudebate na wewe uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana.

Baada ya kutokea storm kubwa Japan, Yakuza Mob ndio walikuwa wa kwanza kwa quick response kutowa misaada yote iliyohitajika kwa wananchi kabla hata ya serikali ya Japan haijatimiza wajibu wake kwa raia wake.

Sasa nikuulize swali kwa kitendo hiki kinawaondowa Yakuza kutoka kwenye kundi la kihalifu na mauwaji?

Poor IQ Son.

Wivu wa kike ndo unaokusumbua.
 
Ila siku zote amna mwekezaji anaependa kupereka kile alichonacho kene sehemu yenye mizengwe.ongea na watu vizuri uone kama utanyimwa sapoti .

Tatizo letu kubwa apa Tanzania hakili zetu zimelemalia kwenye majungu ani ata atuumizi vichwa in positive ways.
 
Back
Top Bottom