Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

Hivi kuna siri gani kati ya Makonda na hawa GSM? Au ni mvuto tu?

".....Wanadamu wana tabia ya kujibu hata kile wasichokijua kwa kuanza kwa maneno kama nadhani au nilisikia...."
 
Huna lolote chuki na husda vinakusumbuwa. Hao GSM wamefadhili watanzania kupasuliwa vichwa karibu nchi nzima hukuliona hilo?
 
Hii kazi ya kufukunyua habari walikuwa nayo global publishers,nashangaa sku hz hawafukunyui sijui wameshiba!
 
Mkuu Matola, nimeguswa ila kwenye marketing strategy, kuna mtindo wa ku capitalize on any publicity opportunity, jamaa ametobolewa macho, amepata public sympathy hivyo wacapitalize wa publicity wanapitia hapo hapo!.

Ninayo taarifa ya connection kati ya hii GSM, Msoga na wale Waarabu, kitu ambacho sijaweza ku connect ni mambo mema makubwa wanayofanya kwa mamilioni ya fedha za kusaidia karibu kila kitu, kwanza hayo mamilioni yanatoka wapi and what for?!.

I fear the Greeks especially when they bring gifts!.

Pasco
Pasco Heshima yako .
mbona wadau wameshajadili sana kuhusu pesa za hawa jamaa..(inasemekana😉 ...inasemekana hawa home shoppin wanatakatisha pesa walizozikusanya kipindi cha jk...
 
Life is too short to hate, sina tatizo na Makonda lakini naanza kupatwa na mashaka what is the secret behind?

Nimesikiliza clouds leo mchana yule jamaa aliyesababishiwa ulemavu wa macho alikuwa studio za clouds, na ndugu Diamonds platnumz pia alikuwepo.

Diamond kama msanii amejikuna amemchangia yule cash millioni 2, lakini kilichonifanya niandike thread hii akaibuka Makonda na ahadi kwamba GSM watamnunulia nyumba huyu muhanga, atapewa bajaj 2 na bodaboda juu.

Hapa ndipo halmashauri yangu ya ubongo imeanza kugoma kuelewa kinachoendelea.

Numero uno; Ieleweke wazi mimi sipingi bwana huyu kupewa msaada lakini nikianza kuconnect dots ndio najiuliuza kunani Makonda na GSM.

Jengo la Bakwata ni GSM ndio watajenga mshenga kwa GSM ni Makonda.
Nyumba ya Muhanga itanunuliwa na GSM mshenga Makonda huyuhuyu, je Makonda anafahamu kuna watu mkoani kwake waliopata majanga makubwa kuliko huyo aliyepoteza tu uwezo wa kuona tena?

Kama kweli kuna wasamalia wema tuwaoneshe na wahitaji wengine kuliko mtu mmoja tu kuonekana ndio kama mgonjwa au muhanga wa Taifa.

Wapo wengi sana wanaohitaji faraja na kufutwa machozi.

Mwisho nawalaumu sana waandishi wetu wa investigation news kwa kutofuatilia kwa kina tukio hili ili umma ujuwe sababu halisi za scorpion kufanya ukatili huu kilikuwa ni kitendo cha kihalifu tu au revenge?

Kuna watu kwa ubaya waliowatendea wenzao ukija kuupata ukweli unaweza kuona hata mtu aliyemtoboa macho mwenzake bado ni adhabu ndogo.

Chonde chonde wanahabari wetu bahasha zitawauwa tafuteni mashirika ya kuwafadhili muandike kalamu zenu mukiwa huru.

Bado akili yangu inagoma tukio hili kuamini kama ni la kihalifu tu ati mkabaji hapana tunahitaji kujuwa ukweli.

Cc: Pasco Manyerere Jackton

Hawa jamaa pia naona wanafanya kila aina ya biashara kuanzia shipping agency, kuuza nguo, shopping malls hadi magodoro. Hata kama ni Ku diversify risk ILA ninachojua unapotaka Ku invest pesa kwenye biashara lazima ufanye research ya kutosha. Najaribu kufumbua jicho la tatu. MUNGU atupe uzima tuone mengi...
 
Ndio aina ya watanzania ,
Ndio sisi tunaotaka tuipite Kenya Na pia ndio sisi tunaolilia maisha bora huku tumekalia umbea kama wa mleta mada.
Mwanzoni story ilikuwa scorpion katili sana ,apigwe risasi ,mara nae atobolewe macho,mara vile ,
Sasa story imekuwa kisasi na habari za udaku wa GSM.
Ukiwaambia thibitisha basi kwa ushahidi usio na shaka wataanza mitusi.
AMA KWELI,UMASKINI HAKUNA ANAYEULIZA LAKINI UKITAJIRIKA ,
maskini Tanzania.


Sass naanza kuelewa maana ya mazombi. Kwa kuanza nahisi ni "majitu mavivu ya kufikiri"
 
".....Wanadamu wana tabia ya kujibu hata kile wasichokijua kwa kuanza kwa maneno kama nadhani au nilisikia...."
Huo unaitwa ujuaji pasipo kujua.
Ukimuuliza umesikia toka kwa nani sidhani kama anaweza kujibu,ama ukimuuliza dhana yako ni sahihi ,sijui anajibu nn.
 
Hivi yule Drug King pin wa Jamaica si aliwajengea nyumba kule Jamaica karibu mji mzima?

Je hii iliwazuia CIA kumtia mbaroni kwa sababu anasaidia masikini?

Unafahamu msaada walioutowa Yakuza kule Japan?

Hivi Panya road wakianza kuwafadhili wakulima wa nyanya na vitunguu pia mtaunga mkono wasitiwe mbaroni kwa sababu wakishatoka kukaba 10% wanawasaidia pembejeo wakulima wadogo?

Hivi kuna tajili nchi hii mwenye viwanda ambaye ana pesa kumshinda Bakhresa? Umeshawahi kusikia Bakhresa anatawanya pesa tu?

GSM wakifunga shughuli zao nchini na warudi kwa Yemen nchi haiwezi hata kutikisika wala kuyumba, ila Bakhresa leo akishut down operations zote completely ni lazima nchi itatikisika.

Ndio maana mtu kama Bakhresa haitaji middle Man Rais amekwenda mwenyewe na akajionea uwekezaji wa huyu mzee na akawaagiza mashetani wa Tanesco ndani ya miezi miwili wawe wamemuunganishia umeme, na anampa ardhi pia aongeze uwekezaji.

Wale ndio wafanyabiashara na wawekezaji wa kweli.

Wahalifu wote duniani hujificha nyuma ya hivi vitu mnaviita Foundation na Charity clubs.
Acha majungu wewe utaolewa. Tutajie biashara haramu wanayoifanya hao GSM otherwise kuendelea kuropoka inaonekana una wivu kama mwanamke.
 
Halafu kuna wapuuzi humu wavivu wakufikiri wanabana puwa kabisa eti tuna wivu? Shubaa miti.
Hakuna lolote nimepitia uzi huo wa mwaka 2012 .mengi hapo tanayozungumziwa ni maisha binafsi ya mtu na familia yake.suala la kusema anahujumu uchumi mnashindwa kuwaelewa kweli magufuli huyu mpaka leo ashindwe kumkamata muhujumu uchumi bandarini? Wangapi wamekamatwa mpaka sasa wapo lupango INA maana magufuli anamuogopa sana huyu mfanyabiashara? Acheni chuki zenu nyie ngoja msikie magufuli kamwita ikulu kunywa nae Chao ndo mtakunywa sumu kabisa. Maana magufuli hapendagi ujinga.
 
Hakuna lolote nimepitia uzi huo wa mwaka 2012 .mengi hapo tanayozungumziwa ni maisha binafsi ya mtu na familia yake.suala la kusema anahujumu uchumi mnashindwa kuwaelewa kweli magufuli huyu mpaka leo ashindwe kumkamata muhujumu uchumi bandarini? Wangapi wamekamatwa mpaka sasa wapo lupango INA maana magufuli anamuogopa sana huyu mfanyabiashara? Acheni chuki zenu nyie ngoja msikie magufuli kamwita ikulu kunywa nae Chao ndo mtakunywa sumu kabisa. Maana magufuli hapendagi ujinga.
Nadhani utafiti ule wa kati ya Watanzania wanne basi mmoja ni kichaa nakubaliana na utafiti huo ni sahihi kabisa.

Maana jinga kama wewe unaamini ni kweli Home Shopping Centre imefirisika halafu wamiliki wanaanza kugawa pesa.
 
Naamini makonda kajuana na hawa watu akiwa bado ni jobless,in short ni marafiki zake,
hawa jamaa wana foundation yao kwa ajili ya kusaidia jamii.
Kampuni kubwa kuwa na foundation kama hiyo ni kawaida sana,wenzetu biashara wanaifanya kisomi,wanajuwa leo wakisaidia jamii,wanatengeza costumer base yao kwa ajili ya product zao,
ni aina fulani ya marketing
Lakin ni Mara chache hata wanajulikana wao ndio waliotoa msaada,utaskia tu Makonda,kama wanatafta kutangaza product zao so tungewajua wao ndio wanatoa kwann kupitia kwa Makonda?
 
Nadhani utafiti ule wa kati ya Watanzania wanne basi mmoja ni kichaa nakubaliana na utafiti huo ni sahihi kabisa.

Maana jinga kama wewe unaamini ni kweli Home Shopping Centre imefirisika halafu wamiliki wanaanza kugawa pesa.
Jibu swali magufuli anawaogopa kuwakamata hawa wahujumu uchumi mpaka sasa ? Tuletee ushahidi wamehujumu Kitu gani. Wacheni wivu nyie. Watanzania wengi hatuna maendeleo kwa sababu ya fitna,wivu, majungu na umbeya na wewe mtoa mada ni mmoja wapo.
 
Huyu mtoa post ni wa kupuuzwa.huwezi kulalamikia uhusiano wa Paul makonda na vijana wa GSM kwa sababu tu jamaa wameamua kusaidia jamii ya watanzania. Hivi watanzania tukoje mbona majungu, fitna na chuki zimetujaa sana? Badala ya kituletea namna wanavyohujumu uchumi ili wakamatwe umebaki kupiga porojo hiyo haisaidii aliyepewa kapewa na wewe Fanya kazi kwa bidii Mungu atakusaidia utapata.
 
Back
Top Bottom