Hivi Kuna ushahidi wowote Yesu alikuja duniani or it's just a conspiracy theory ya watunga stori?

Facts tunazo tunaofuata Kanuni. Kama unataka facts fuata Kanuni. Nakushangaa kwamba unataka kitu ambacho ili kitokee kina Kanuni zake halafu at the same time hutaki kuzifuata Kanuni hizo,my friend unachekesha!.

This physical world has its own rules and so is this spiritual world. Hapa duniani huwa tunatafuta FACTS kisayansi kwa kufuata Principles of scientific investigation ambazo ni OBSERVATION, HYPOTHESIS FORMULATION, EXPERIMENTATION,DATA COLLECTION AND RECORDING,DATA ANALYSIS & INTERPRETATION, CONCLUSION then tumalizia na GIVING A REPORT.

Wakati kwa Upande wa Mungu(Ulimwengu wa Roho) kuna Kanuni zake pia ambazo ni reciprocal ya Kanuni za Ulimwengu huu unaonekana. Huku mtiririko upo hivi:
1. Kusikia Neno lake(FACTS)
2.Kuamini kwamba Mungu yupo
3.Kupitia kumwamini kwako ndipo sasa unakuwa connected nae spiritually
4. Ukishakuwa connected nae spiritually ndipo sasa yeye(Mungu) anaanza kujidhihirisha kwako ili umjue kiundani. Hapa sasa ndipo utakutana na hizo EVIDENCES unazozitaka ambazo zitakuacha mdomo wazi. Nini kutembea juu ya Maji?. Utayaona MAKUBWA zaidi. That little mind of yours will surely be exceedingly blown!.

Kwa kifupi huku kwa Mungu, tunaanza kuambiwa FACTS kwanza kumuhusu (kwa sababu yeye ana uhakika na yeye.Hahitaji Principles of scientific investigation kuthibitika)halafu ndipo YEYE anatupa EVIDENCES sisi tulioamini ili kuthibitisha NENO LAKE(FACTS). Anajidhihirisha kwa njia ambazo kisayansi hazielezeki. Kwa mfano Sayansi inasema ugonjwa fulani HAUTIBIKI,
yeye anautowesha ndani ya sekunde tu. Hizi siri tunazijua tunaomwamini tu(Tuliochagua kufuata KANUNI za Mungu)

Kama kweli upo serious unataka EVIDENCES kuhusu Mungu(Yesu) basi fuata kanuni zake vinginevyo endelea kujifurahisha kwa njia uliyoichagua(Atheism/UkanaMungu) wakati sisi tukiendelea kuandika KURASA mpya kila siku za MIND-BLOWING EVIDENCES za Mungu kwenye maisha yetu. Hapo vipi?
Acha stori njoo na fact. No one needs hear stories wewe njoo na ushahidi hapa unaoeleweka
 
Kanuni zipi mkuu
 
(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)

Proof of Jesus

HAKUNA
mtu aliyeacha nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo, HAKUNA!

Yesu Kristo ndiye Mtu mashuhuri kupita wote kwenye historia, nakuhakikishia.

1) Kwanza dini zote (ikiwemo dini ya atheism) zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.

Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.

Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.

Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa (enlightened).

Wahindu na imani za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.

New age spiritualists wanaohubiri power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.

Waamini sayansi kuwa ndo itawapa majibu ya kila kitu (wakana Mungu) wanasema Yesu alikuwa jamaa mjanja mjanja, mwanasiasa flani ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.

Kuna viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.

YESU KRISTO hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee:

• ndiye Njia inayotafutwa na watu,
• ndiye Kweli inayotafutwa na watu,
• ndiye Uzima wa binadamu
unakopatikana,

• ndiye Mwanga kwenye ulimwengu
huu wenye giza,

•  ndiye Ufufuo kwani kifo sio mwisho,

• ndiye Mlango wa kuingilia Next
Level
,

• ndio Jina pekee tunalopaswa kuliitia,
sio majina ya watu waliokufa,

• ndiye Mchungaji mwema atatupa
kila tunachohitaji,

• ndiye Mwana wa Mungu, Muumba aliyeingia ndani ya uumbaji wake mwenyewe, akawa Mwana wa Binadamu

• ndiye Kristo/ Masihi/ Mwokozi, anayetuokoa na uharibifu (dhambi) na kifo ambacho binadamu anahangaika kukiepuka.

1000036340.jpg

(kuna mtu atakwazika kisa YESU ni ngozi nyeupe. Acha ushamba! Katafute ngozi nyeupe uoe uachane na hizi hoja za bei rahisi)

2) Hakuna mtu mwenye rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.

Waongo na wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa kinastahili kuwa uthibitisho?

Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni hawapendi kuona wanachoona.

Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni, hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.

- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani 6000 za agano jipya katika lugha ya Kigiriki peke yake! Wastani wa hati moja ni kurasa 450!

- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa karne za kwanza kwa kilatini, kiCoptic, kiSyriac n.k tunakuwa na makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya.

NI AIBU kwa waongo na wazushi!

- Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye shehena la nakala kama agano jipya! HAKUNA.

1000036915.jpg

3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu walioshuhudia hayo matukio.

Mpelelezi wa mauaji, James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.

Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.

Tena ukija kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana focus, hamu yake, mtazamo wake, makuzi yake n.k.

- Sasa basi, kitabu cha Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).

- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika walishuhudia kwa macho yao.

- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.

1000036342.jpg

Je kuna sababu yoyote ya kushuku shuhuda hizi?

a) Utasikia "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya".

Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! !

Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.

Kama wazee wa kanisa (church fathers) wa karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini? ?

1000036343.jpg

b) Au utasikia "maandiko yenyewe yameandikwa mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".

i) Kwanza hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:

•Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.

•Muda mrefu umepita.

Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa nakala ya kwanza kabisa.

ii) Pia Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.

iii) Inawezekana pia waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.

1000036344.jpg

c) Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:

i) Kwanza njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya hati 6000 za kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.

ii) Pili njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda kilatini, kiCoptic na kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za Kigiriki.

iii) Tatu njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na utamaduni wa kuandika maoni/uchambuzi kuhusu biblia.

Tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda asilimia 95 ya agano jipya kwa kutumia maandishi ya wazee wa kanisa tu! Kwahiyo wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo walioandika kwenye Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.

Kusema kuwa Biblia imebadilishwa ndio Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)

1000036345.jpg

d) Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka 100AD.

Linganisha na nakala zingine za kihistoria, mfano za mwanahistoria Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya miaka 1000 baada ya Josephus! ! !

Au za Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe! ! !

Au Aristotle, kopi yake ni ya miaka 1400 baaya ya Aristotle! ! !

1000036913.jpg

e) Je tunaweza kujua wakati ambapo nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?

Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa kabla ya 70AD.

Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu alivyotabiri kuwa Yerusalemu itakuja kuharibiwa.

Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya kutoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!

Unakuta mtu badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu haiwezekani kutabiri! ! !

Kwahiyo mtu ameshaamua akilini kwake miujiza haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio! Hapo tayari umeleta ubaguzi (bias) kwenye kupima umri wa hizi nakala za kihistoria.

Kingine, wakati vitabu vya Matendo na Luka vinaandikwa bado kina Paulo, Petro, Yakobo walikuwa hai (miaka ya vifo vyao unajulikana), wakati vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka ya Yohana vinatajwa.

Inawezekana mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90 asitaje kifo cha Nyerere? ?

1000036347.jpg

1000036902.jpg

f) Sasa tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi hazijabadilika?

Tutafuata mlolongo wa ulinzi (chain of custody).

Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha Yohana, alimpa nani hiyo nakala?

Tunawajua baadhi ya wanafunzi wa Mtume Yohana: Ignatius, Polycarp, Papius.

Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao wanajulikana.

So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu linabadilika? Je Yesu alianza kama mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa Mungu mtu?

Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni lilelile: Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka! ! !

Kitabu kama 1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya 50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!

1000036911.jpg

Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu karne ya kwanza, na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitwa - Injili ya Luka, ya Mathayo n.k.

Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka baadae ambavyo wazee wa kanisa hawakuvitambua!

1000036346.jpg

g) Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa mamia na maelfu ya nakala za awali kabisa za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima, kwa lugha zaidi ya nne tofauti.

Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata. Lakini ni maelfu ya nakala tena kwa lugha nne tofauti! !

1000036351.jpg

h) Utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo hatujui nani kakiandika na hakiaminiki".

Unajua ni historia kiasi gani itabidi tuitupilie mbali tukitumia hii hoja?

Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.

Tumeona hapo juu (f), uhalali wa waandishi wa nakala hizi tunaupata kupitia mlolongo wa umiliki (chain of custody).

i) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (contradictions) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?

Kwanza contradiction maana yake haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (variation) sio contradiction.

Kwa mfano, kwenye ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.

Lakini Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6),

huku Luka akifwata ukoo kupitia Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31)!

Njia mbili tunazoweza kupatanisha kisa hiki:

a) Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia Yosefu baba yake mlezi huku Luka akifwata ukoo kupitia Maria mama yake. Ndomana Luka anasema "...na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN).

Yosefu anakuwa mwana wa Heli kupitia ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa mwana wa Daudi kupitia Maria kisheria.

b) Au kupitia ile Sheria ya kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu, kisha Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria.

Unaweza kutafiti zaidi.

Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?

1000036352.png

Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?

Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.

Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio wakikubaliana kila kitu.

Kwanza chochote atakachojibu shahidi kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia hukuniuliza!

Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu maswali tofauti.

Mathayo na Marko hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili.

Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! ! Hakijaharibika kitu.

Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo mmoja tu.

Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya tetemeko na jiwe la kaburi.

Mathayo
anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko"?

Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?

Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi.

Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.

J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya kutegemeka.

Hata yangefanana neno kwa neno, wazushi wangekataa pia! Wangesema hawa watu wametunga.

1000036353.jpg

4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye kutegemeka kihistoria.

Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD) ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la, basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.

Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.

Kwanza Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo yalilindwa sana, yalitunzwa, yalisambazwa na kutafsiriwa!

Tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu waliofuatilia na kulinda maandishi yake! ! Kama kuna uongo amesema hakuna wa kumpinga!

Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1‭-‬4 BHN)

Mtume Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)

Mtume Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (1 Wakorintho 15:4‭-‬6 BHN)

Biblia ni nyaraka zenye kutegemeka kabisa za historia.

Sio hekaya au hadithi!

Biblia sio Gilgamesh epic!

Biblia iliandikwa na mashahidi wa matukio halisi ya historia, wakishuhudiwa na mashahidi wenzao wa hayo matukio.

1000036354.jpg

5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha mateso makali sana kwa wakristo.

Walichohitaji ni kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha yao,

lakini mamia na maelfu walikubali kuuawa: walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!

Kuna faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani?

Pesa? Mamlaka? Wanawake?

Zaidi ya mateso na kudharaulika!

Au wote walikuwa wanaota?

Ni nini kilichowasukuma?

Na kuna tofauti ya mtu kukufuata kukuua kwasababu ya imani yako, na mtu aneyeenda kujitoa kafara kwasababu ya imank yake.

1000036356.jpg

1000036355.jpg

6) Tuna uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt).

Haiwezekani kuwa na uthibitisho bila shaka kabisa (beyond possible doubt).

Hiyo itahitaji kujua KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.

Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha bila shaka kabisa maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika bila shaka kabisa kwamba hutogongwa na gari kesho, hutopigwa na radi, hutotekwa n.k.

Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa hazihitaji uthibitisho bila shaka kabisa.

Nafasi ndogo iliyobaki kati ya uthibitisho bila shaka yoyote na uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na majibu.

Ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya IMANI.

Sio Imani kipofu: ni Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!

Kuwa na TUMAINI sio kuwa na matamanio ya kufikirika.

Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana uthibitisho usio na shaka uliopata.

"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
Yohana.6.28‭-‬29.SRUV

"Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta."
Waebrania.11.6.BHN

"Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema."
1Wathesalonike.5.21.BHN

1000036357.jpg
 
Mambo kwa ushahidi nadhani Kuna watu kama kina Kiranga humu ni wakongwe kuliko Mimi na wengine, wamewahi kuleta ushahidi mbalimbali humu hivi vitu ni stori.

Na ili ukweli ujulikane njoo na ushahidi, sio stori burden of proof ndicho kinachohitajika.
Kama huwezi kuamini haya niliyosema hata nikitoa ushuhuda huwezi kuamini pia. Siwezi kukulaumu maana haya ni mambo ya imani zaidi. Sikumwona Yesu kwa macho yangu lakini niliamua kumwamini kupitia maandiko ya Biblia na nikamwona dhairi katika maisha yangu na hakuna wa kuweza kunigeuza nimwache. Nikiwa kwake nina matumaini, kuna amani tele, faraja nyingi, kwenye shida anaonekana akikusaidia, anakuponya magonjwa, anakulinda pamoja na familia yako na mengine mengi tu. Kuna mengi ningeweza kukueleza kuhusu huyu Yesu lakini kwa sasa niishie hapo tu maana mengine itakuwa magumu wewe kuelewa. Nikikuambia YEYE ndiye muumbaji wa vitu vyote, na ujue pia kwamba kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA. Hayo utakutana nayo suku moja huko mbele ya safari hata kama kwa sasa bado kuamini uwepo wake.
 
(not debating, just leaving this here for Genuine Truth Seekers)

Proof of Jesus

HAKUNA
mtu aliyeacha nyayo nyingi kwenye historia kama Yesu Kristo, HAKUNA!

Yesu Kristo ndiye Mtu mashuhuri kupita wote kwenye historia, nakuhakikishia.

1) Kwanza dini zote (ikiwemo dini ya atheism) zinamkubali Yesu Kristo, halafu Yesu anajikubali mwenyewe tu.

Wayahudi wanasema Yesu alikuwa Rabi/mwalimu.

Waislamu wanasema Yesu alikuwa nabii.

Wabuddha wanasema Yesu ni mtu aliyeangaziwa (enlightened).

Wahindu na imani za huko Mashariki wanasema Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu, mungu flani aliyechukua umbo la binadamu, mwalimu, mtawa, mtu mtakatifu aliyeamua kuachana na ya ulimwengu n.k.

New age spiritualists wanaohubiri power of the mind, wanasema Yesu alikuwa ni mtu aliyefuzu kwenye hiyo sekta.

Waamini sayansi kuwa ndo itawapa majibu ya kila kitu (wakana Mungu) wanasema Yesu alikuwa jamaa mjanja mjanja, mwanasiasa flani ambaye alianzisha chama chake na kupata wafusi.

Kuna viazi vichache vinasema Yesu hakuwepo kabisa.

YESU KRISTO hamtaji yeyote yule, anasema yeye pekee:

• ndiye Njia inayotafutwa na watu,
• ndiye Kweli inayotafutwa na watu,
• ndiye Uzima wa binadamu
unakopatikana,

• ndiye Mwanga kwenye ulimwengu
huu wenye giza,

•  ndiye Ufufuo kwani kifo sio mwisho,

• ndiye Mlango wa kuingilia Next
Level
,

• ndio Jina pekee tunalopaswa kuliitia,
sio majina ya watu waliokufa,

• ndiye Mchungaji mwema atatupa
kila tunachohitaji,

• ndiye Mwana wa Mungu, Muumba aliyeingia ndani ya uumbaji wake mwenyewe, akawa Mwana wa Binadamu

• ndiye Kristo/ Masihi/ Mwokozi, anayetuokoa na uharibifu (dhambi) na kifo ambacho binadamu anahangaika kukiepuka.

View attachment 3555605

(kuna mtu atakwazika kisa YESU ni ngozi nyeupe. Acha ushamba! Katafute ngozi nyeupe uoe uachane na hizi hoja za bei rahisi)

2) Hakuna mtu mwenye rekodi nyingi kumhusu kwenye historia kama Yesu Kristo.

Waongo na wazushi wanasema hamna uthibitisho. Ni nini hasa kinastahili kuwa uthibitisho?

Shida sio kuwa hamna uthibitisho, shida ni hawapendi kuona wanachoona.

Yesu angekuwa ni mwalimu tu mwenye hekima ambaye hakuzaliwa na bikra, hakufanya miujiza, hakufufuka na kupaa mbinguni, hakuna ambaye angepinga kuwa hakuna mtu mwengine kwenye historia ambaye kumbukumbu zake zilitunzwa kwa wingi kama Yesu.

- Kwa sasa tuna takriban hati za zamani 6000 za agano jipya katika lugha ya Kigiriki peke yake! Wastani wa hati moja ni kurasa 450!

- Tukiongeza na nakala zilizotafsiriwa karne za kwanza kwa kilatini, kiCoptic, kiSyriac n.k tunakuwa na makumi ya maelfu ya nakala za agano jipya.

NI AIBU kwa waongo na wazushi!

- Hakuna maandiko yoyote kwenye historia yenye shehena la nakala kama agano jipya! HAKUNA.

View attachment 3555608

3) Vitabu vya Injili viliandikwa na watu walioshuhudia hayo matukio.

Mpelelezi wa mauaji, James Warner Wallace (J.W.W), mkana Mungu aliyegeuka na kumwamini Yesu anasema akiitwa kwenye tukio la mauaji, maelekezo ya kwanza anayotoa kwa polisi ni kuwa wawatenganishe walioshuhudia hilo tukio. Maana wakikaa wote wataanza kujadili hilo tukio mpaka aje afike atakuta wana maelezo yanafanana fanana.

Lakini wakitenganishwa, akija kuwahoji mashahidi, maelezo yao huwa ni shagala bagala, huenda yakaonekana hata kuwa yanapingana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa yanapingana.

Tena ukija kuchanganya maelezo yao yanayoonekana kupingana ndo unapata picha vizuri kwasababu kila mtu anakuwa anasimulia kutokana na mazingira aliyokuwepo wakati wa tukio, alichokuwa ana focus, hamu yake, mtazamo wake, makuzi yake n.k.

- Sasa basi, kitabu cha Luka kinasema kabisa anayoandika daktari Luka ni shuhuda za mashahidi alioenda kuwahoji (Luka 1).

- Mathayo na Yohana wanasema waliyoandika walishuhudia kwa macho yao.

- Injili ya Marko inakubalika na wachambuzi kuwa ni Marko alikuwa akiandika kwa niaba ya mtume Petro aliyekuwa anamsimulia, akimsaidia kutafsiri kwenda Kigiriki.

View attachment 3555611

Je kuna sababu yoyote ya kushuku shuhuda hizi?

a) Utasikia "haiwezani kitabu cha 1 Petro kiwe kiliandikwa na mtume Petro kwasababu kimeandikwa kwa Kigiriki cha kisomi kabisa na mtume Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya".

Sasa kwanini asijue kigiriki wakati maisha yake yote aliishi eneo ambalo watu waliongea kigiriki! !

Lakini pia inaoneka kuwa Petro alikuwa anamsimulia mtu anamuandikia.

Kama wazee wa kanisa (church fathers) wa karne ya kwanza na ya pili kwenye barua zao walikuwa wanarejea maandiko na wanakubaliana kuwa yaliandikwa na flani na flani, unakataa nini? ?

View attachment 3555613

b) Au utasikia "maandiko yenyewe yameandikwa mamia ya miaka baada ya matukio kwahiyo yamebadilishwa au kutungwa ".

i) Kwanza hatuna nakala halisi zilizoandikwa kwa mikono ya mitume wenyewe, sababu ni wazi:

•Nyenzo walizotumia (ngozi) hazingeweza kudumu.

•Muda mrefu umepita.

Nakala za historia zilikuja kuanza kudumu wakati walipoanzisha taasisi za kutunza nakala hizi, ndomana unapokuja kukutana na nakala yoyote ya historia ya zamani zaidi iliyotunzwa unaweza kukuta ni ya miaka zaidi ya 90, 300, 1000 baada ya kuandikwa kwa nakala ya kwanza kabisa.

ii) Pia Nakala nyingi ziliharibiwa na waliochukia ujumbe wa Wakristo.

iii) Inawezekana pia waliiga utamaduni wa Wayahudi ambao waliharibu nakala za zamani zilizochakaa kila waliponakili maandiko kwenye sehemu mpya.

View attachment 3555614

c) Kama watu wangetaka kubadilisha biblia, ingebidi wapitie njama za viwango vitatu:

i) Kwanza njama ya hati - ingebidi wachukue zaidi ya hati 6000 za kigiriki agano jipya wazibadilishe na wafiche ushahidi kuwa wamefuta wino wakabadilisha.

ii) Pili njama ya lugha - Kisha itabidi wakatafute maelfu ya hati za agano jipya zilizotafsiriwa kwenda kilatini, kiCoptic na kiSyriac wazibadilishe zote ziendane na uongo waliyoandika kwenye zile za Kigiriki.

iii) Tatu njama ya maoni ya wazee wa kanisa (early church fathers) - wazee wa kanisa wa karne za kwanza walikuwa na utamaduni wa kuandika maoni/uchambuzi kuhusu biblia.

Tukisema tutupe biblia zote, tunaweza kuunda asilimia 95 ya agano jipya kwa kutumia maandishi ya wazee wa kanisa tu! Kwahiyo wanaotaka kubadilisha biblia ingebidi pia wapitie barua zote za wazee wa kanisa wabadalishe iendane na uongo walioandika kwenye Kigiriki na kilatini, kiCoptic na kiSyriac.

Kusema kuwa Biblia imebadilishwa ndio Conspiracy Theory kubwa kuliko zote kwenye karne yetu (ikifuatiwa na Evolution)

View attachment 3555620

d) Bila kusahau kopi tulizonazo za Injili zinakaribiana umri na nakala halisi, mfano tuna kopi za miaka 100AD.

Linganisha na nakala zingine za kihistoria, mfano za mwanahistoria Josephus ambaye kopi yake ya zamani kabisa tuliyonayo ni ya miaka 1000 baada ya Josephus! ! !

Au za Julius Caesar na vita zake kopi tuliyonayo ya zamani kabisa kumhusu ni ya miaka 900 baada ya Caesar mwenyewe! ! !

Au Aristotle, kopi yake ni ya miaka 1400 baaya ya Aristotle! ! !

View attachment 3555714

e) Je tunaweza kujua wakati ambapo nakala ya kwanza kabisa iliandikwa?

Kwa mfano, kitabu cha Matendo kilichoandikwa na Luka kinaongelea utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu (Matendo 6:14). So tunaweza kuhitimisha kuwa kiliandikwa kabla ya 70AD.

Kwenye kitabu cha Luka, Luka anasimulia jinsi Yesu alivyotabiri kuwa Yerusalemu itakuja kuharibiwa.

Hakuna kitabu chochote kwenye agano jipya kilichosimulia tukio la kuharibiwa kwa Yerusalemu, zaidi ya kutoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu (70AD)!

Unakuta mtu badala ya mtu kuhitimisha kuwa Yesu anaweza kutabiri kwa usahihi, mtu anasema hivyo vitabu viliandikwa baada ya tukio kwasababu haiwezekani kutabiri! ! !

Kwahiyo mtu ameshaamua akilini kwake miujiza haiwezekani kwahiyo akiona simulizi la utabiri uliokuja kutimia maana yake liliandikwa baada ya tukio! Hapo tayari umeleta ubaguzi (bias) kwenye kupima umri wa hizi nakala za kihistoria.

Kingine, wakati vitabu vya Matendo na Luka vinaandikwa bado kina Paulo, Petro, Yakobo walikuwa hai (miaka ya vifo vyao unajulikana), wakati vifo vya wafuasi wengine wa Yesu kama Stephano na Yakobo kaka ya Yohana vinatajwa.

Inawezekana mtu aandike historia ya Tanzania ya miaka ya 90 asitaje kifo cha Nyerere? ?

View attachment 3555622

View attachment 3555718

f) Sasa tutajuaje kuwa nakala hizi za agano jipya zilizonakiliwa vizazi baada ya vizazi hazijabadilika?

Tutafuata mlolongo wa ulinzi (chain of custody).

Kwa mfano, aliyeandika kitabu cha Yohana, alimpa nani hiyo nakala?

Tunawajua baadhi ya wanafunzi wa Mtume Yohana: Ignatius, Polycarp, Papius.

Hawa wanafunzi nao wana wanafunzi wao wanajulikana.

So tunaangalia kwenye huu mlolongo wa wanafunzi, Je simulizi kumhusu Yesu linabadilika? Je Yesu alianza kama mtu wa kawaida kadri muda ulivyoenda akageuka kuwa Mungu mtu?

Hapana! Tangu kitabu cha Yohana hadi barua za wanafunzi wake (wazee wa kanisa) na wanafunzi wao, simulizi ni lilelile: Yesu alizaliwa na bikra, alifanya miujiza, alikufa, akafufuka! ! !

Kitabu kama 1 Wakorintho kinakadiriwa kuwa cha miaka ya 50AD, na kinaongelea Ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15). So Ufufuo wa Yesu ni habari iliyokuwepo tangu karne ya kwanza, haikutungwa baada ya miaka kupita!

View attachment 3555652

Hata kuhusu vitabu vilivyokuja kurasimishwa kwenye Baraza la Laodicea (363AD), ndo hivyo hivyo vilivyokuwa vinanakiliwa kwenye barua za wazee wa kanisa tangu karne ya kwanza, na vilikuwa vinaitwa hivyo hivyo vinavyoitwa - Injili ya Luka, ya Mathayo n.k.

Baraza halikuja kuamua lolote jipya kuhusu vitabu zaidi ya kukataa vitabu vilivyokuja kuibuka baadae ambavyo wazee wa kanisa hawakuvitambua!

View attachment 3555716

g) Kingine cha kutujuza kuwa nakala hazijabadilika ni uwepo wa mamia na maelfu ya nakala za awali kabisa za agano jipya kwa visehemu au nzima nzima, kwa lugha zaidi ya nne tofauti.

Zingekuwepo kopi mbili tu kungekuwa na utata. Lakini ni maelfu ya nakala tena kwa lugha nne tofauti! !

View attachment 3555656

h) Utasikia "kitabu cha Mathayo hakijasema kimeandikwa na Mathayo kwa hiyo hatujui nani kakiandika na hakiaminiki".

Unajua ni historia kiasi gani itabidi tuitupilie mbali tukitumia hii hoja?

Hakukuwa na utamaduni wa mtu kuandika jina lake kwenye makala zake.

Tumeona hapo juu (f), uhalali wa waandishi wa nakala hizi tunaupata kupitia mlolongo wa umiliki (chain of custody).

i) Vipi kuhusu zinazodaiwa kuwa ni utata (contradictions) zinazoonekana kwenye zile Injili nne?

Kwanza contradiction maana yake haziwezi kupatanishwa. Kilichopo kwenye Injili ni tofauti (variation) sio contradiction.

Kwa mfano, kwenye ukoo wa Yesu, Mathayo 1:16 inasema baba ya Yosefu ni Yakobo huku Luka 3:23 inasema baba ya Yosefu ni Heli. Mtu anakimbilia kusema ni contradiction.

Lakini Mathayo kafuata ukoo wa Yesu kupia Solomon Mwana wa Daudi (Mathayo 1:6),

huku Luka akifwata ukoo kupitia Nathani mwana wa Daudi (Luka 3:31)!

Njia mbili tunazoweza kupatanisha kisa hiki:

a) Mathayo anafuata ukoo wa Yesu kupitia Yosefu baba yake mlezi huku Luka akifwata ukoo kupitia Maria mama yake. Ndomana Luka anasema "...na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli...." (Luka 3:23 BHN).

Yosefu anakuwa mwana wa Heli kupitia ndoa yake na Maria, hivyo Yesu anakuwa mwana wa Daudi kupitia Maria kisheria.

b) Au kupitia ile Sheria ya kurithi mke (levirate marriage), kwamba Heli na Yakobo walikuwa Ndugu, kisha Heli alikufa bila mwana kwahiyo Yakobo akamuoa mjane wake akamzaa Yosefu, kwahiyo Yosefu alikuwa mwana wa Heli kisheria.

Unaweza kutafiti zaidi.

Je maelezo haya hayapatanishi Injili hizo?

View attachment 3555634

Mfano mwingine, kulikuwa na malaika mmoja au wawili kwenye kaburi la Yesu?

Mathayo 28 na Marko 16 inasema mmoja. Luka 24 na Yohana 20 inasema wawili.

Mpelelezi J.W.W anakwambia hajawahi kusikia mashahidi wawili wa tukio wakikubaliana kila kitu.

Kwanza chochote atakachojibu shahidi kinategemea swali ulilomuuliza, ndomana anaweza asitaje jambo muhimu sana kwenye kesi, ukija kuumuliza kulihusu anakwambia hukuniuliza!

Na ndo anachoona kwenye kisa hiki cha malaika kwenye kaburi la Yesu. Waandishi wanaonekana kujibu maswali tofauti.

Mathayo na Marko hawajasema kulikuwa na malaika mmoja tu! Lakini Yohana na Luka wanasema waliwepo wawili.

Sasa kama kuna wawili si kuna mmoja! ! Hakijaharibika kitu.

Ili kuwe na contradiction, Mathayo na Marko waseme alikuwepo mmoja tu.

Ukisoma vizuri utaona Mathayo na Marko walikazia issue ya tetemeko na jiwe la kaburi.

Mathayo
anaonekana kujibu swali "Ni nini kilisababisha tetemeko"?

Marko anaonekana kujibu swali "ni nani aliondoa jiwe kwenye kaburi"?

Luka anaonekana kukazia fikra kupotea kwa mwili kwenye kaburi.

Yohana yeye alikazia fikra ripoti ambayo wanawake hao walienda kutoa.

J.W.W anasema anavyoona jinsi ambavyo waandishi wa Injili hizi hawakujihangaisha kulinganisha masimulizi yao Ili yafanane, ni uthibitisho kuwa masimulizi haya ni ya kutegemeka.

Hata yangefanana neno kwa neno, wazushi wangekataa pia! Wangesema hawa watu wametunga.

View attachment 3555636

4) Masimulizi kwenye agano jipya (na la kale) ni yenye kutegemeka kihistoria.

Kuna taarifa nyingi za zisizo za kikristo za kihistoria kwenye biblia. Yani kama utamsoma Josephus (36-100AD) ukamwamini na usijiulize mara mbili kama yuko sahihi au la, basi hata Injili unaweza kusoma bila kujiuliza.

Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka.

Kwanza Injili inakuwa na mamlaka zaidi kwakuwa yalionekana kuwa maandiko yenye thamani kubwa kwahiyo yalilindwa sana, yalitunzwa, yalisambazwa na kutafsiriwa!

Tofauti na maandishi ya wanahistoria kama Josephus ambaye hakuwa na watu waliofuatilia na kulinda maandishi yake! ! Kama kuna uongo amesema hakuna wa kumpinga!

Daktari Luka anasema: "....Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa." (Luka 1:1‭-‬4 BHN)

Mtume Petro naye anasema: "Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe." (2 Petro 1:16 BHN)

Mtume Paulo anasema: "....alizikwa, akafufuka siku ya tatu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa." (1 Wakorintho 15:4‭-‬6 BHN)

Biblia ni nyaraka zenye kutegemeka kabisa za historia.

Sio hekaya au hadithi!

Biblia sio Gilgamesh epic!

Biblia iliandikwa na mashahidi wa matukio halisi ya historia, wakishuhudiwa na mashahidi wenzao wa hayo matukio.

View attachment 3555637

5) Bila kusahau kuenea kwa ukristo karne za kwanza kulihusisha mateso makali sana kwa wakristo.

Walichohitaji ni kumkana Yesu halafu waepuke kifo waendelee na maisha yao,

lakini mamia na maelfu walikubali kuuawa: walisulubiwa, walipigwa mawe hadi kufa, walichomwa moto wakiwa hai, walitupwa waliwe na wanyama!

Kuna faida waliyokuwa wanapata kwa kushikilia hiyo Imani?

Pesa? Mamlaka? Wanawake?

Zaidi ya mateso na kudharaulika!

Au wote walikuwa wanaota?

Ni nini kilichowasukuma?

Na kuna tofauti ya mtu kukufuata kukuua kwasababu ya imani yako, na mtu aneyeenda kujitoa kafara kwasababu ya imank yake.

View attachment 3555638

View attachment 3555645

6) Tuna uthibitisho wa kutosha kabisa wa kukubali masimulizi ya Yesu bila shaka yoyote (beyond reasonable doubt).

Haiwezekani kuwa na uthibitisho bila shaka kabisa (beyond possible doubt).

Hiyo itahitaji kujua KILA KITU na haiwezekani kujua kila kitu.

Hakuna anayeishi maisha kwa kiwango hicho cha bila shaka kabisa maana hata nyumbani tusingetoka hadi mtu uwe na uhakika bila shaka kabisa kwamba hutogongwa na gari kesho, hutopigwa na radi, hutotekwa n.k.

Hata hukumu za wahalifu wabaya kuliko wote wanaohitaji kunyongwa hazihitaji uthibitisho bila shaka kabisa.

Nafasi ndogo iliyobaki kati ya uthibitisho bila shaka yoyote na uthibitisho bila shaka kabisa ndo nafasi ya maswali yako yasiyokuwa na majibu.

Ni nafasi ya wewe kuchukua hatua moja tu, ya IMANI.

Sio Imani kipofu: ni Imani yenye uthibitisho usio na shaka yoyote!

Kuwa na TUMAINI sio kuwa na matamanio ya kufikirika.

Ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia kutokana uthibitisho usio na shaka uliopata.

"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
Yohana.6.28‭-‬29.SRUV

"Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta."
Waebrania.11.6.BHN

"Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema."
1Wathesalonike.5.21.BHN

View attachment 3555655
Mkuu Asante kwa kutoa maelezo yaliyoshiba yakiambatana na vielelelezo muhimu katika swali hili, naamini aliyeuliza amepata majibu murua kabisa.

Kuna jambo nimesoma katika maelezo yako hapo juu naomba ufafanuzi zaidi hapa
Ukikuta tofauti kwenye taarifa fulani ya kihistoria (mfano issue ya sensa ya Quirinus wakati Yesu alipozaliwa) sio unampuuza Luka na kumsikiliza Josephus, maandishi ya Josephus hayana mamlaka yoyote zaidi ya Luka
Hapa ulikua unamaanisha kwamba Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius
Je hapa taarifa sahihi itakua ya Mathayo au ya Luka?. au huu utofauti ukauelezea vipi hapa?
 
Hapa ulikua unamaanisha kwamba Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode ambacho ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius
Je hapa taarifa sahihi itakua ya Mathayo au ya Luka?. au huu ugotauti ukauelezea vipi hapa?
Injili zote zinasema YESU alizaliwa kipindi cha mfalme Herode.

Sasa Luka anaongeza detail kuwa ni wakati mkuu wa mkoa (gavana) wa Syria alikuwa ni Quirinius, ndipo wazazi wa YESU walisafiri naye wakahesabiwe.

Huku Mwanahistoria wa kiyahudi Josephus anasema hiyo sensa ya wakati wa Quirinius ilikuwa mwaka 6AD! Mwaka huo mfalme Herode alikuwa ameshakufa miaka 10!

So which is which? Nani kakosea, Luka au Josephus?

Au tunapatanishaje hii tofauti?

Ndo point inakuja kuwa Luka (na vitabu vingine vya Biblia) vina mamlaka zote kama chanzo halali cha taarifa za kihistoria hata zisizo za kikristo. Kitabu cha Luka ni hati ya kihistoria, kama zilivyo vitabu vya Josephus.

Kwahiyo:

1) Kwanza Luka anasema alihoji mashahidi. Labda alienda kuhoji watu wa familia ya YESU, kama James the Just. Simulizi la Luka halipaswi kukataliwa mara moja.

2) Inawezekana Josephus alikosea. Watafiti wameonyesha Josephus amekosea mara kadhaa kuunganisha matukio, au alipangilia vibaya matukio kwenye maandishi yake, so inawezekana alihusisha sensa na tukio la 6AD kimakosa.

3) Watalaam wa Kigiriki wanasema Luka 2:2 inaweza kueleweka namna tofauti:

Luka 2:2 BHN - Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria.

i) kwamba kulikuwa na sensa nyingine ya mapema iliyohusiana na Quirinius, kwahiyo Luka na Josephus wanaongelea sensa tofauti.

ii) au ni sensa iliyotokea kabla Quirinius hajawa gavana wa Siria, sio wakati akiwa gavana, so Luka na Josephus wote wako sahihi.

4) Kuna na theory nyingine....

Inshort, hakuna suluhisho moja kamilifu.

Na hakuna ushahidi wa kutosha wa kusema kwamba Luka alikosea kihistoria.

Ni suala ambalo bado wanahistoria wanajadili.

Asante kwa ufafanuzi mzuri, ngoja nipitie na hio link uliyoniwekea hapo chini
 
I think a lot of people lack logical thinking which is one of the most important thing in human life.
 
Ndugu yangu Mungu akusamehe maana hujui ulisemalo. God is real and is the creator and the owner of the Universe. Believe it or not.
Pale dot blue

Tatizo watu mnajifanya mnajua sana you don't even understand how life works. I think the universe is too much big and we don't know even 5% of it ila Kuna watu na Imani zao wataleta ujuaji mwingi.

Better to work on facts than random conspiracy theories.
 
Kuna stori hadi sasa nikisikia naona kama hazina utofauti na mere stories. A lot of story kama, yesu alitembea juu ya maji, kufufua wafu, 🤔still doesn't make sense....View attachment 3552988
Mkuu suala la dini ni la kiimani (faith). Usije ukashawishika kutafuta ushahidi wa kisayansi utaumiza ubongo wako. Ni either uamini kwamba Mungu yupo na Yesu alikuja kutuokoa, au usiamini kabisa upambane na hali yako. Hii dunia ukichemsha akili kutafuta kila kitu uhalisia wake utapotea. Kwa taarifa yako vitu vingi hapa duniani they are just scam. Mfano, tunafundishwa kuhusu democracy, wapi wewe uliona kuna democracy? Kwangu mimi democracy is a scam. Tunadanganywa tuu, hata waanzilishi wa dhana ya democracy Marekani ni waongo hakuna democracy. Unaaminishwa katika jambo flani wewe unakuwa mfuasi alafu too late unakuja kujua kumbe uliingizwa chaka. Kuna mifano mingi naweza kukupa, hata ndoa ni scam tuu hakuna lolote ni mchakato uliojaa unyang'anyi, unyanyasaji, na udhalimu. If you believe in it endelea ila ukiitazama kwa jicho la haki hakuna haki katika ndoa ni utumwa
 
😂😂 Stori tu hizi.

Come up with facts.
Ndiyo ni story lakini siku utakapotuaga na kwenda njia ya wanadamu wote utakutana na aliyekuumba. Unfortunately it will be too late for you. Facts si angalia juu nani aliyeziumba hizi mbingu.
 
Back
Top Bottom