Kwa mtu alie na basic knowledge ya udukuzi au ni advanced hacker huwa wanafanya hivi, inaundwa payload kwanza ambayo wanajua wao wameweka nini ili kusaidia kupata infos kwa victim, sasa kinachofanyika ile payload inapachikwa kwenye either link, apk, photo au kitu chochote ambacho victim anaeza vutiwa nacho! Akishamaliza hivyo anakutumia kama ni link basi inakua na maelezo mengi ya kukuhamasisha ui click (refer kwa zile affiliate program links au zile sijui unaambiwa click link kupata gb30 za internet mitandao yote duniani nafikiri ushakutana nazo links za design hiyo)
Hapo uki click link au ku install app labda kakutumia ile payload inajifungua na kujipa permissions automatically au kama umeipa app permissions nayo unakua umejikaanga pia inafanya kazi chap kuchukua infos ilizo codiwa kuzibeba mfano IP Address, Mac Address, IMEI no, Phone Contacts, Model ya simu nk yaani inaeeza chukua infos zote muhimu kwenye simu yako au kifaa kingine unapokua connected to kwenye internet.
Sasa ikisha kusanya hizo infos inampa mhusika kinachofata nafikiri kama ana lengo zuri au baya na wewe basi utajua hujui kama kapata contacts wako anaweza mpigia mmoja wa rafiki/ndugu wa karibu akamuuliza mawili matatu kuhusu ulipo au kama ni advanced hacker anaweza kukamilisha hitaji lake kupitia IP Address (kama huku tumia VPN atapata real location yako) au kupitia Mac Address. Hizo payloads huwa wanaunda kwenye termux (kwa Android smartphones) Kali Linux au Andrax hizi ni platforms za computer.
Cha msingi na sekondari epuka ku click links zisizo na maana au zisioeleweka, make nyingine ni za ma script kiddies (vidukuzi vinavyojifunza na kutaka kujaribu practically) so unaweza jikuta ume formatiwa kifaa chako au kuibiwa infos muhimu zikatumiwa vibaya kukuchafua au kukudharirisha.. Pia epuka ku install apks hovyo, unakuta unatumiwa apk ya whatsapp ina kb 300 au mb 3 naww una install tu hujiulizi au hujui apk ya whatsapp ina ukubwa wa mb zaidi ya 50+mb..