Shetan haonekani ila roho itendayo uovu ambayo humuingia mtu...
Hata malaika ni roho itendayo mema ndio maana Catholic huita roho mtakatifu
Ni nafsi zisizoonekana
Lengo si kubishana Bali kubadilishana uzoefu
Kabla ya kujibu hoja yako ngoja nigusie kidogo kuhusu roho mtakatifu WA Roma au Ukristo Kwa ujumla
Yesu alipoondoka alisema atakuja huyo ambaye atasema kweli,kuhusu hukumu na sheria.
Kama Yesu alikuja kama mwili INA maana hata ambaye angemfuata Angekuja kama mwili ili adhihirike duniani kote na kusadiki Yale aliyosema Yesu,lkn inakuwaje huyu aje Kiroho na kuwa sehemu ya watu wachache Tu?
Je mbona Yesu alikuwa sehemu ya watu wengi, je huyo roho ameeleza kuhusu hukumu na sheria kama alivyosema Yesu?
Endelea kutafakari juu ya hayo....
Sasa turudi kwenye jambo letu.
Malaika ni mwili pia,na wao Kwa mujibu wa Qur'an wameumbwa na mbawa mbili,wengine tatu na wengine nne, wakati huo huo hao ambao unasema wanaamini Malaika ni roho utakuta wamechora picha za malaika WA kike wakiwa na mbawa.
Ila kuna pazia Kati ya Malaika,majini na wanadamu, Malaika huwaona majini,Ila majini hawawaoni Malaika,majini wanatuona Sisi Ila Sisi hatuwaoni majini.
Nije kwenye swali lako la awali.
Malaika na majini ni tofauti ndio maana ,Malaika wameumbwa na Nuru na majini na Moto kama ambavyo Sisi tumeumbiwa na Udongo,kwahiyo kizazi cha majini ni cha maji kama Sisi,hapa namaanisha shahawa au manii.
Kwahiyo asili ya Malaika na majini/Ibilisi ni tofauti toka kuumbwa kwake.
Malaika hawana jinsia hata kidogo na hawana matamanio kama majini na wanadamu