Hivi kuna watoto waliosomeshwa shule za kulipia na ni jobless?

Basi tumepishana kidogo hapa. Mm nilikuwa narejelea kilio cha Irene Uwoya ambaye alikuwa analalamikia kushindwa kuendelea kulipa ada kubwa kwenye international school. Ambapo akadai mwanaye kamshuri amhamishe lkn yeye Uwoya anaona itakuwa siyo sawa.
 
Basi tumepishana kidogo hapa. Mm nilikuwa narejelea kilio cha Irene Uwoya ambaye alikuwa analalamikia kushindwa kuendelea kulipa ada kubwa kwenye international school. Ambapo akadai mwanaye kamshuri amhamishe lkn yeye Uwoya anaona itakuwa siyo sawa.
Hiyo ya Uwoya siifahamu, nilikuwa nasemea ya jumapili mtoto mmoja mzaliwa wa huko Mara nadhani.
 
Kwani huko kwenye shule za kulipia wanachosoma ni connected na ajira.
 
Mi sijasoma private mkuu
 
Usikariri maisha,alicho nacho kichwani kwake na maisha anayoishi ni mepesi kuliko wale kayumba waliotumia muda wao mwingi chimbo😁
 
Watanzania ni wasahaulifu sana[emoji35]
Ina maana huyu mtoa mada kasahau kwamba mwaka 2015 kurudi nyuma shule zote za sekondari zilikuwa za kulipia?

Anasahau kwamba shule zote iwe serikali au binafsi zilikuwa na ada na michango mingine...na ... Hiyo maana yake n kulipia?

Au bado anamezwa na neno KULIPIA lililokuwa linatumiwa enzi za mwalimu wakati shule za umma zote kusoma ilikuwa bure[emoji848][emoji1787]
 
msalimie sana
 
Mi namfahamu mmoja, kazi hana ila bado maisha mazuri anayo maana wazazi walijipanga kwelikweli, nafikiri wazazi wake walitafuta hadi za vitukuu, nyumba ya masaki wameivunja wametengeneza nyumba za kupangisha tatu na kila mpangaji analipa dola 800/month
 
Mbona wapo wengi tu, wengine ni walinzi
 
Shule ya kulipia? Kulipia bei gani??

Maana kuna shule wanalipana kwa kilo za mchele na magunia ya mahindi wanapokea.
Huna cash peleka kiroba cha mchele, huna cash peleka kuni vipi na hao pia wako humo au mnawaongelea hawa wa Feza, Tanganyika na st Francis??.
 
Pole aiseh!

Kuna baadhi ya skills unazitumia kwenye huo udalali na ulizipata chuo hasa Lugha na psychology kuwasoma wateja!Endelea Hadi ufungue kampuni ya udalali!!

Utajiri hauna kazi maalum ya kuanzia,popote pale!

Big up!
 
Huyo anajikweza! Hakuna jobless hata mmoja aliyesoma shule za kishua. Labda awe na biashara kali tena kubwa inayozalisha au anafanya telework na haishi kupaa majuu! Vijana punguzeni kujikweza na masifa! Mnajiharibia wenyewe! Kwanza wanaosoma hizo shule Mama zao na Baba zao ni Vigogo na Vibopa.

Wataishiaje kwenye udalali?! Labda wafungue kampuni za udalali ambazo zitaendeshwa kisomi zaidi na teknolojia mpya ya kujua watu wa dunia hii ya leo wanataka nini.

Namfahamu mmoja alifanya kazi Stanbic bank miaka takribani mitano mpaka nane kama sikosei, alikuwa na nafasi nzuri sana! Kama hakuwa head of credit, basi alikuwa mtu wa marketing... Akafungua kampuni yake ya Real estates agency, Mbezi beach huko.... akawa anapiga kazi na mabenki kusongesha collateral za wateja pindi walipokuwa wanachukua mkopo. Ana connection za BM's wa benki kibao nchini, deal zote za kusongesha mali za walioshindwa kulipa madeni ya benki anapewa mchizi. Juzi kati nikaona kapiga picha na C.E.O wa TANZANIA COMMERCIAL BANK (T.C.B) nikasema hapa kuna jambo.

Jamaa ana pesa hatari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…