Hivi kuna watoto waliosomeshwa shule za kulipia na ni jobless?

Wapo sana, but most of them wana miss concept of education. The idea ilikuwa ni kukuoa knowledge sio kukupa kazi.
Ni huku tz kuanzia mashuleni unamuaminisha mwanafunzi kuwa atakuwa hivi atakuwa vile kumbe huko duniani nafasi hamna au mahitaji yamebadilika

Swali kwa mamlak why hawabadilishi mitaala iendane na current market?
 
Angeenda kusoma chuo UK or USA
 
We jamaa unaonekana una vituko sana! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
 
Wewe umeweka wazi mambo na umeelezea kwa ufanisi mkubwa ingawa ni maneno machache.

Watu wanaropoka sana! Yale mashule ni Next-level! Wanaosoma huko mababa na Mamama zao hawana njaa! Mostly ni wamiliki wa makampuni na wameajiri watu na wanawalipa vizuri, wengine ni viongozi wetu. Watoto wao watakosaje kazi na kuishia mitaani?!

Kama wanazungumzia hizi private za kihuni haya sawa! πŸ˜‚πŸ‘
 
Mleta mada anasemea private za kawaida.
Kumbe hizi teremka tukazeπŸ˜‚... Hapo sawa!

Hizi za kawaida wazazi tunalipa kama kubahatisha tu! Tunacheza bahati nasibu, akijitambua huko na akafanya vizuri, huenda atapata chuo kizuri na kujitengenezea connection yake huko mapema kutokana na watu atakao kutana nao ili na yeye angalau hata aje kuambulia kanafasi ka ukarani akunje hiyo laki tatu na nusu akapange mwananyamala ajitafute kimaisha atuondolee vurugu nyumbani πŸ˜‚πŸ‘
 
Jamaa yangu sana kapiga AMANI(peace) miaka ya nyuma sana(primary&seconday), advace kasoma shule moja maarufu sana ukanda wa Dar, chuo kaenda India. Now ni dalali wa moto sana.
 
Tatizo ni wahitimu ni wengi kuliko ajira πŸ™„
Creation of new jobs iko na matatizo πŸ™„
 
Wajinga wachache huwa wapo
 
Tena hao ndo wengi uki compare Na ambao walisoma za kawaida
 
Mimi nimesoma shule za serikali zile za chini sana. Usisikie maneno ya wakosaji, sijawahi ona mtu kasoma private za gharama kubwa alafu analia njaa. Labda afanye makusudi kama kuvuta bangi na kuendekeza pombe.
Hadi anasoma private maana yake huyo anatoka familia yenye pesa hivyo ana network ya pesa huyo hata akikwama ajira anawekwa kwenye miradi ya familia
 
Education is better than....
Hii ili watu ama jamii igeukie kugharimikia elimu ,wakaja na ukiona elimu ghali jaribu ujinga.
Am sure elimu halisi haipatikani shuleni.
Niambie matajiri wote Kama wanachojivunia kuwa walifundishwa shuleni. Ma profesa wa uchumi wanafundisha stock investing wanakuja na earning profit ratio Ila hawezi kuwekeza kwa kutumia theories zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…