Hivi kuna watu wapo humu na hawajawahi kabisa kufika jijini Dar es Salaam?

Hivi kuna watu wapo humu na hawajawahi kabisa kufika jijini Dar es Salaam?

Wewe baada ya kufika pengine na kuishi imetuzidi nini sisi ambao hatujafika na tunaishi Tandahimba na Simiyu?

Wewe umewahi kufika kwetu?

Utoto
Muulize kashawahi fika Gambosi au Lagangabilili au kule Ikungulyabashasi au anapasikia Nkololo?
 
Nimewaza tuu eti Kuna watu mpo humu mnaisikia Dar redioni tuu?

How come? Yani una miaka 30 plus dar hujawahi kufika??
Dar ni nini? Yaani kufika Dar unaona umemaliza!!!! 🙆🙆🙆
Kufika kwenyewe Dar umefika baada ya dada yako kumbembeleza shemeji yako ili angalau uende ukasafishe macho. Halafu unaona uko juu🤣🤣🤣
Watu bwana, mkishashiba kiporo kwa shemeji zenu mnapoteza akili.
 
Wakishua ukimwambia Dsm michesho atashangaa Sana.

Dsm ukiwa na Pesa ni Pepo ndogo, ukiwa Huna NI kuzimu.

Mimi bado naparangana
Wanaofurahia hilo jiji ni wachache mno tena wale wanaotembeaga na ving'ora, wafanyabiashara wakubwa,, tuliobaki kero zipo palepale,

Foleni, msongamano, harufu, joto, gharama kubwa za maisha ya kila siku, huduma mbovu za kijamii, isipokugusa kero 1 au 2 kati ya hizo basi utaenjoy sasa kuna wale hizo kero zote zinatuhusu na tuko wengi
 
Wakati wewe unaona kufika kwako Dar umemaliza, vile vile kuna mwamba anakushangaa umefikaje miaka 40 hujawahi Fika ama SA ama UK, ama US, china au Dubai. m
Maisha ni fumbo mkuu kirefu kwako ni kifupi kwa mwenzio.
Kuna watu mpaka wanakufa hawajawahi fika Makao makuu ya Mkoa anaoishi. Dunia ndivyo ilivyo.
Dah huitaji visa wala passport wala laki tano,kama hujafika Dar wewe ni mtu wa kustaajabisha sana
 
Wanaofurahia hilo jiji ni wachache mno tena wale wanaotembeaga na ving'ora, wafanyabiashara wakubwa,, tuliobaki kero zipo palepale,

Foleni, msongamano, harufu, joto, gharama kubwa za maisha ya kila siku, huduma mbovu za kijamii, isipokugusa kero 1 au 2 kati ya hizo basi utaenjoy sasa kuna wale hizo kero zote zinatuhusu na tuko wengi
Sio kweli,ukifeli juenjoy maisha Dar ujue hujatumia brain yako vizuri,sina hela nyingi kihivyo ila kwa Tanzania Dar ni the best to live ni peponi kabisa kwangu
 
Sio kweli,ukifeli juenjoy maisha Dar ujue hujatumia brain yako vizuri,sina hela nyingi kihivyo ila kwa Tanzania Dar ni the best to live ni peponi kabisa kwangu
Upo kwenye list ya wale wenye ving'ora hongera😂😂
 
Back
Top Bottom