Hivi Kwa hii Ada ya Udaktari, watoto wa Masikini watatimiza ndoto zao kweli?

Ccm ni mafii
 
Watanzania mnapenda sifa mnaacha kupeleka watoto kozi hapo Mweka ya Utalii ikiwezekana mtaweza kuwa na Kampuni ya Utalii ambayo vizazi na vizazi watakula matunda yake bado mpo na maisha ya Zamani ya kufikiria watoto wasome waendelee kupata tabu...
 
nchi ya imani na miujiza
 
Hapa ndipo watu wanapoenda nje ya malengo yao na kuiacha kada waliyoipenda.Nakumbuka maumivu tuliyopitia 2016 mdogo wangu toka o level hadi a level alikuwa anapasuwa vema mathe,phys,chemia lakini kutokana na mikopo kuwa tight ikambidi chuo aingye kusoma education ili kupata mkopo.
 
Udaktari ukiupeleka NGO ya kimataifa utakuwa una uhakika wa kulipwa mara 3 ya mshahara wa serikali.
 
Watanzania tujifunze kuwapigania watoto wetu tuliowazaa wenyewe tusitumie umaskini kama kichaka cha kulia lia

#beba hata bunduki kasake pesa
 
Watanzania tujifunze kuwapigania watoto wetu tuliowazaa wenyewe tusitumie umaskini kama kichaka cha kulia lia

#beba hata bunduki kasake pesa

Unaweza niambie ni kitu gani kinafanya Ada ya Udaktari iwe kubwa katika nchi yenye watu masikini ambao chakula tuu kinawasumbua?

Watanzania wanaweza kupigania watoto wao lakini kuna gharama hazishikiki,
Kijana anaakili, anandoto ya kuwa Daktari anasoma Kwa moyo alafu anakuja kuwa disappointed akifika Chuo.

Serikali ndio mzazi Mkuu. Yeye ndiye anapaswa apiganie watoto wake, ambao ni wananchi
 
Hii shida ilikuja pale serikali ilipoingia kichwa kichwa kuanzisha bodi ya mikopo kutoa pesa kwa kila mwanafunzi, wakati awali waliokuwa wanapata ufadhili wa serikali ni wale waliokuwa wamedahiliwa vyuo vikuu vya umma pekee. Hii ilileta mzigo mkubwa kwa serikali maana vyuo binafsi vilianzishwa hadi vichochoroni. Kwa hiyo utaona kwamba kinachotakiwa kufanywa ni kurudisha utaratibu wa awali ambapo serikali inatoa ufadhili wa wanafunzi kwenye vyuo vyake vya umma kwani hivyo ndo vinaendeshwa kwa kodi za wananchi. Hii itakuwa mkombozi hata kwa watoto wa wanyonge wenye uwezo mkubwa wa kiakili kuweza kupata ufadhili wa serikali wanapokuwa wamedahiliwa kwenye vyuo vikuu vya umma.​
 
Ada iko sawa ...mwisho udaktari uwe kama uwalimu kila mtu ana soma tu
 
Mbali na huduma uganga inalipa bado, iyo laki 9 kama salary take-home kama ulipata mkopo lakini kuna fedha nyingi hapo katikati .kuna posho za vikao kazi,kuna posho za extraduty, kuna posho kazi nje ya kituo nk..
Kasome uhasibu miaka 3 bach ukalipwe laki 7 kabla ya makato ndio utaelewa nachokizungumza hapa.
 
Hiyo ada ni kwa vyuo binafsi mkuu..kwa vyuo vya serikali gharama ipo chini mnoo.
 
Hiyo ada ni kwa vyuo binafsi mkuu..kwa vyuo vya serikali gharama ipo chini mnoo.
Hivi vyuo binafsi hivi aisee ni balaa. Mwaka 2010 nilipata MBBS hapo IMTU mbezi beach, sasa enzi hizo tuition fee ilikua ni 4500$ mixer makolokolo mengine ilikua inasoma kama 8m per year. Ndio ndoto za Udaktari zikapoletea hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kozi za vyuo zenye umuhimu ndo gharama kubwa kuliko hizo za sanaa na biashara. Waweke mpango maalum wa kuwawezesha ili tuzalishe kada muhimu.
 
Huku ni kuhalalisha kuwa masikini..!!!
 
Pole sana mkuu. Lakini natumai haujutii ulipo sasa hivi.
 
Pole sana mkuu. Lakini natumai haujutii ulipo sasa hivi.
Sijutii ila kwa kiasi fulani ndoto za kukosa nafasi ya kile nilichokua nakipenda zaidi maishani zinanitesa sana. Ila bottom point ni kuwa nilipo paniwezesha kimaisha na familia kiujumla basi nasemaga tu Mungu ni mwema
 
Sijutii ila kwa kiasi fulani ndoto za kukosa nafasi ya kile nilichokua nakipenda zaidi maishani zinanitesa sana. Ila bottom point ni kuwa nilipo paniwezesha kimaisha na familia kiujumla basi nasemaga tu Mungu ni mwema


Yeah ni kweli. Mungu anamakusudi yake.
Katika maisha lazima uwe na options zaidi ya moja, ndoto zaidi ya Moja mpaka tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…