Hivi kwa nini wafanyakazi wengi wa halmashauri hawana uweledi?

Hivi kwa nini wafanyakazi wengi wa halmashauri hawana uweledi?

Mkuu ulichokiona Ubungo ujue kina-reflect hali ya halmashauri zote za Tanzania ​
Ubungo imezidi wengine. Kwanza ukifika unakuta watoa huduma wamekasirika halafu wanakuona kama mtuhumiwa fulani hivi.
Kama utakua na sherehe halafu ukakodi ukumbi, kuna kodi fulani ambayo unatakiwa uilipe pale manispaa, kwa mtu wa kawaida utafikiri ukienda kulipa kodi utapokelewa na mikono miwili, hiyo siyo Ubungo kaka, utazunguushwa mpaka uzunguushike ndio upate makadirio, then upande gorofa ukalipe, then uende kwingineko ukapewe risiti. Kumbuka huko kote una deal na watu waliokasirika.
Kama ni mtumishi say mwalimu, ukienda pale uende na kopi za barua zako zote na vyeti vyako vyote maana utakaye mkuta hawezi ku access file lako kwenye komputa au hajui au jeuri na kumbuka amekasirika utadhani anafukua kaburi la mganga.
Au labda wafanyakazi wa pale wameokotwa okotwa tu. WHY???
 
MTOA MADA ANAONGEA JAMBO LA UKWELI KABISA MIMI SIPO HALMASHAURI ILA WATUMISHI KARIBIA WOTE WALIOHAMIA NINAPOFANYIA KAZI HAWAJIWEZI KABISA. UNAWEZA KUKUTA GRADUATE HAJUI KUTUMIA KOMPYUTA KABISA HADI UNASHANGAA ALIPITAJE HUKO CHUONI, NJOO KWENYE KUFANYA KAZI SASA HAMNA KITU KABISA.

PIA KWA KUONGEZEA GRADUATES WENGI AMBAO WAMESOMA HAPA NCHINI ILA HAWAKUSOMA UDSM, SUA, DIT, MZUMBE, ARDHI NA MUHAS NI VILAZA WA KUTUPWA YAANI NI ZERO BIN SIFURI. NIMEANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUONESHA MSISITIZO.
 
Kwenye halmashauri zilizo mikoani kuna hii kitu. NDUMBA , wenyewe kwa wenyewe wanarogana usiombe, halafu rushwa ya ngono.
Ukimkuta mtu wa halmashauri yuko kwenye channel ya pesa nje ya mshahara ujue kabisa ana consultant wake (mganga wa kienyeji) otherwise hatadumu kwenye hicho cheo au hapa duniani.
Kada zenye washirijina tanzania inaongoza polisi, then halmashauri then mahakama
 
We dogo hajitambui. Tuanzie kwenye ajira, Halmashauri haziajiri. Management ya utumishi na utawala bora ndio wanaajiri. Mishahara ya Halmashauri wengi TGS japo kuna wengine wenye kada tofauti salary scale zao zinatofautiana na TGS humo humo ndani ya Halmashauri.

Halmashauri kuna wataalamu wengi kuanzia afya, Elimu, Kilimo, Uchumi, Ujenzi n.k na salary scale ni tofauti.

Acha kupotosha. We umeleta Tangazo la Ajira ndogo ndogo ambazo Halmashauri wanaomba kibali toka Management ya utumishi wa umma kuajiri na mishahara haitoki Halmashauri inatoka Hazina.

Nilianzia Ajira Halmashauri mengi uliyoandika ni ya kupotosha kwa chuki zako.
Ulioandika hapo kwamba wanaajiri sio kweli wao wanatoa vibali vya ajira na wanaoajiri ni Sekretarieti ya Ajira. Pia, kuna kada ambazo huajiriwa moja kwa moja na Halmashauri ambapo Halmashauri hupewa mamlaka hayo na Sekretarieti.
 
Umeongea kwa ujumla na hadi mwisho hoja yako haijulikani. Uandishi huu unadhihirisha kuwa shida iko upande wako
Uzuri ni kwamba kuna shuhuda zimetolewa na wachangiaji wengine wengi kwenye huu uzi kuwa watumishi wa halmashauri uweledi na uelewa ni mdogo sana​
 
Nimepata nafasi ya kutembelea halmashauri mbalimbali hapa Tanzania nilichogundua watumishi wengi ni vilaza sana kwenye utendaji.

Yaani idara zote za halmashauri unakuta watumishi hawana weledi katika kazi ufanisi ni zero kabisa.

Nafikiri ifikie pahala serikali iangalie kwa kina vigezo vya mtu kuajiriwa kama mfanyakazi wa halmashauri kuna madudu mengi sana.
​
Changamoto ni kwamba,huwa unaenda na matarajio yako kichwani bila kujua unakutana na akina nani.You need some perfections within a vacuum cleaner!Tuliza wenge.
 
Mkuu umekosea sana. Huko Halmashauri ndiko kuna watu wenye uwezo, walipata bila vimemo isipokuwa hawa Godfathers wa kuwapeleka BOT, TPA nk.
Mazingira wanayofanyia kazi ikiwemo kukosa mafunzo ya Umahiri kazini, kuishi na Wanavijiji, kuongozwa na Madiwani wanaojua kusoma na kuandika, kukosa exposure na Ushindani kumewafanya waduamae. Lkn vichwani Halmashauri kuna Dhahabu ambazo zimekosa tanuru la kuzichoma zing'ae japo vilaza wapo lkn siyo kwa kiwango hicho.

Vilaza wapo taasisi kubwa kubwa ambazo hijawahi skia interview wala tangazo la kazi na wana wamejazana jiulize wametoka wapi
LGA wanafanya kazi kisiasa sana....kule hakuna weledi mkuu...ukienda na weledi wako hutoboi! Na Mungu Magufuli ndio alizidisha zaidi Hali hii ,siku hizo na Miungu Watu MaDC nao.wamekuwa Wanyapara! Kwa kifupi mfumo wa Utawala wa nchi hii ndio kikwazo cha Maendeleleo!
 
Shida sio wafanyakazi.
Shida ni Serikali Yenu, Na sera duni za Kazi.

Imagine, Mtu anafanya kazi Office haina WIFI, hana Laptop ya kwake binafsi au hata ya Office, Hakuna Proffessional development yeyote, Hakuna trainings, Hakuna motivationa Ni Ujuha tu na kufokeana, Office hazuna budget.

Hao mnao waita Vilaza walisoma pamoja na wafanyakazi walio ajiriwa kwenye mabank, Migodi na Taasisi nyingine Private na wanaonekana wana weredi. Ushawai jiuliza kwanini?

Kama Hujui kwanini, Mimi ntakupa sababu
1. Wako well equiped na Vifaa vya kufanyia kazi,
2. Wanapewa training mbali mbali, kuongezea uelewa na maarifa ya kazi
3. Wanakua rewarded & appreciated for their work
4. Wanalipwa vizuri, hivyo wanajituma kazini.
5. Kuna perfomance evakuation, hivyo usipofikia targets kina kuramba
6. Kuna promotion ukifanya Vizuri, Wakati upande wa pili ili uwe promoted inatakiwa uwe chawa

Hayo ni baadhi ya mambo yanayotofautisha Wafanyakazi wa Halmashauri na Taasisi nyingine. Hata huko Serikali Ni halmashauri ndo wanatoa huduma mbivu kuliko wengine na malipo yao ni kiduchu sawa na hakuna
 
Nimepata nafasi ya kutembelea halmashauri mbalimbali hapa Tanzania nilichogundua watumishi wengi ni vilaza sana kwenye utendaji.

Yaani idara zote za halmashauri unakuta watumishi hawana weledi katika kazi ufanisi ni zero kabisa.

Nafikiri ifikie pahala serikali iangalie kwa kina vigezo vya mtu kuajiriwa kama mfanyakazi wa halmashauri kuna madudu mengi sana.
​
Mazingira yanawameza wanatoka na energy ya kutosha chuoni wakiingia huko wanakutan na urasimu usio na kifani hivyo wanakata tamaa
 
Yoo! Trauma ambayo huwa nabaki nayo nikiwa na deal na hawa watu kwa siku kadhaa mara kwa mara sijui niielezeje.

Hawana haraka, hawajui emergency, hawajui priority zaidi ya kula na kutafuna tafuna ofisini muda wote.

Kwenye mbanga zangu zote dada mmoja wilaya ya Kasulu ndiye alinishangaza, aliact fast, matured and professionally, Kidogo nimwambie dada haufai kuwepo LGA. Probably unafaa kuwepo private sector.

Ndugu zangu waTz kuna siku tutabadilika kweli? It’s 2025!
 
No Reform no Election....Watu hawaelewi kuwa mfumo wa Utawala ndio chanzo cha haya yote! Itakiwa mtu analalamika huduma.mbovu za afya .....kesho yake unakuta anashabikia uozo wa CCM😭
 
Mkuu umekosea sana. Huko Halmashauri ndiko kuna watu wenye uwezo, walipata bila vimemo isipokuwa hawa Godfathers wa kuwapeleka BOT, TPA nk.
Mazingira wanayofanyia kazi ikiwemo kukosa mafunzo ya Umahiri kazini, kuishi na Wanavijiji, kuongozwa na Madiwani wanaojua kusoma na kuandika, kukosa exposure na Ushindani kumewafanya waduamae. Lkn vichwani Halmashauri kuna Dhahabu ambazo zimekosa tanuru la kuzichoma zing'ae japo vilaza wapo lkn siyo kwa kiwango hicho.

Vilaza wapo taasisi kubwa kubwa ambazo hijawahi skia interview wala tangazo la kazi na wana wamejazana jiulize wametoka wapi
Working culture ndio tatizo namba moja huko makazini kwenu.
 
Back
Top Bottom