Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Huyu au mwenzake ndio atakuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Atatakiwa awe na mawaziri vivuli. Atatakiwa atoe majibu ya Upinzani kila Bajeti ikiwasilishwa. Atatakiwa awe mjumbe wa kamati nyingi tu akiwakilisha upinzani. Hapo bado kuwakilisha wananchi wa jimbo lake pamoja na chama chake Bungeni. Akiweza vyote hivyo atakuwa jembe kweli.

Amandla...
 
Mbunge anadhaminiwa na chama sio wananchi. Hta bungeni mnakaa kwa mfumo wa kichama, same to kamati. Na ndio maana Leo Mbowe akimfuta uanachama huyo dada ndio ubunge wake unafia hapi hapo.
Hata akimfuta, Spika na Tume ya Uchaguzi watakataa kutambua kuwa amefutwa. Kama amewekwa kama boya, hamna namna watakubali akose ubunge.

Amandla...
 
Sasa atakuwa na raha gani wenzake wote wanalia yeye peke yake anafurahia?na je anaamini wenzake wote Tanzania nzima wameshindwa kihalali kama sivyo aungane na wenzake kushinikiza watawala kutopoka tena haki ya wananchi ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aunge juhudi mkono, uchaguzi urudiwe, yaishe, mbona rahisi sana. Kessy aweza kuhamia naye upande wa pili.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 

Hajatumwa na wenzake Diba ametumwa na wananchi. Akijiuzulu atakua amevunja mkataba na hatawatendea haki aliowaahidi kuwatumikia miaka5
 
Kujiudhuru kutaonesha hayupo kimaslahi. Mtu mwenye akiki timamu hawezi furahia kwenda bungeni wakat wenzake wamefanyiwa michezo michafu

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
No no no. Eti kutaonyesha hayupo kimaslahi. Ni mbunge yupi ambae hayuko kimaslahi?

Kuanda aende.. lakin atarajie harrasment kubwa kutoka kwa ccm. Hapa chama lazima kiweze kumfariji or else.. anaweza aka give up.
Aendelee ameshinda ni haki yake.
 
Mbunge anadhaminiwa na chama sio wananchi. Hta bungeni mnakaa kwa mfumo wa kichama, same to kamati. Na ndio maana Leo Mbowe akimfuta uanachama huyo dada ndio ubunge wake unafia hapi hapo.
kiongozi wa upinzani bungeni...ila nawaza kina mbowe na wengine kina zito wavifute tu vyama vyote wakibakize ccm waingie huko..alafu tuone hao wanainchi watafanyajwe....watalimia meno.kujenga lami kwa mikono na kupasua milima kwa visigino..tz itakuwa utumwani....dawa mtakula mitishamba mtafanya kazi kwa mijeledi...sijui kama kuna mtu anafikiri kama mimi tuumalize upinzani..
 
Mbowe alikua ni:
  • Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni
  • Mwenyekiti cha CHADEMA Taifa
  • Mbunge jimbo la Hai
  • Mjumbe mkuu kamati ya upinzani
Na bado vyeo vingine vidogo vidogo alikua navyo.
Kwahyo huyu Mama aachwe akafanye wajibu atakaokua nao hata kama wako wawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…