Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Miaka 60 baada ya uhuru bado tunayaogopa mapori yetu wenyewe kweli? Kwa nini kusiwe na network hicho kipande wakati hiyo ni highway? Sina lengo la kukushambulia wewe personally but nataka hoja zangu ziwafikie wahusika kwa sababu hatuwezi kupiga maendeleo kwa staili hii.
Wee jamaa ni kiazi sana unang'ang'ania miaka 60 ya Uhuru tu VP nchi kama marekani wamepata Uhuru miaka 200 iyoyopita ila bado matukio ya kihalifu yanatokea na apo wanateknolojia kubwa kuzidi yoyote mapori ya skonge ni makubwa kieneo ipatikanaji was huduma za kidharura ni mdogo sana na ni rahisi kuvamiwa ila huelewi nakumbuka nilikuwa natoka tabora kupitia skonge kwendaa chunya sijui kama ile barabara imetengenezwa maana ilikuwa 2010 saivi ila ile barabara ina pori bays sana
 
Suala la ajabu sana. Lami ni nzuri na mpya kuanzia hapo.Sikonge kuna ka bar hapo kana piga piga mziki.pabovu kinoma hapo.
 
Dereva wenu ndie Mzembe. Angefika hapo kabla ya saa 3 usiku mngetoboa sasa Hapo Sikonge madereva wanapenda kulala kwa maksudi maaana wameoa Warabu koko wapo kibao so dereva anachelewa maksudi kufika ili akahudumie nyumba ndogo yake.

Siku nyingine Ongea na afande kiume uone ka hamjaruhusiwa.
Dah !...
 
Ulichosahau ni kwamba polisi nao ni binadam na wanakufa pia, wakimalizana na askari wanakuja kutembeza kifiro kwa abiria sasa
Kama trained askari wanaogopa ina maana hata uwepo wao hauna maana yoyote basi, naamini wakiwepo askari na njugu za kutosha watashika adabu.
 
Tunayo majeshi mengine mkuu, na nimeshaona JW TZ wakisaidia kwenye mambo mbalimbali nchini, sembuse hili la kuwadhibiti hawa vibaka kwenye mapori?
Unajitahidi kuwaeleza, ila watu wameweka pamba masikioni. Hawaoni hata nguvu ya hoja yako. Serikali ilifanikiwaje kukomesha issue ya Kibiti?
 
Mawazo chanya tuliyoleta ndio yalifanya hiyo bara bara ikawekwa lami. Enzi izo nyie mlikuwa mnawaza utelezi tu...
Hatuzungumzii mawazo Chanya kwenye barabara kuwekwa lami, tunazungumzia mawazo Chanya ili tuondokane na hili zuio hapo Sikonge... Nini faida ya kuwa na barabara ya lami ya mabilioni ikiwa utazuia watu wasisafiri masaa 24 ili kujenga nchi yao?
 
Miaka 60 baada ya uhuru bado tunayaogopa mapori yetu wenyewe kweli? Kwa nini kusiwe na network hicho kipande wakati hiyo ni highway? Sina lengo la kukushambulia wewe personally but nataka hoja zangu ziwafikie wahusika kwa sababu hatuwezi kupiga maendeleo kwa staili hii.
Suala la network sio la serikali bosi, na la network providers, wakiona kuna uhitaji na ina tija kwenye biashara zao wataweka. Kwa mfumo wetu wa minara unahisi unahitaji minara mingapi kuhudumia pori zima? Mbaya zaidi itakuwa inaendeshwa na generators za mafuta, nani atafanya biashara kichaa hiyo.
 
Urefu wa Hilo pori kufuata hiyo barabara ni kilomita ngapi!?..panatakiwa vituo vingapi vya ulinzi vya kuweka Askari!?..au escorts wangapi kwa kila gari!?..unajua kwamba polisi Haina Askari wa kutosha!?..ipi cheap kati ya kuzuwia usafiri usiku na kujaza Askari kwenye Hilo pori!?
Unafahamu kwamba nchi hii ina majeshi mengine zaidi ya Polisi? Unafahamu kwamba majeshi mengine pale inapohitajika amiri jeshi mkuu anaweza kutoa maelekezo yakaimarishe ulinzi au kufanya kazi yoyote nyingine? Kuhusu urefu wa hayo mapori jiongeze uingie Google Earth [emoji289] utajua juu... Narudia tena na tena huu si wakati wa kuwapigia magoti wahalifu kwa kuzuia watanzania kutosafiri usiku. Wahalifu wanatakiwa washughulikiwe ili waiogope serikali and not the other way around.
 
DTO wa Sikonge anachojua ni bangi tu ukikuta ameshavuta hawezi kukupa ruhusa huyo mhuni
 
Buses Za Kwenda Kigoma, Mpanda, Kagera Hakuna Namna Lazima Mlegeze Mwili Hapo Mpaka Asubuhi Ndiyo Safari Iendelee
Ukitoka Dar Es Salaam ~Mpanda Mtalala Sikonge/Kaliua
Ukitoka Dar Es Salaam ~Kigoma Mtalala Hapo Hapo

Wasafiri Dar Es Salaam ~Kagera Nao Kahama/Ushirobo Kulala

Zamani 2007 Wanaokwenda Kigoma Walikuwa Wanapita Kahama Hapo Watu Tele Wanalala Kwenye Bus, Kubwa Zaidi Usalama Ni Mdogo Na Mapori Makubwa Sana
Ninja Akiwa Waziri Wa Mambo Ya Ndani Alisema Majambazi Yasitupangie Muda Wa Kusafiri


Watu Wasafiri Muda Wote Wanakotaka Ila Nakwambia Siyo Kagera, Kigoma, Mpanda
Mtalala Tu Njiani Mnapotoka Dar Es Salaam, Huko Noma Sana Unatembea Kilometres Tele Ni Mapori Tupu

Ukitekwa Hupati Msaada Mpaka Wachukue Vitu Vya Thamani
Serikali Vitendo Hakuna!!!
Kwa hiyo 60 yrs baada ya kujitawala bado tuendelee kuwapigia magoti hawa majangili mkuu? Kwa nini sasa serikali inatumia matrilioni ya pesa kutandaza barabara za lami kila kona ya nchi?
 
Eneo hatarishi. Wanafanya hivyo kwa usalama wako.
Mpaka baada ya miaka mingapi labda ndiyo tutaacha kuwasujudia hao majangili mkuu? Wewe unaamini nchi yetu hatuna uwezo wa kuwakabili kweli?
 
Kudhibiti haya unayolalama pande ndege , Tunaojiendea kigoma kaliua hapo ndo kituo chetu Cha kwanza kabla kuingia kigoma kesho yake sa 4 asb
 
Huo Msitu wa Kola hapo sio salama kabisa na sio.swala la.jana ama juzi

Kuna Majangili, Majambazi na kila aina ya wahalifu na ni eneo ambalo network bado ni shida kidogo

So ukisema kwamba wanakosea kutotembea usiku embu waza kuhusu familia yako halafu mkatekwe, Kumbuka Police wa escort hamtapewa kituo kizima watatoka wachache ila wale jamaa kule ndio nyumban kwao so u can imagine

Muhimu sana ni watu walale Tabora mjini, Japokuwa wenye mabus hawatak maana watachelwa kufika Mpanda.
Kwa hiyo kwa kuwa ilitokea basi iachwe tuu mpaka mwisho wa dunia? Sikonge kuna mtandao wa Simu, pale Ipole kama sikosei kuna mtandao, halkadhalika pale Inyonga kuna mtandao. Kwa hiyo sioni ugumu wowote serikali ikiamua kumalizia kuweka mtandao hapo katikati. If you don't ask you don't get it, so hatuwezi kuacha kulizungumzia jambo hili eti tuu kwa sababu huko nyuma watu walitekwa. Kumbuka serikali ni kubwa na ina priorities nyingi hivyo sisi wananchi ndiyo wenye wajibu wa kuibua hizi kero ili zifanyiwe kazi. Kwa mfano serikali inaweza kuamua kuweka kambi ndogo ya JKT au hata ya wazee wa Kazi JW hapo katikati ya hayo mapori, nothing is ever impossible mkuu hivyo tuache kutoa visingizio vya matukio ya zamani.
 
Wadau tumetoka Dar na Bus la HAPPY NATION saa 12 asubuhi na tumefika hapa Sikonge, Tabora Bus limezuiwa kuendelea na safari eti mpaka saa 12 asubuhi, eti kwa sababu njiani kuna mapori makubwa.

Kwa maoni yangu hii si sawa kabisa, yaani pamoja na jitihada kubwa za serikali kukamilisha barabara hii na sasa ni lami kutoka Dar mpaka Mpanda, bado tunawapotezea muda watanzania kukaa hapa masaa 8 kisa hatuwezi kuimarisha usalama?

Hivi tutajikwamua vipi na umasikini ikiwa tunapoteza muda kiasi hiki? Halafu sehemu yenyewe hakuna hata stend yenye facilities za kuhudumia hata abiria wa Bus mbili. Kingine cha kushangaza kwenye maamuzi yetu ni kwamba hivi unawezaje kuacha bus ilale Tabora mjini kwenye huduma nyingi halafu uje kuzuia ma Bus Sikonge?

Kwa staili hii ya kupotezeana muda kiasi hiki uchumi wa kati tutausikia tuu kwa wenzetu. Nimesikitika sana kwa kweli.
Nasikia Kuna tajiri kajenga hotel yake hapo kwa hiyo anahonga ili watu walale na kula hapo amefanya wasafiri wa mpanda ili apate wateja kwenye biashara zake.
 
Kuna kaukweli hapa maana hawa madereva wala hawajali, pia imeingia Majinja nayo imezuiwa. Swali langu ni kwa Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini hili jambo nyie hamlioni kwa jinsi abiria tunavyoteseka? Kwa nini bus zisilale Tabora mjini stend kuu ambako kuna lodges, vyakula na huduma mbalimbali badala ya kuruhusu tulale hapa Kijijini??
Hakuna hotel iliyojengwa hapo mkuu
 
Hebu tupe correlation ya Black Mamba na kuzuia mabus kusafiri usiku mkuu.
Mbona wametaja wenzangu msitu mnene,watekaji hakuna huduma za kijamii...mfano gari ikiharibika ktkt ya msitu kuna watu watashuka watataka kujisaidia kuvuta fegi...huoni ni hatari kuweza kudhuriwa na BM? na wasipate msaada, hayo machache unganisha dots zako pia..
 
Back
Top Bottom