Hivi kwanini nguvu za waganga wa kienyeji wengi wakianza ufuska/umalaya nguvu zao za tiba zinaisha?

Hivi kwanini nguvu za waganga wa kienyeji wengi wakianza ufuska/umalaya nguvu zao za tiba zinaisha?

Tiba za kienyeji ili zifanikiwe zinahusisha imani kwa kiasi kikubwa(haswa kwa anayehitaji tiba).

Sasa, kama mgonjwa anakuja na imani yake kwamba atapata tiba na atapona badala yake mganga anamtaka kingono(hata kama ataihusisha na matibabu yenyewe), imani ya mgonjwa kupona inapungua hivyo kuharibu uponyaji.
Sifa ya mganga inaanza kuharibikia hapo.
 
Uhalisia waganga hawanaga nguvu zozote .. ni janja janja za kisaikolojia na viini macho tu.

Kama unabisha weka password kwenye simu yako. Hakikisha unaijua peke yako hata mkeo wala mama yako haijui..

Kisha nenda kwa mganga.. mwambie apige ramli zake na dawa zake kisha aitoe password simu yako uone kama ataweza

Ndege ya malaysia airline mh 370 ilivyopotea lilitangazwa dau kwa waganga dunia nzima waseme iko wapi.. waganga kimyaaaa kama hawajaona tangazo vile

Hiv ile ndege ilirudi?

Halafu nakumbuka miaka ya 2006 hivi kuna mtoto alitangazwa kupotea huko ulaya alikua anatangazwa sana na cnn mpaka shehe yahya akaingilia kati naye sijui alipatikana?
 
Wasalaam nyote,

Tukubbali tukatae Rais Hassan. Anaupiga mwingi, 🙏🙏🙏🙏🙏

Niende kwenye mada moja kwa zote, katika harakati zangu za kuchangamana na watu mbalimbali sehemu nyingi katika mizunguko ya kikazi hasa ndani ya nchi si mara moja nimewasikia wakulungwa wakisema.

Mganga wa kienyeji awaye yeyote awe wa kitabu, tunguli, awe wa kurithi mizimu, akianza ufuska ama umalaya tu nguvu za tiba na ubora wake vinapotea, kupungua au kuexpire kabisa. Je umalaya unasumu gani kwenye tiba za uganga ?

Je kuna uhusiano gani kati ya hivi vitu nguvu za uganga na umalaya?

Wenye uzoefu au idea elimu asili na elimu tiba asili karibu kwa majibu tafadhari,

Wadiz

ccc. UMUGHAKA
ccc. Mshana Jnr
ccc. etc
Kuna watu mapenzi yanawaongezea nguvu.
Kuna wengine yanawapunguza nguvu.
 
Kuna dogo huku kwetu alikuwa msanii na kaweka rasta,sasa mizimu yake ikataka awe mganga,kishingo upande akakubali baada ya hyo mizimu kumsumbua akaanza kutoa huduma

mWanzo akawa na wateja wengi tu,alikuwa ametafuta mbugani huko kaweka vijumba vyake,baadae akaanza umalaya na kucheza kamali,wateja wakaanza kupungua akaanza hadi kuuza baadhi ya mali zake ikiwemo hadi pikpik moja matata sana na alikuwa anaipenda sana

Baadae alihama
 
Wasalaam nyote,

Tukubbali tukatae Rais Hassan. Anaupiga mwingi, [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Niende kwenye mada moja kwa zote, katika harakati zangu za kuchangamana na watu mbalimbali sehemu nyingi katika mizunguko ya kikazi hasa ndani ya nchi si mara moja nimewasikia wakulungwa wakisema.

Mganga wa kienyeji awaye yeyote awe wa kitabu, tunguli, awe wa kurithi mizimu, akianza ufuska ama umalaya tu nguvu za tiba na ubora wake vinapotea, kupungua au kuexpire kabisa. Je umalaya unasumu gani kwenye tiba za uganga ?

Je kuna uhusiano gani kati ya hivi vitu nguvu za uganga na umalaya?

Wenye uzoefu au idea elimu asili na elimu tiba asili karibu kwa majibu tafadhari,

Wadiz

ccc. UMUGHAKA
ccc. Mshana Jnr
ccc. etc
Kuna stori nlisoma humu nadhani aliiandika mkongwe JBourne59 JBourne59 kama ukifanikiwa kuisoma itakufunua kidogo
 
Mganga hatakiwi kulala na mtu aliyemfanyiq kazi akifanya hivyo nguvu zake hupungua. Hii ni miiko ya uganga hairuhusiwi. .

Ila mganga akilala na mtu baki nadhani haina shida.
 
Back
Top Bottom