Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

kama ilivyo Monaco kwa ufaransa..Vaticani kwa italy ...na Zanzibar watoe idadi yao nasi tutoe idadi yetu kama Tanzania maana naona Zanzibar wanazua taharuki..kila MTU atoe na kurekodi takwimu zake na zikipelekwa John khoping university kila mamlaka icompile data zake.
 
Muungano wetu ni wa serikali mbili...wizara ya afya siyo ya Muungano.Tanzania yaani ukijumuisha na zanzibar ndiyo inatambulika na WHO......Ndiyo maana katka taarifa ya kidunia Zanzibar huwezi kuiona kwenye taarifa za WHO
 
Watanzania na dunia tumekuwa tukipewa taarifa mbili tofauti za visa vya Corona kutoka katika taifa la Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huku wakati mwingine kukiwa na mchanganyo wenye kutupa wasiwasi au marudio ya taarifa zile zile pasipo sababu ya msingi.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amekuwa akitoa taarifa za Corona kwa Tanzania nzima (ikiwemo Zanzibar) na wakati huo huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa taarifa za Corona kwa Zanzibar.

Ni kweli tunajua suala la Afya sio suala la muungano, hivyo Zanzibar wako sahihi na wanayo haki ya wao kulisemia bila mamlaka za serikali ya muungano kuwaingilia, lakini busara ingeweza kutumika kwa suala hili kubakia kusemewa na waziri wa Tanzania tu ili kuepusha mchanganyo wa kitaarifa kwa dunia inayofuatilia suala hili kwa karibu mnoo.

Upande wa pili ni kuwa, kwa kuwa la suala la Afya sio la muungano, ingekuwa ni busara kwa waziri wa muungano wa Tanzania kuwasemea watanzania bara tu na kuwaacha wazanzibar wao wenyewe kulisemea maana halimhusu.

Busara ianze kutumika sasa, huko tunakoelekea ipo hatari ya mmoja kumharibia mwingine taarifa zake pasipo kukusudia.
Huo ugumu unaletwa na mfumo wa muungano uliopo wa serikali mbili...tungelikuwa na serikali moja tabu hio isingekuwepo
 
Hizi ni nchi mbili tofauti, kila moja ikiwa na wizara yake ya afya, Tanganyika waziri ni Ummy Mwalim na Zanzibar waziri ni Hamad Rashid.

Wanaosema Zanzibar sio nchi wasubiri Kagera nayo ianze kutoa taarifa zake za Corona.
Nchi ni moja ila serikali ni mbili...Ummy Mwalimu ni waziri wa nchi nzima (zanzibar inclunsive), ndiye anayetambulika na WHO, na ndiye anayetakiwa kutoa takwimu za nchi kwa WHO na Other international bodies
 
Sasa inakuwaje waziri wa Afya wa Tanzania (Ummy Mwalimu) anatoa tena taarifa za Corona za Zanzibar?
Katumwa na nani?
Amepata wapi hayo mamlaka?

Moja: Yeye anatoa takwimu za nchi (zanzibar inclusive)....Hamad Rashid ni kama anatoa takwimu za mkoa

Mbili: WHO na taasisi nyingine za UN zinataka takwimu kutoka kwake (wanamtambua Ummy Mwalimu tuu)
 
Mleta maada, ni jumuiaya ipi ya kimataifa iliyopata mkanganyiko? Maana mimi hufuatilia live updates kwenye international sites kama worldometer na hakuna siku wamekanganyika.

Mihemuko yenu isiwatie upofu hata kwenye masuala kama haya ambayo hayahitaji ujuaji. Ikiwa mnashangaa waziri Ummy kuisemea mpaka Zanzibar ilhali yenyewe inaye Hamad Rashid anayeisemea tayari, basi yawapasa kuwatafuta walimu wenu wa uraia mrudishiwe ada mlizolipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kupotosha umma kisa eti una Id fake na chuki za kisiasa. Soma ibara ya 1 ya katiba ya Zanzibar na ibara ya 2(1) ya katiba ya JMT. Wala hamna mkanganyiko wowote ila unataka kuleta siasa za chuki kwa jambo halina hata dosari.
Reference halali ni katiba ya Jamuhuri ya Muungano tuu
 
  • hamad anawakilisha zanzibar,
  • ummy mwalimu anawakilisha Tanzania (muunganiko wa Tanganyika na zanzibar)
sijaliona kosa la Ummy mwalimu mpaka muda huu

Tanganyika haina utofauti na shetani wa ruhani, hajitokezi mpaka asomewe kisomo maalum
" AG othman massoud"
 
Hata mimi huwa najiuliza kwanini tusiwe na serikali moja tu, kuliko namna ilivyo sasa?? Naamini ipo siku tutafikia hapo.
Serikali ya Muungano, Bunge la Muungano, na CCM wakinuia jambo hili linawezekana hata kesho.....Awamu ya tano walitazame hili
 
Hata kama wakitaka kuendelea kutoa kila mmoja lwake, basi kuwepo coordination. Haya mambo ya kusubiliana yanatia shaka. Afterall vipimo vyote vinatokea Dar. Kwa nini wasitoe taatifa wakati mmoja? Inaonekana wa bara anadubiri wa unguja aseme kwanza!
 
Nchi ni moja ila serikali ni mbili...Ummy Mwalimu ni waziri wa nchi nzima (zanzibar inclunsive), ndiye anayetambulika na WHO, na ndiye anayetakiwa kutoa takwimu za nchi kwa WHO na Other international bodies
Thubutu yake! Jidanganye tu...

Umewahi kumuona Ummy mwalim akienda kule chake chake ziara ya kikazi au kushughulikia masuala ya afya???
 
Mleta maada, ni jumuiaya ipi ya kimataifa iliyopata mkanganyiko? Maana mimi hufuatilia live updates kwenye international sites kama worldometer na hakuna siku wamekanganyika.

Mihemuko yenu isiwatie upofu hata kwenye masuala kama haya ambayo hayahitaji ujuaji. Ikiwa mnashangaa waziri Ummy kuisemea mpaka Zanzibar ilhali yenyewe inaye Hamad Rashid anayeisemea tayari, basi yawapasa kuwatafuta walimu wenu wa uraia mrudishiwe ada mlizolipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiwe mbishi sana.
Mashirika mengi ya kimataifa yanakusanya taarifa zao kutoka taarifa za rasmi za nchi husika na WHO na kuna wakati huchelewa kuupdate taarifa zao ikiwa chanzo chao kikuu cha taarifa kikichelewa kutoa taarifa.

Ngoja nikumpe mfano rahisi sana.
Mpaka sasa Tanzania tuna wagonjwa 32 wa COVID. Sasa kwa mfano kesho Zanzibar ikatoa taarifa kuwa kuna wagonjwa wapya 3 wa Corona kwa Zanzibar, pasipo waziri wa Muungano kutoa taarifa mpya ya wagonjwa wa Corona hapa Tz kwa kesho. Hapo worldometer itasema Tanzania tuna wagonjwa wangapi?

Wasiwasi wangu ni kuwa unapokuwa na mamlaka mbili tofauti zenye jukumu la kutoa taarifa zake rasmi mpya huku zikitakiwa kufanana, upo uwezekano mkubwa sana wa kuja na taarifa mikanganyiko.
 
Thubutu yake! Jidanganye tu...

Umewahi kumuona Ummy mwalim akienda kule chake chake ziara ya kikazi au kushughulikia masuala ya afya???
Majukumu yake yamekasimishwa kwa anayeitwa waziri wa afya wa zanzibar

Hata bara haendi kote, na kule asikoenda subordanets humsaidia...upo!
 
Back
Top Bottom