Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

Watanzania na dunia tumekuwa tukipewa taarifa mbili tofauti za visa vya Corona kutoka katika taifa la Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huku wakati mwingine kukiwa na mchanganyo wenye kutupa wasiwasi au marudio ya taarifa zile zile pasipo sababu ya msingi.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amekuwa akitoa taarifa za Corona kwa Tanzania nzima (ikiwemo Zanzibar) na wakati huo huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa taarifa za Corona kwa Zanzibar.

Ni kweli tunajua suala la Afya sio suala la muungano, hivyo Zanzibar wako sahihi na wanayo haki ya wao kulisemia bila mamlaka za serikali ya muungano kuwaingilia, lakini busara ingeweza kutumika kwa suala hili kubakia kusemewa na waziri wa Tanzania tu ili kuepusha mchanganyo wa kitaarifa kwa dunia inayofuatilia suala hili kwa karibu mnoo.

Upande wa pili ni kuwa, kwa kuwa la suala la Afya sio la muungano, ingekuwa ni busara kwa waziri wa muungano wa Tanzania kuwasemea watanzania bara tu na kuwaacha wazanzibar wao wenyewe kulisemea maana halimhusu.

Busara ianze kutumika sasa, huko tunakoelekea ipo hatari ya mmoja kumharibia mwingine taarifa zake pasipo kukusudia.
Mbona ushajijibu tyr swali lako,!
 
Huu ni Muungano ni wa Nchi mbili Tanganyika na ZANZIBAR ndani ya Tanzania kuna serikali ya Tanganyika ambayo inasimamiwa na Wazir Mkuu kama Makamo wa pili anavyosimamia mambo ya ZANZIBAR
Sisi hatujaungana kila kitu ndio maana ZANZIBAR ina Mawazir wake ktk mambo yasiyo ya Muungano
Mfano mzur ni WIZARA YA AFYA
Nyinyi mnawazir wenu na sisi una waziri wetu

Kama mnataka taarifa za CORONA ziwe ni moja basi ziratibiwe na WIZARA YA AFYA YA SMZ na Waziri Hamad Rasshid awe ndio msemaji Mkuu

Hivyo mkigundua mgonjwa huko TANDAHMBA nimerufuku kutangaza mpaka taarifa muilete ZANZIBAR wizara yaw Afya ithibitishe kisha wazir wa Afya wa ZANZIBAR atangaze hizo kesi

#STAY at HOME
# OSHA MIKONO
#Tumechoka tamaa zenu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simple! Afya sio Union Matter. Ni kutokana na kuwa territory moja ndio maana tunapeana taarifa kwa pamoja na kuzijumlisha. Eleweni maana ya territory kwa wale wabishi. Lakini pia hakuna nchi inaitwa Zanzibar huko nje. Hii ni baada ya makubaliano ya Muungano. UN wanatambua nchi moja tu inayoitwa Tanzania. Hata mashirika na nchi zingine zinaitambua nchi moja ya Tanzania. Kwa hiyo ni lazima tujumlishe ili tusiwachanganue duniani kwa mambo yetu tunayoelewana wenyewe.
 
kama ilivyo Monaco kwa ufaransa..Vaticani kwa italy ...na Zanzibar watoe idadi yao nasi tutoe idadi yetu kama Tanzania maana naona Zanzibar wanazua taharuki..kila MTU atoe na kurekodi takwimu zake na zikipelekwa John khoping university kila mamlaka icompile data zake.
Kama ni hivyo nyinyi hamuezi kutoa kama Tz inabidi mutoe zenu za Tanganyika tu. Kiufupi suluhisho ya yote haya ni kuvunja muungano.
 
Simple! Afya sio Union Matter. Ni kutokana na kuwa territory moja ndio maana tunapeana taarifa kwa pamoja na kuzijumlisha. Eleweni maana ya territory kwa wale wabishi. Lakini pia hakuna nchi inaitwa Zanzibar huko nje. Hii ni baada ya makubaliano ya Muungano. UN wanatambua nchi moja tu inayoitwa Tanzania. Hata mashirika na nchi zingine zinaitambua nchi moja ya Tanzania. Kwa hiyo ni lazima tujumlishe ili tusiwachanganue duniani kwa mambo yetu tunayoelewana wenyewe.
Mkuu kupeana taarifa ndani kwa ndani kiserikali na kutoa taarifa mbili tofauti kwa umma ni mambo mawili tofauti.

Sina tatizo kwa SMZ na JMT kupeana taarifa 'internally' lakini ninaona tatizo kubwa ikiwa kila serikali kwa nyakati tofauti inatoa taarifa zake kwa umma (Public notice) kwa jambo lile lile.

Hivi nani anapaswa kutangulia (source) kutoa taarifa na yupi afuate nyuma (Copy)?
Vipi ukitokea mmoja akachelewa taarifa zake?
Vipi ikitokea taarifa zikawa na utofauti (Discrepancy)?
 
Mi naona labda ni hii corona inawachanganya, Ummy anatoa taarifa za jamuhuri ya muungano wa Tanzania na anajitahidi kila siku kufafanua wagonjwa wa zanzibar ni wangapi na bara ni wangapi , na huyo wa zanzibar anatoa taarifa za zanzibar peke yake kwa watu wa huko visiwani. Sasa msichoelewa hapo ni nini?
 
Mkuu kupeana taarifa ndani kwa ndani kiserikali na kutoa taarifa mbili tofauti kwa umma ni mambo mawili tofauti.

Sina tatizo kwa SMZ na JMT kupeana taarifa 'internally' lakini ninaona tatizo kubwa ikiwa kila serikali kwa nyakati tofauti inatoa taarifa zake kwa umma (Public notice) kwa jambo lile lile.

Hivi nani anapaswa kutangulia (source) kutoa taarifa na yupi afuate nyuma (Copy)?
Vipi ukitokea mmoja akachelewa taarifa zake?
Vipi ikitokea taarifa zikawa na utofauti (Discrepancy)?
Swali lako sio la kisera, sio la kumuundo, sio la kisheria, sio la kikanuni na sio la kikatiba.
Wewe una shida na mode of delivery. Hapo sasa ni wao. Wa bara anaweza akanakili taarifa iliyokwishatolewa Zanzibar. Sababu ya kushawishi hapa ni kwa sababu macho ya dunia sana sana huelekezwa bara kutokana na mazoea na umaarufu wa jina, si tuliacha Tanganyika, wao wakendeleza Zanzibar. Taarifa zinazochukuliwa Kimataifa sana ni zile zitolewazo huku bara.
 
Mimi nashangaa sana .Nimekosa cha kuandika maana walisema Muungano huruhusiwi kuhoji
 
Muungano umekaa kitapelitapeli tu, Kuna mambo hayapo sawa kwenye huu muungano. Natamani Ummy atambulishwe kama waziri wa afya wa tanganyika and not Tanzania
Fahamu hili, Serikali ya muungano ipo kwa ajili ya mambo ya muungano na mambo yanayohusu Tanganyika ambayo hayapo kwenye muungano. Mfano Afya, Elimu, Utalii, Nishati, Maji, Ajira nk.

Kwa kuwa afya sio suala la muungano, hivyo waziri wa Afya wa Tanzania anawajibika na mambo ya afya ya Tanganyika tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnajibagua wenyewe kwa wenyewe lakini Wachina wakiwabagua mnaanza kulia lia kua mnaonewa,

Pathetic.

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Back
Top Bottom