Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

Hivi kwanini taarifa ya Corona kwa Tanzania bara na Zanzibar isiwe moja tu?

Majukumu yake yamekasimishwa kwa anayeitwa waziri wa afya wa zanzibar

Hata bara haendi kote, na kule asikoenda subordanets humsaidia...upo!
Acha kuongea uongo. Bara anakwenda kote, Zanzibar hawezi kufika kikazi kwa sababu mwisho wake chumbe
 
  • hamad anawakilisha zanzibar,
  • ummy mwalimu anawakilisha Tanzania (muunganiko wa Tanganyika na zanzibar)
sijaliona kosa la Ummy mwalimu mpaka muda huu

Tanganyika haina utofauti na shetani wa ruhani, hajitokezi mpaka asomewe kisomo maalum
" AG othman massoud"
Hivi unajua maana ya "mambo yasiyo ya muungano"?

Afya sio suala la muungano, hivyo waziri Ummy Mwalimu hapaswi kikatiba kuwasemea wazanzibar afya zao. Afya za wazanzibar hazihusiani na serikali ya muungano.
 
Watanzania na dunia tumekuwa tukipewa taarifa mbili tofauti za visa vya Corona kutoka katika taifa la Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huku wakati mwingine kukiwa na mchanganyo wenye kutupa wasiwasi au marudio ya taarifa zile zile pasipo sababu ya msingi.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amekuwa akitoa taarifa za Corona kwa Tanzania nzima (ikiwemo Zanzibar) na wakati huo huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa taarifa za Corona kwa Zanzibar.

Ni kweli tunajua suala la Afya sio suala la muungano, hivyo Zanzibar wako sahihi na wanayo haki ya wao kulisemia bila mamlaka za serikali ya muungano kuwaingilia, lakini busara ingeweza kutumika kwa suala hili kubakia kusemewa na waziri wa Tanzania tu ili kuepusha mchanganyo wa kitaarifa kwa dunia inayofuatilia suala hili kwa karibu mnoo.

Upande wa pili ni kuwa, kwa kuwa la suala la Afya sio la muungano, ingekuwa ni busara kwa waziri wa muungano wa Tanzania kuwasemea watanzania bara tu na kuwaacha wazanzibar wao wenyewe kulisemea maana halimhusu.

Busara ianze kutumika sasa, huko tunakoelekea ipo hatari ya mmoja kumharibia mwingine taarifa zake pasipo kukusudia.
Zanzibar ni nchi. Ina Rais na mipaka yake.
 
Acha kuongea uongo. Bara anakwenda kote, Zanzibar hawezi kufika kikazi kwa sababu mwisho wake chumbe
SMZ imekasimishwa majukumu na SMT...hii ndio maana ya muungano wa serikali mbili...pole lakini kwa kutofahamu kwa undani codes za muundo wa serikali mbili

Viongozi wote wa SMZ wanahudumu on behalf ya serikali ya muungano (hii ndio serikali kuu)
 
Hivi unajua maana ya "mambo yasiyo ya muungano"?

Afya sio suala la muungano, hivyo waziri Ummy Mwalimu hapaswi kikatiba kuwasemea wazanzibar afya zao. Afya za wazanzibar hazihusiani na serikali ya muungano.
mkuu hayo mambo ya muungano baki nayo nafsini mwako..
Ummy anawakilisha Tanzania (ndivyo ninavyofahamu mimi) na anapowasilisha taarifa kuhusiana na corona anapaswa kuunganisha takwimu za pande zote mbili.

Unashangaa ya Ummy haliyakuwa muungano wetu umempa heshima ya mjumbe wa baraza la mawaziri (Raisi wa zanzibar),
mamlaka ya Hamad yanaishia kisiwa cha Chumbe kwa sababu hakuna nchi inayoitwa Zanzibar kwenye medani za kimataifa.
 
Afya si swala la muungano lakini hapo hapo mambo ya nchi za nje ni swala la muungano (serikali mwanachama wa wa WHO ni serikali ya muungano) so mwanamke wa kitanga Ummy Mwalimu hakwepeki...nawe upo!
 
Sasa waziri wa afya wa JMT amewekwa wa nini wakati suala sio la muungano?

Sent using Jamii Forums mobile app
Fahamu hili, Serikali ya muungano ipo kwa ajili ya mambo ya muungano na mambo yanayohusu Tanganyika ambayo hayapo kwenye muungano. Mfano Afya, Elimu, Utalii, Nishati, Maji, Ajira nk.

Kwa kuwa afya sio suala la muungano, hivyo waziri wa Afya wa Tanzania anawajibika na mambo ya afya ya Tanganyika tu.
 
mkuu hayo mambo ya muungano baki nayo nafsini mwako..
Ummy anawakilisha Tanzania (ndivyo ninavyofahamu mimi) na anapowasilisha taarifa kuhusiana na corona anapaswa kuunganisha takwimu za pande zote mbili.

Unashangaa ya Ummy haliyakuwa muungano wetu umempa heshima ya mjumbe wa baraza la mawaziri (Raisi wa zanzibar),
mamlaka ya Hamad yanaishia kisiwa cha Chumbe kwa sababu hakuna nchi inayoitwa Zanzibar kwenye medani za kimataifa.
Bora nikuache na ubishi wako.
Unajaribu kubishana na mimi badala ya kubishana na katiba ya Tanzania.
 
Bora nikuache na ubishi wako.
Unajaribu kubishana na mimi badala ya kubishana na katiba ya Tanzania.
hakuna sehemu niliyoonyesha ubishi, hii ishu haihitaji kuwa guru wa katiba na sheria bali ni uelewa tu wa kawaida ndio unaohitajika
  1. Hamad anatangaza kwanza taarifa za zanzibar
  2. ummy anatangaza taarifa za Tanganyika pamoja na Zanzibar (lakini baada ya Hamad kutoa taarifa), ndivyo utaratibu ulivyo bila ya shaka unafahamu.
  3. Ummy hawezi kutoa taarifa za Tanzania bara pekee kwa sababu hakuna nchi inayoitwa Tanganyika....hizi Takwimu haziishii ndani ya nchi tu, Ummy anawakilisha serikali ya Muungano na si chama cha wanasheria wa Tanganyika
nimeshakwambia Tanganyika ni shetani wa ruhani, hawezi kujitokeza mpaka kwa kisomo maalumu.
 
Afya si swala la muungano lakini hapo hapo mambo ya nchi za nje ni swala la muungano (serikali mwanachama wa wa WHO ni serikali ya muungano) so mwanamke wa kitanga Ummy Mwalimu hakwepeki...nawe upo!
Naona unaunganisha unganisha mambo ili kutengeneza sababu, lakini unakwepa ukweli halisi.

Kukusaidia tu, ni kuwa Ummy Mwalimu ni waziri wa Afya wa Tanzania, hawajibiki popote kikatiba moja kwa moja kuwasemea watanzania katika diplomasia ya kimataifa. Anawajibika kuwasemea watanganyika katika mambo ya Afya.

WHO ni shirika la Afya duniani, linaweza kushirikiana na mamlaka za nchi yoyote kuhakikisha suala la afya kwa watu duniani linaboreshwa. Huhitaji kuwa na chochote ili WHO ishirikiane na wewe. WHO sio taasisi ya kisiasa, uwe muasi, gaidi au muhuni bado WHO inaweza kushirikiana na wewe.
 
hakuna sehemu niliyoonyesha ubishi, hii ishu haihitaji kuwa guru wa katiba na sheria bali ni uelewa tu wa kawaida ndio unaohitajika
  1. Hamad anatangaza kwanza taarifa za zanzibar
  2. ummy anatangaza taarifa za Tanganyika pamoja na Zanzibar (lakini baada ya Hamad kutoa taarifa), ndivyo utaratibu ulivyo bila ya shaka unafahamu.
  3. Ummy hawezi kutoa taarifa za Tanzania bara pekee kwa sababu hakuna nchi inayoitwa Tanganyika....hizi Takwimu haziishii ndani ya nchi tu
nimeshakwambia Tanganyika ni shetani wa ruhani, hawezi kujitokeza mpaka kwa kisomo maalumu.
Soma mada yangu ndio utanielewa vizuri.

Sina tatizo na nani katika nchi atawasemea watanzania kitaifa au kimataifa, kama tukienda kikatiba haswaa, basi Hamad Rashid yuko sahihi kwa 100% kuwasemea wazanzibar kuhusu Afya zao (pasipo hata kuwasiliana na mamlaka za serikali ya muungano) na tukija kwa Ummy Mwalimu kikatiba HAYUKO SAHIHI kwa 100% kutoa taarifa za afya za wazanzibar pasipo idhini ya serikali ya Zanzibar kwanza. Nasema hivi kwa sababu mara kadhaa Ummy Mwalimu ametoa taarifa za COVID kabla ya Serikali ya Zanzibar kuitoa kwanza!

Yote hayo sio issue, issue yangu ni kuona mamlaka mbili za serikali mbili tofauti kukazana kutoa taarifa mbili nyeti kwa nyakati mbili tofauti, taarifa ambazo zinapaswa kuwa zinashahabiana kwa 100%. Tunatafuta nini?
Nini kitatokea ikiwa taarifa zitatofautiana?
 
Kuongezwe taarifa za waganga wakuu wa mikoa ikionesha idadi ya waliopimwa na ikiwezekana idadi ya washukiwa ielezwe.
Japo kwa kila wiki.

Msisitizo uongezwe watu wazingatie lishe bora,usafi na ushauri wa selikari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom