TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,593
Mbona ushajijibu tyr swali lako,!Watanzania na dunia tumekuwa tukipewa taarifa mbili tofauti za visa vya Corona kutoka katika taifa la Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huku wakati mwingine kukiwa na mchanganyo wenye kutupa wasiwasi au marudio ya taarifa zile zile pasipo sababu ya msingi.
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amekuwa akitoa taarifa za Corona kwa Tanzania nzima (ikiwemo Zanzibar) na wakati huo huo Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa taarifa za Corona kwa Zanzibar.
Ni kweli tunajua suala la Afya sio suala la muungano, hivyo Zanzibar wako sahihi na wanayo haki ya wao kulisemia bila mamlaka za serikali ya muungano kuwaingilia, lakini busara ingeweza kutumika kwa suala hili kubakia kusemewa na waziri wa Tanzania tu ili kuepusha mchanganyo wa kitaarifa kwa dunia inayofuatilia suala hili kwa karibu mnoo.
Upande wa pili ni kuwa, kwa kuwa la suala la Afya sio la muungano, ingekuwa ni busara kwa waziri wa muungano wa Tanzania kuwasemea watanzania bara tu na kuwaacha wazanzibar wao wenyewe kulisemea maana halimhusu.
Busara ianze kutumika sasa, huko tunakoelekea ipo hatari ya mmoja kumharibia mwingine taarifa zake pasipo kukusudia.
Kama ni hivyo nyinyi hamuezi kutoa kama Tz inabidi mutoe zenu za Tanganyika tu. Kiufupi suluhisho ya yote haya ni kuvunja muungano.kama ilivyo Monaco kwa ufaransa..Vaticani kwa italy ...na Zanzibar watoe idadi yao nasi tutoe idadi yetu kama Tanzania maana naona Zanzibar wanazua taharuki..kila MTU atoe na kurekodi takwimu zake na zikipelekwa John khoping university kila mamlaka icompile data zake.
Mkuu kupeana taarifa ndani kwa ndani kiserikali na kutoa taarifa mbili tofauti kwa umma ni mambo mawili tofauti.Simple! Afya sio Union Matter. Ni kutokana na kuwa territory moja ndio maana tunapeana taarifa kwa pamoja na kuzijumlisha. Eleweni maana ya territory kwa wale wabishi. Lakini pia hakuna nchi inaitwa Zanzibar huko nje. Hii ni baada ya makubaliano ya Muungano. UN wanatambua nchi moja tu inayoitwa Tanzania. Hata mashirika na nchi zingine zinaitambua nchi moja ya Tanzania. Kwa hiyo ni lazima tujumlishe ili tusiwachanganue duniani kwa mambo yetu tunayoelewana wenyewe.
Swali lako sio la kisera, sio la kumuundo, sio la kisheria, sio la kikanuni na sio la kikatiba.Mkuu kupeana taarifa ndani kwa ndani kiserikali na kutoa taarifa mbili tofauti kwa umma ni mambo mawili tofauti.
Sina tatizo kwa SMZ na JMT kupeana taarifa 'internally' lakini ninaona tatizo kubwa ikiwa kila serikali kwa nyakati tofauti inatoa taarifa zake kwa umma (Public notice) kwa jambo lile lile.
Hivi nani anapaswa kutangulia (source) kutoa taarifa na yupi afuate nyuma (Copy)?
Vipi ukitokea mmoja akachelewa taarifa zake?
Vipi ikitokea taarifa zikawa na utofauti (Discrepancy)?
Fahamu hili, Serikali ya muungano ipo kwa ajili ya mambo ya muungano na mambo yanayohusu Tanganyika ambayo hayapo kwenye muungano. Mfano Afya, Elimu, Utalii, Nishati, Maji, Ajira nk.
Kwa kuwa afya sio suala la muungano, hivyo waziri wa Afya wa Tanzania anawajibika na mambo ya afya ya Tanganyika tu.
Huyo waziri wa afya wa JMT ni nani?
Kama akili yako imewekewa kufuri sasa unategemea nini?Ummy, na wakati wizara siyo ya muungano [emoji56][emoji56][emoji56][emoji56]
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama akili yako imewekewa kufuri sasa unategemea nini?
Kwa kweli sifahamu.Ummy huwa anatangaza vifo na idadi ya waloathirika na Corona kote bara na visiwani yeye kama nan? Tafadhari naomba ujibu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli sifahamu.
Baada ya mbili kinachofuata tatu sio moja tayari moja imeshapitwa maisha yanasonga mbele sio kurudi nyumaHata mimi huwa najiuliza kwanini tusiwe na serikali moja tu, kuliko namna ilivyo sasa?? Naamini ipo siku tutafikia hapo.