Hivi kwanini watu wapole wako hivi?

Ni kawaida kwa JF ... Members wa platform hii kila member ana gari .. Kila member hatumii tecno ..kila member ni muhitimu wa chuo kikuu and the likes
mzee usiwe mtu wa ku generalize mambo, JF ina members zaid ya laki tano, hapa kuna comments za members kama mia hamsin kasoro hv. afu ww unakuja kusema member wote wa Jf.......hawa memba wote wa JF hua mnawapata wapi?

Sku zote "Maudhui ya uzi ndo huamua aina ya wachangiaji". Mfano ukianzishwa uzi wa introvert utakuta introverts wanajisema humo. na sio members WOTE.
 
Mimi ni mpole na mkimya kwa pamoja

Ila nikigusa gambe nawaka kama moto naongea sana.
 
Mara nyingi huwa hatupendi usumbufu.
Hili ndio jibu sahihi,hata mimi ni mpole huwa sipendi kabisa usumbufu au purukushani za aina zozote zile na wala sipendi kupoteza muda kwa namna yoyote ile.
Kwa hiyo nikiingia kwenye mahusiano huwa natumia akili nyingi sana kumsoma huyo mwenza kimyakimya bila yeye mwenyewe kujua kuwa namsoma/namchunguza.
Nikishaona ana mawenge au ujuaji mwingi uliopitiliza au makelele mengi najiandaa kumpiga chini fasta.
 
Wengi mnaowaita wapole siyo wapole bali ni wa kimya tu!

Kuna tofauti kati ya upole na ukimya!

Upole ni mojawapo ya tunda la Roho Mtakatifu.

Ni mwenye Roho Mtakatifu tu anaweza kuwa mpole ijapokuwa inategemea.

Ukimya ni tabia kubwa ya majambazi!
Fafanua huo upole wa Roho mtakatifu
 
Wengi mnaowaita wapole siyo wapole bali ni wa kimya tu!

Kuna tofauti kati ya upole na ukimya!

Upole ni mojawapo ya tunda la Roho Mtakatifu.

Ni mwenye Roho Mtakatifu tu anaweza kuwa mpole ijapokuwa inategemea.

Ukimya ni tabia kubwa ya majambazi!
Tutake radhi , unawezaje kutufananisha sisi na Majambazi.

Mbona maccm sio mapole lakini yana yanajambaza pesa za watz
 
Dah mkuu wewe utakuwa umesomea saikolojia.
Yaani tabia zote ulizotaja ndio niko nazo mimi,huwa sipendi kumpa mtu promise kwa maneno mengi bali mtu akiniomba kitu nitaitikia tu kwa kichwa bila kuongea,lakini lazima nitimize kwa vitendo sasa mtu asiyejua anakasirika akihisi labda umedharau ombi lake.
Mke wangu pia unishangaa muda mwingi vitu vyangu huwa navimaliza kichwani kwangu bila kuongea,lakini mwisho wa siku naibuka na utekelezaji.
 
Pamoja sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…