Wapole au wakimya, maana kuna watu ambao ni waongeaji lakini ni wapole.
Ngoja nikusaidie tu , watu wengi hasa wanawake wanachanganya kati ya watu wakimya na wapole.
Upole ni tabia ya ndani, ambayo inatafsiwa Kwa MTU kuwa na huruma, caring na upendo. Na kinyume cha upole ni ukatili.
Na kuna ukimya maana sio muongeaji. Kinyume cha mkimya ni muongeaji.
Kuna watu wakimya halafu wapole pia. Lakini kuna watu wakimya halafu ni makatili. Hawana huruma, upendo na sio caring.
Pia kuna watu waongeaji lakini wapole pia.
Watu wengi wanaingia chaka Kwa kushindwa kujua jambo hili wanapochagua wenza wao, Mara nyingine unaingia Kwa MTU mkimya lakini sio mpole unaishia kuchezea kichapo. Unakuta MTU huyo anakuwa mafia, mwenye tabia mbaya, asiyejali kabisa ila ndio hivyo sio muongeaji.