Kuna Movie Moja hivi niliangalia mwaka jana, (2019) inaitwa "Plus One". Ni love story flani hivi imechangamka. Anyway ngoja niende kwenye point..
Kuna Jamaa huko anaitwa Ben, kaigiza kama introvert flani hivi (aina ya watu unaowasemea hapo juu, wapole). Kuna mahali aliulizwa swali na bestie yake, Alice kuwa kwanini anashindwa ku date muda mrefu (or kudumu kwenye mahusiano)?
Nafikiri jibu alilotoa linaweza ku fit kwenye huu uzi..
Alisema "Watu wa aina yake (wapole) huwa sio rahisi sana kuwa kwenye mahusiano kwa sababu ni ngumu sana kuwazoea (especially wanaume), kwaiyo hii inawafanya wawe Single kwa muda mrefu sana. Sasa kuwa Single kunawafanya wajijue zaidi, kunawafanya wajue ni vitu gani hasa wanahitaji kwenye mahusiano. Kwaiyo hii inawapelekea kujua kwa haraka zaidi kuwa mtu wanayekutana nae hafai au hataendana naye kwenye mahusiano, na hapotezi muda akishagundua hilo, anaamua kuachana naye tu."
Nadhani hiyo point ina ukweli ndani yake kulingana na uzi wako!