Imagine this;upo na character hiyo toka mdogo,hujichanganyi sana na watu,si mwongeaji sana,unaishi sana katika fikra na mawazo yako,mengi yanaamuliwa katika kichwa chako bila kuhusisha sana ushawishi wa mazingira ya nje.
Baada ya miaka kadhaa unakuwa master ya hiyo kitu.Unaona dalili ya mengi mabaya,unajua dalili hii inamaanisha hivi na italeta mambo fulani.
Na sio katika kuacha tu,pia unaweza angalia tu kwa namna mtu alivyo,anavyoongea,tembea,vaa n.k ukajua hapa sio.
Na shida sio tu kwamba tunawavutia extroverts,na labda tunapenda waongeaji...bali pia tunaofanana nao ni wachache sana,hivyo hisia huzidi akili mara kadhaa na kusema ngoja nijaribu hapa,akili inaporudi unaona hapa sio,unaacha.