Hivi kwanini Yesu hakuoa wala kuwa na mchumba miaka yote hiyo?

Hivi kwanini Yesu hakuoa wala kuwa na mchumba miaka yote hiyo?

Yeye ni mungu alikuja kuifanya kazi ya mungu🤔🤔🤔 huyo mungu mwengine ni yupi sasa?

Yohana 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
² Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
³ Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


¹⁴ Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

LAZIMA UCHANGANYIKIWE TU, HAMNA NAMNA!
 
Uwiiiii hapa ndo mnaponiachaga hoi ndugu zangu kusema Yesu ni Mu-ngu

Yohana 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
² Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
³ Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


¹⁴ Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

LAZIMA UJICHANGANYE TU HAPO, HAMNA NAMNA.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Huyo Mungu aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kutenda dhambi?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wasio na uwezo wa kutenda dhambi?

Kama huyo Yesu alikuja duniani kumsaidia binadamu na dhambi, Kwa nini ukifa unahukumiwa dhambi zako?

Kama ukifa unahukumiwa dhambi zako, Huyo Yesu alikomboa nini?

Yohana 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
¹⁷ Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
¹⁸ Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
¹⁹ Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
 
Hakuoa ila alikuwa na mwanamke aliyekuwa karibu yake sana hata jamii ikamshuku kuwa huenda ni wapenzi, hata miongoni mwa wafuasi wake.

Hata baada ya kuondoka kwake yule mwanamke alisema kaachiwa maagizo na hayo maagizo yalikuwa tofauti na aliyoachiwa Petro na wanafunzi wengine.

Petro akaona mambo yasiwe mengi akaelekea.zake Roma ambapo baadae sana kukazaliwa catholic.

Ila Maria wa Magdala alipewa kipaumbele cha kipekee san na Yesu, kuanzia mwanzo hadi mwisho wa uwepo wake.

Kuna kitu tumechukua hapo wakuu wa kataa ndoa.
Maria Magdalena alikuwa mama mzee mwenye Fedha nyingi alizozitumia kuwezesha injili ya Yesu
 
Zipi zilikuwa sababu za msingi za yeye kutooa wala kuwa na mchumba?

Mje mtupe darasa kwa kweli.
The man kwa wakati ule alikuwa outcast. Akivunja karibu taratibu zote za wale wanaojiita wastaarabu wa zama hizo hivyo kwao alionekana msela fulani hivi huenda ingekuwa hata sasa watu wangemkataa.
 
Angeendekeza mapenzi angepoteza umakini kwenye kazi yake aliyotumwa na Mungu.
Wanawake ukiwaendekeza endekeza unapotea mazima.
 
Moja ya mada za kipuuzi na zimeachwa kwa makusudi na Moderator kutrend humu jukwaani, basi na hii nayo haikosi. Mada inagusa imani ya baadhi ya watu, ila imeachwa kwa makusudi ili watu watoe tu maneno yao dhihaka, nk.
 
Back
Top Bottom