Hivi kwanini Yesu hakuoa wala kuwa na mchumba miaka yote hiyo?

Hivi kwanini Yesu hakuoa wala kuwa na mchumba miaka yote hiyo?

Alijua kusudi lake la yeye kuwepo duniani.

Kila mtu ana kusudi la yeye kuzaliwa na mission ya kufanya. Usipojua kusudi la wewe kuwepo duniani utaishi tu na kuishia hutaacha legacy yoyote hata kwa ngazi ndogo tu ya familia.
 
Kwanza, Yesu Kristo hakuja duniani kwaajili hiyo

Pili, Hakuongozwa na tamaa ya Ngono, alizishinda tamaa zote za mwili, alikuwa na uungu ndani yake

Nakusubiri,
Yesu ni Mungu?
 
Tazama watu Wengi genius huwa awaoi maana kua na mwanamke lazima utasitisha mambo yako kwa ajiri yake, pia lazima ufanye mambo ya kijinga Ili mueze kwenda sawa na mwanamke,pia mwanamke naishi kwa hisia, sio Akili au Logic

Genius hawaongozi jamii, na ukiwaangalia ni kama wehu!

Musa, Ibrahim, Suleiman, Daudi wote walioa!
 
Ametuokoaje. Mbona bafo tuna dhambi?
Kwa kujua na kwa kutokujua.. Yesu alikuja ulimwenguni kulikuwa ni kwasababu ya kumsaidia mwanadamu na dhambi..


Hapo mwanzo shida kubwa ya mwanadamu ilikuwa ni dhambi na dhambi ikasababisha uadui wa mtu na Mungu wake..

Kwahiyo Bwana Yesu alikuja kuabolish dhambi kwa kuna kaka na kufufuka kwake.. Mshahara dhambi ni mauti..

Ili mpasa mtu afe kwasababu ya dhambi na kukosa ushirika na Mungu.. Lakini Bwana Yesu(hakufanya dhambi huyu wala hakuwa na asili ya dhambi) akatulipia hilo deni(adhabu ya watu wote ilikuwa juu yake), akafa yeye na kwa kufufuka kwake akaishinda mauti na kuzimu..

Kwa uzima huo uliomo ndani yake ndio wanatakuwa nao wote watakao amini hicho nilichoandika hapo juu..

Sasa unaweza ukasikia ukachagua kutokuamini na unaweza ukasikia ukachagua kutokuamini lakini haimanishi ni uongo..

Tatizo la dhambi limefutwa ukiamini unafanyika kiumbe kipya ambacho hakiongozwi na mwili bali na Roho wa Mungu..

Ila usipoamini ni lazima tu mwili ukutawale na mwili ukikutawala ndio inaleta hapo matokeo ya dhambi kama wizi, uzinzi chuki na mengineo
 
Ndoa ni kwa wanaume tuu, wavulana daima hawana uwezo wa kuvumilia hekaheka za ndoa
 
Hiyo ya trinity haina mashiko kiroho yaani Mungu kwenye Mungu mwana Mungu roho na Mungu neno ni mambo ambayo ukimwambia mtu ajustify beyond doubt huwa ni mwendo wa kung'atang'ata meno tu
Ila unaamini wewe una Roho, nafsi na Mwili?
 
Back
Top Bottom