Hivi kweli hili taifa la Marekani (USA) litakuja kupitia kiuchumi?

Baada yakusoma hii koment naomba niwe mpenzi msomaji tu mgonga like wa hizo zinazofuatia huko chini
Ila niwakumbushe watu US sio mwisho wa dunia wala mwanzo wa dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi Kama ni hivo mchina anatawala karibia bara zina la Africa Baadhi ya mataifa ya Asia, Baadhi ya mataifa ya ulaya,Marekani ya kaskazini[U.S.A] mataifa mengibya ya Marekani ya Kusini na Australia kote huko mchina anadai madeni yasiyolipika kirahisi
 
Uwe watumia akili

Mchina kampita Mmarekani watu tu

Wachina wanapenda kwenda ishi au pewa Uraia Marekani na si kinyume chake
Aya bhana umeshinda [emoji1]











 

Attachments

  • Top-Countries-by-Exports-2.jpg
    39.3 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220510-004348.jpg
    38.1 KB · Views: 9
Watu wanaongozwa na mahaba sio uhalisia
Wanasema china Hana madhara kwa U.S.A ni Kama kikaragosi [emoji1].akamuulize Trump au Biden je china anafanana na mnyama gani? Watamwambia china ni Kama dragon ukicheza nae anakutemea Moto unaungua. Wakitaka kujua china Hana madhara kwa America wafanye Kama kumuekea vikwazo ndio watajua hawajui
 
Kwani English ilikuwa lugha ya U.S.A au Uingereza tokea zamani Sana ata kabla U.S.A ajawawa Superpower na je ni sahihi kusema ufaransa ni super power kwa sababu lugha yake ni kubwa duniani?[emoji848]
 
Uwe watumia akili

Mchina kampita Mmarekani watu tu

Wachina wanapenda kwenda ishi au pewa Uraia Marekani na si kinyume chake
Unadhani wanauomba uo uraia kwa ajili ya vacation tu[emoji1]? Wachina mpaka Africa wapo kutokana na wingi wa raia wao .wapo sehemu mbali mbali duniani kusaka fursa na si kingine. population ya china ni Mara tatu ya population ya U.S.A
 
Unajua na sababu zipi zilizoifanya U.S.A kuwa race mbalimbali?
 
Marekani bado tupo nae saana
 
Kwani English ilikuwa lugha ya U.S.A au Uingereza tokea zamani Sana ata kabla U.S.A ajawawa Superpower na je ni sahihi kusema ufaransa ni super power kwa sababu lugha yake ni kubwa duniani?[emoji848]
Sijaelewa lengo la kuliza hivi mkuu.Sema kiufupi sana ni kwamba hii inayoitwa US kama superpower mchango mkubwa umetoka kwa watu wa mataifa yafuatayo,Scotland,Ireland,The UK,Wales(ambao kiufupi sana English ni first language)plus contribution ya watu wa Afrika ya Magharibi kama historia itakuwa haijasema uongo.

Jambo ilikuwa ni kuongelea mchango wa lugha katika kueleza utawala wa mtu/taifa.Lugha ni chombo cha mawasiliano,bila lugha haya mambo unayoita maendeleo ya kiuchumi sijui tech hakuna kwa maana lugha ina facilitate sharing(i.e info,experience,trade and list goes on) ndio lugha pekee imefanya kitu kama transfer of tech kuwa rahisi.

Ukiniuliza kwamba English ndio lugha ya Kwanza kwa US?Jibu langu litakuwa ndio, kwa maana English ni first language kwa majority ndani ya US.Ukiniuliza habari za kifaransa kuwa lugha kubwa? sina ushahidi wowote zaidi tu ya kuangalia rank yake basi,lakini ukubwa wa English natizama influence yake katika tech,sports and games,films,international trade,education n.k linganisha na kifaransa chako au lugha nyingine pendwa na jibu utalipata mwenyewe.

Jingine kuweka mambo sawa ni kwamba na France ni superpower sema katika daraja tofauti na US,which is why the US is said to be a leading capitalist Superpower.Remember the word "leading".
 
Marekani anaimiliki China yenyewe. Kapeleka makampuni yake kule halafu kawaleta huku wanunue bond zake.

Ukiona China ujue huyo ni mmarekani. Kwahiyo jumla ya uchumi wa marekani ni kujumlisha na huo wa China.
Wamarekani wa Buza
 
Unanihakikishia kuwa nikilikagua jeshi la Marekani nitawakuta wasandawe?
 
Basi Kama ni hivo mchina anatawala karibia bara zina la Africa Baadhi ya mataifa ya Asia, Baadhi ya mataifa ya ulaya,Marekani ya kaskazini[U.S.A] mataifa mengibya ya Marekani ya Kusini na Australia kote huko mchina anadai madeni yasiyolipika kirahisi

Madeni yapi hayo yasiyolipika
 

Hadhari ndogo. USA sio taifa la kikabila (racial) kama China, India, Japan, Russia, Germany, etc. Linakusanya vipaji vyote na mitaji yote ulimwenguni. Km, tajiri mkuu duniani hivi sasa, Elon Musk, asili yake ni Afrika ya Kusini na kampuni yake ya Tesla inayoongoza kwa magari ya umeme. Silicon Valley imejaa wahamiaji wenye akili kubwa wanaendeleza the American dream.

USA ni dhana (concept) ni ndoto iliyoasisiwa na watu waliotaka uhuru kamili wa mtu binafsi wakipinga kudhibitiwa na tawala za kikale za kikabila na kihafidhina kama Babeli, Greek, Roma, Ottoman, British empires.

Ni kazi ngumu sana kulishinda taifa ambalo ni dhana (concept) na ndoto ya wajasiriamali duniani. Wamarekani wenye asili ya Ujerumani ndio walioiwahisha Marekani kuongoza kwenye teknolojia ya anga; wenye asili ya India na China wanaongoza kwenye ICT na mitandao ya fedha; wenye asili ya Ulaya wanaongoza kwenye tafiti za sekta kadhaa. Best brains za Afrika zinahamia Marekani kila kukicha.

Utawala ni wa kimfumo, kidemokrasia; hautegemei maono na busara za mtu mmoja. Itachukua muda sana kubomoa hiyo dhana na ndoto ya wengi duniani.
 

Fatilia history ya Athens kipindi Cha kina pilato na Socrates ilikuwaje.
 
Fatilia history ya Athens kipindi Cha kina pilato na Socrates ilikuwaje.
Dunia ime-advance sana toka enzi za medieval empires. Marekani ni product ya mchakato wa uboreshaji (refinement) wa dhana zote kuu za kijamii toka enzi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…