Hivi kweli hili taifa la Marekani (USA) litakuja kupitia kiuchumi?

Hivi kweli hili taifa la Marekani (USA) litakuja kupitia kiuchumi?

Nikukubushe kidogo tu.
Ilikuwa Misiri na civilization ya kutosha, badae akaja muashuru akafata Mbabeloni Tena akaja umedi na uajemi, then Mambo yakarudi ulaya ambabo Ugiriki ilitamba chini ya Alexander the great na badae Roma chini ya mpompei, Mambo yalirudi mashariki ya Kati katika enzi za Ottoman empire. Mkuu ulaya iliendelea Tena hapo mara Uk, mara Ujerumanu chini ya Hitler na mambo yakarudi USA miaka ya 1900s. History never stop, the power will continue to shift from one country to another and from one continent to another. Don't worry mabadiliko huwa pole pole lakini huwa linajitokeza Jambo moja tu ndani ya one year na kila kitu kinabadilikika kabisa.
Baada yakusoma hii koment naomba niwe mpenzi msomaji tu mgonga like wa hizo zinazofuatia huko chini
Ila niwakumbushe watu US sio mwisho wa dunia wala mwanzo wa dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siku hz watu wana mfumo mpya wa kukutawala ambayo huenda ni hatari na ni ngumu kujikwamua , mfumo wa akina Uingereza na Ufaransa ni old fashioned , Amka bro , ss hv watu wanachagua wanaenda wap na kufuata nn ? na kina umuhimu gan kwao ? Huo mfumo wa zaman ulikuwa unawacost sana maana wanatoa ela kufanya ujenz wa miundombinu ambayo wataiacha bila kuwa na faida nao ila ss hv unaomba mkopo wa kujenga mradi wa reli pia ela unawalipa wao wajenge hiyo reli kisha wanakuendesha kupitia deni lao ( akil kwa mukichwa )
Basi Kama ni hivo mchina anatawala karibia bara zina la Africa Baadhi ya mataifa ya Asia, Baadhi ya mataifa ya ulaya,Marekani ya kaskazini[U.S.A] mataifa mengibya ya Marekani ya Kusini na Australia kote huko mchina anadai madeni yasiyolipika kirahisi
 
Uwe watumia akili

Mchina kampita Mmarekani watu tu

Wachina wanapenda kwenda ishi au pewa Uraia Marekani na si kinyume chake
Aya bhana umeshinda [emoji1]
Eqw9Uzo6hjGfdbju40_RHscQchAmrgSTxJ-qQ4r5Ywk.jpg

1236.jpg

UstNFnoWyiCpBUXgQ_s6iyqgoNhIZe_IxENIiFF5eyw.jpg

SOURCE-IMF.jpg

Top-Countries-by-Exports-2.jpg

maxresdefault(2).jpg

Screenshot_20220503-233921.jpg
Screenshot_20220503-231520.jpg
Screenshot_20220503-225719.jpg
Screenshot_20220503-233510.jpg
Screenshot_20220503-155902.jpg
Screenshot_20220503-101850.jpg
Screenshot_20220503-085751.jpg
IMG_20220503_104322.jpg
 
Attachments

  • Top-Countries-by-Exports-2.jpg
    Top-Countries-by-Exports-2.jpg
    39.3 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220510-004348.jpg
    Screenshot_20220510-004348.jpg
    38.1 KB · Views: 9
Watu wanaongozwa na mahaba sio uhalisia
Wanasema china Hana madhara kwa U.S.A ni Kama kikaragosi [emoji1].akamuulize Trump au Biden je china anafanana na mnyama gani? Watamwambia china ni Kama dragon ukicheza nae anakutemea Moto unaungua. Wakitaka kujua china Hana madhara kwa America wafanye Kama kumuekea vikwazo ndio watajua hawajui
 
Asee kama hii ni kweli basi ujue ni hatari kwa US.

Sema ujue nini!! utawala wa US hapa kwa planet sio currency yake pekee.Guess what!! US ana influence katika hii planet katika haya maeneo,technology(hapa jaribu kidogo tu uangalie katika info.tech usiangalie industrial tech.Kampuni kama Meta,IBM,ALPHABET,Paypal,Apple inc na kuendelea zote either ownership yake ni Wamarekani au zinamaskani na operation zake nyingi ni huko)

Angalia kwa mfano kwenye michezo pamoja na burudani(ukitoa football ambayo Uk,Spain,Germany,France na Italy wanautawala mkubwa, basi michezo mingine yote karibia US ana ushawishi mkubwa kupita hao wanaodhaniwa kuja kuchukua status yake.Mfano,Basketball,NBA unaona ushawishi wake,Rugby,Wrestling nenda kwenye Music industry najua ni rahisi sana kutaja wasanii kutoka US ila task hii ukipewa utaje wachina sidhani kama utaeleweka hapa).

Mwisho kabisa kwanini inakuwa ngumu ata China kumbwekea US,ni kwasababu uchumi au niseme ustarabu wa Mchina uko embedded na kile tunaita American culture.Just imagine,China anapiga hatua katika technology lakini hawezi kumarket product zake duniani bila kuzipa label au kudocument katika lugha ya Kiingreza(hii ina maana kwamba China bado sio independent katika aspect tunaita culture i.e refer to language that China use to market their products worlwide).Hii naweza kusema haina tofauti na mtoto ambaye bado yupo kwa baba yake kapatiwa chumba tu cha kuishi lakini kila kukicha anatunisha misuli kwa baba yake(Hii nikimanisha mtoto kumkosea baba yake heshima)
Kwani English ilikuwa lugha ya U.S.A au Uingereza tokea zamani Sana ata kabla U.S.A ajawawa Superpower na je ni sahihi kusema ufaransa ni super power kwa sababu lugha yake ni kubwa duniani?[emoji848]
 
Uwe watumia akili

Mchina kampita Mmarekani watu tu

Wachina wanapenda kwenda ishi au pewa Uraia Marekani na si kinyume chake
Unadhani wanauomba uo uraia kwa ajili ya vacation tu[emoji1]? Wachina mpaka Africa wapo kutokana na wingi wa raia wao .wapo sehemu mbali mbali duniani kusaka fursa na si kingine. population ya china ni Mara tatu ya population ya U.S.A
 
Alijaribu akashindwa ndo maana sasa hatawali, ndo maana nilisema kamwe dunia haiwezi kutawaliwa race moja. Wamarekani ni combination ya damu ya dunia nzima, Marekani kutawala dunia ni sawa na kwamba dunia inajitawala. Mfano leo ukitawaliwa na mchina ni kutawaliwa na race moja, damu moja. Angalia viongozi na maafisa wa Taasisi za Marekani afu linganisha na China, Russia, Japan, Saudia, ama nchi yoyote Ile.
Unajua na sababu zipi zilizoifanya U.S.A kuwa race mbalimbali?
 
Hii kitu tangu miaka ya 2000 wachambuzi wanasema Marekani itapitwa na China na Leo tupo 2022.
Mwaka 2011 kuna report ya IMF ilisema kwamba China itaipita USA kiuchumi 2016
2016: when China overtakes the US | Mark Weisbrot

Kuna nyingine ilisema China ingeipiku USA mwaka 2020 lakini Leo tupo 2022 na Ngoma bado mbichi.

Na sasa hivi reports zinasema China itaipiku Marekani 2030s au 2050.
Marekani itakuja kupitwa kiuchumi lakini sio Leo wala kesho ukizingatia Kwasasa uchumi wa China haukui kwa Kasi kama ulivyokua unakua mwanzoni Kwa double digit Kwa sasa unakua kwa 6-5 asilimia na kila siku Kasi inapungua,pia China inasumbuliwa na tatizo la uzee,rasilimali watu (watu hawazai Sana),viwanda vinahama vinahamia nchi nyingine km Vietnam nk sababu gharama ya uzalishaji inazidi kuongezeka (China).Tuombe Mungu atupe uhai tuone itakavyokua,lakini km trend ikiendelea hivi siioni China ikiipiku USA kiuchumi Karne hii.
Marekani bado tupo nae saana
 
Kwani English ilikuwa lugha ya U.S.A au Uingereza tokea zamani Sana ata kabla U.S.A ajawawa Superpower na je ni sahihi kusema ufaransa ni super power kwa sababu lugha yake ni kubwa duniani?[emoji848]
Sijaelewa lengo la kuliza hivi mkuu.Sema kiufupi sana ni kwamba hii inayoitwa US kama superpower mchango mkubwa umetoka kwa watu wa mataifa yafuatayo,Scotland,Ireland,The UK,Wales(ambao kiufupi sana English ni first language)plus contribution ya watu wa Afrika ya Magharibi kama historia itakuwa haijasema uongo.

Jambo ilikuwa ni kuongelea mchango wa lugha katika kueleza utawala wa mtu/taifa.Lugha ni chombo cha mawasiliano,bila lugha haya mambo unayoita maendeleo ya kiuchumi sijui tech hakuna kwa maana lugha ina facilitate sharing(i.e info,experience,trade and list goes on) ndio lugha pekee imefanya kitu kama transfer of tech kuwa rahisi.

Ukiniuliza kwamba English ndio lugha ya Kwanza kwa US?Jibu langu litakuwa ndio, kwa maana English ni first language kwa majority ndani ya US.Ukiniuliza habari za kifaransa kuwa lugha kubwa? sina ushahidi wowote zaidi tu ya kuangalia rank yake basi,lakini ukubwa wa English natizama influence yake katika tech,sports and games,films,international trade,education n.k linganisha na kifaransa chako au lugha nyingine pendwa na jibu utalipata mwenyewe.

Jingine kuweka mambo sawa ni kwamba na France ni superpower sema katika daraja tofauti na US,which is why the US is said to be a leading capitalist Superpower.Remember the word "leading".
 
Marekani anaimiliki China yenyewe. Kapeleka makampuni yake kule halafu kawaleta huku wanunue bond zake.

Ukiona China ujue huyo ni mmarekani. Kwahiyo jumla ya uchumi wa marekani ni kujumlisha na huo wa China.
Wamarekani wa Buza
 
Hizo tawala zote ulizotaja ilikuwa ni race moja, kamwe dunia haiwezi kuwaliwa na race moja, lazima utaanguka tu. Unapozungumzia Marekani unazungumzia race zote za dunia, makabila na mataifa yote ya dunia, yaani wahaya, wahindi, wachina, wakorea, wasomali, wakerewe, waarabu, waajemi, nk. Kwa kifupi wamarekani ni watu wa makabila yote ya dunia. Yaani kwa lugha nyingine ni akili kutoka Kona zote za dunia zimeungana kutengeneza kitu kimoja. Kwenye jeshi la Marekani kuna hadi wachanga, kwa hiyo usilinganishe kabisa na hizo tawala zingine zilizopita, Marekani ni mkusanyiko wa dunia nzima hakuna mwenyeji pale.
Unanihakikishia kuwa nikilikagua jeshi la Marekani nitawakuta wasandawe?
 
Basi Kama ni hivo mchina anatawala karibia bara zina la Africa Baadhi ya mataifa ya Asia, Baadhi ya mataifa ya ulaya,Marekani ya kaskazini[U.S.A] mataifa mengibya ya Marekani ya Kusini na Australia kote huko mchina anadai madeni yasiyolipika kirahisi

Madeni yapi hayo yasiyolipika
 
Nikukubushe kidogo tu.
Ilikuwa Misiri na civilization ya kutosha, badae akaja muashuru akafata Mbabeloni Tena akaja umedi na uajemi, then Mambo yakarudi ulaya ambabo Ugiriki ilitamba chini ya Alexander the great na badae Roma chini ya mpompei, Mambo yalirudi mashariki ya Kati katika enzi za Ottoman empire. Mkuu ulaya iliendelea Tena hapo mara Uk, mara Ujerumanu chini ya Hitler na mambo yakarudi USA miaka ya 1900s. History never stop, the power will continue to shift from one country to another and from one continent to another. Don't worry mabadiliko huwa pole pole lakini huwa linajitokeza Jambo moja tu ndani ya one year na kila kitu kinabadilikika kabisa.

Hadhari ndogo. USA sio taifa la kikabila (racial) kama China, India, Japan, Russia, Germany, etc. Linakusanya vipaji vyote na mitaji yote ulimwenguni. Km, tajiri mkuu duniani hivi sasa, Elon Musk, asili yake ni Afrika ya Kusini na kampuni yake ya Tesla inayoongoza kwa magari ya umeme. Silicon Valley imejaa wahamiaji wenye akili kubwa wanaendeleza the American dream.

USA ni dhana (concept) ni ndoto iliyoasisiwa na watu waliotaka uhuru kamili wa mtu binafsi wakipinga kudhibitiwa na tawala za kikale za kikabila na kihafidhina kama Babeli, Greek, Roma, Ottoman, British empires.

Ni kazi ngumu sana kulishinda taifa ambalo ni dhana (concept) na ndoto ya wajasiriamali duniani. Wamarekani wenye asili ya Ujerumani ndio walioiwahisha Marekani kuongoza kwenye teknolojia ya anga; wenye asili ya India na China wanaongoza kwenye ICT na mitandao ya fedha; wenye asili ya Ulaya wanaongoza kwenye tafiti za sekta kadhaa. Best brains za Afrika zinahamia Marekani kila kukicha.

Utawala ni wa kimfumo, kidemokrasia; hautegemei maono na busara za mtu mmoja. Itachukua muda sana kubomoa hiyo dhana na ndoto ya wengi duniani.
 
Utawala ni wa kimfumo, kidemokrasia; hautegemei maono na busara za mtu mmoja. Itachukua muda sana kubomoa hiyo dhana na ndoto ya wengi duni

Hadhari ndogo. USA sio taifa la kikabila (racial) kama China, India, Japan, Russia, Germany, etc. Linakusanya vipaji vyote na mitaji yote ulimwenguni. Km, tajiri mkuu duniani hivi sasa, Elon Musk, asili yake ni Afrika ya Kusini na kampuni yake ya Tesla inayoongoza kwa magari ya umeme. Silicon Valley imejaa wahamiaji wenye akili kubwa wanaendeleza the American dream.

USA ni dhana (concept) ni ndoto iliyoasisiwa na watu waliotaka uhuru kamili wa mtu binafsi wakipinga kudhibitiwa na tawala za kikale za kikabila na kihafidhina kama Babeli, Greek, Roma, Ottoman, British empires.

Ni kazi ngumu sana kulishinda taifa ambalo ni dhana (concept) na ndoto ya wajasiriamali duniani. Wamarekani wenye asili ya Ujerumani ndio walioiwahisha Marekani kuongoza kwenye teknolojia ya anga; wenye asili ya India na China wanaongoza kwenye ICT na mitandao ya fedha; wenye asili ya Ulaya wanaongoza kwenye tafiti za sekta kadhaa. Best brains za Afrika zinahamia Marekani kila kukicha.

Utawala ni wa kimfumo, kidemokrasia; hautegemei maono na busara za mtu mmoja. Itachukua muda sana kubomoa hiyo dhana na ndoto ya wengi duniani.
Fatilia history ya Athens kipindi Cha kina pilato na Socrates ilikuwaje.
 
Fatilia history ya Athens kipindi Cha kina pilato na Socrates ilikuwaje.
Dunia ime-advance sana toka enzi za medieval empires. Marekani ni product ya mchakato wa uboreshaji (refinement) wa dhana zote kuu za kijamii toka enzi hizo.
 
Back
Top Bottom