Hivi, kweli kabisa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliamini Polepole yuko Tanzania?

Hivi, kweli kabisa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliamini Polepole yuko Tanzania?

naamini walitaka kuchukua ndugu zake kama ramsom ili asiongee, wamekosa nini sasa? ndio hao kosa la gwajima adhabu wanapewa waumini. kosa la polepole,mange au maria sarungi (kama kweli wangekuwa na kosa) lakini adhabu wanapewa watanzania wote kwa kufunga mitandao. hawajui humo kwenye mitandao wengine ndio wanapata pesa ya kula, wanahubiri wanafanya yote. mfano, wakifunga youtube leo au facebook, sisi tunaosali tutapata shida kwa sababu tunapata mahubiri humo, tunapata na nyimbo. imagine taifa kubwa lenye vyombo vyote vya ulinzi wanaweweseka kwa viwatu vinna au kumi tu hadi kufungia mitandao yote, nadhani wanataka watanzania wasijue wala kuona chochote, waishi gizani tu ili wao wawafanye wapendavyo.
Imeonyesha ishara ya vitu wanavyoviogopa
Kuna mtu anatoa hayo maagizo wayafuate na iwe siri kwao na wakijaribu kufuatilia nani
Inapotezewa au mtu anatishiwa kifo
Mamlaka inayohusika na mawasiliano
Kwa nn wafanye hivyo

Na kama huo mtindo umeanza
Utatumiwa sana kufunga Youtube
Na itafika stage wanazima mitandao yote
Kisa kuficha ukweli

Wamejidhihirisha wanachokiogopa
Hawaoni aibu

Jiulize kwa nini hadi leo Mapolisi hawajawakamata watekaji?
Yani waseme kikundi fulani kinahusika au watu fulani
 
Mkuu Mshana Jr . Hivi unadhani ''hawa watu'' wana akili? Tukiona wanavyoteka na kuua vijana wadogo kabisa wasio na hatia tunaweza kudhani wana akili hata za kuvukia barabara? Ukiona wanapiga picha eti wakifuatilia ''kesi'' ya Lissu unadhani kuna ubongo hapo? Yaani kwangu mimi nadhani kuna kikundi cha watu wajinga kabisa, na possibly kinasimamiwa na wajinga wenzao (may be mzee wa mapete na Abdul?) kufanya operation. Hivi hata kuzima mitandao leo ilikuwa ni lazima?
Huo muda waliopoteza kufuatilia kesi ya lissu na kupoteza muda kufunga makanisa ya Gwajima
Kwa nn wangeutumia huo muda kutafuta wahalifu wanaohusika na utekaji
 
ndo utamaduni tulio jiwekea baada ya mkapa kumaliza kipindi chake, tukaanza kung'oa watoto wa watu kucha, na tukapata pori letu pendwa kwa ajili ya kutesea watoto wa watu,

yaani pol pole ana hoja asikilizwe ila kwa machawa hawa wenye njaa siyo rahisi kumulwa Ndugu Slowslow
Dah we jamaa unajua kuchonganisha jamii
 
AMANI haiombewi. AMANI ni matokeo ya kutenda HAKI, kutendeana kwa HAKI...

AMANI sio tendo linalokuja automatic pasipo kutenda wajibu fulani...

Hata tukimwomba Mungu atupe AMANI, bado jibu lake ni kuturudisha kutenda vyema yale tunayoyakosea kuyatenda na kuifukuza AMANI tuitakayo....

Jibu lake litakuwa mtaipata AMANI kama mtatendeana nyie kwa nyie kwa HAKI maana mimi Mungu wenu ni MUNGU wa HAKI..!

KWA HIYO: Hakutakuwa na AMANI bila kuomba Mungu atupe neema ya kutendeana kwa HAKI..

NA KWA HIYO TENA: Tutakuwaje na AMANI kama hatujui kuwa hii AMANI tuiombayo ni tunda la HAKI...?
Wewe hata haukunielewa nililenga kuonesha kuwa ikiwa polepole anatungaisha hivi itakuaje tukipata Adui kutoka nje !?
 
Ila chadema bwana.🤣🤣🤣🤣🤣
Si Mzee si kijana wote akili zao zinakuwa sawa tu. Yaani hapa wenyewe ndo wanajadili mada yaani.....ya kitaaalamu, inayohusu ukinzi na usalama wa nchi yaani. Mijinga mijinga flani inakesha jf hapa kufarijiana eti inafahamu kuhusu tiss🤣🤣🤣🤣

Ushauri;
Tunajua hamumpendi Samia, na hiyo sio hoja kabisa kwake na kwetu watanzania wote, ila tumieni akili basi jamani hata kidogo.
 
Ila chadema bwana.🤣🤣🤣🤣🤣
Si Mzee si kijana wote akili zao zinakuwa sawa tu. Yaani hapa wenyewe ndo wanajadili mada yaani.....ya kitaaalamu, inayohusu ukinzi na usalama wa nchi yaani. Mijinga mijinga flani inakesha jf hapa kufarijiana eti inafahamu kuhusu tiss🤣🤣🤣🤣

Ushauri;
Tunajua hamumpendi Samia, na hiyo sio hoja kabisa kwake na kwetu watanzania wote, ila tumieni akili basi jamani hata kidogo.
Chadema wamefungiwa kufanya siasa popote pale, kwani Polepole na Gwajima ni Chadema
 
Back
Top Bottom