Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

Ndio zipo , Kariakoo watu wanaburuza hyo faida Kwa masaa, inatokana na bidhaa unaozouza , na mtaji ulio nao na coverage ya wateja , kama una coverage mpak nje ya nchi Mzee lazima ugonge tuu
Sahihi kabisa mkuu
 
Sportkula kunasiku anaingiza hiyo faida Hadi Bilion kwa siku japo sio siku zote 😄 niutani lakini
 
Ukiuza milioni Mia kiwa ahesabu faida Ni Kama 10% hivyo kwa MTU mwenye mauzo ya Bilion moja anauhakika wa kutoa Milion 100 faida lakin hapo Kuna VAT na makorokoro mengine kibao
 
Swala ni kwamba,lzm kuwe na uhusiano Kati ya mtaji,faida na risk huwezi niambia una million 5,kwa mwezi ufunge 100m,kitu ambacho hakiwezekani Sasa mtoa mada unasema umechoka kufanya unachokifanya unamtaji wa Bei gani uingize hiyo hela?
 
Nafikiri kuna biashara ambazo unaweza piga hela hio kama mzunguko mkubwa. Mfano Azam na biashara nyinginezo kama hizo.
 
Hilo ni kweli mkuu
 

Mkuu,, biashara ya milion 100 faida uelewe na mtaji wake utakua kuanzia bilioni!!

Hizo ni za makampuni ya simu na madini au wenye sheli zinazojaza wateja
 
Sema unatumia lugha Kali saana kuonesha ww unajua saana but ungeongea kawaida tuu ,,maana limeulizwa swali kama ww hujui au huamini piga chini sasa cha ajabu nini hapo km mtu anaagiza kutoka njee na anauza nguo au vifaa vya umeme Kwa bei ya jumla?!!!
 
Sema unatumia lugha Kali saana kuonesha ww unajua saana but ungeongea kawaida tuu ,,maana limeulizwa swali kama ww hujui au huamini piga chini sasa cha ajabu nini hapo km mtu anaagiza kutoka njee na anauza nguo au vifaa vya umeme Kwa bei ya jumla?!!!
samahan kama nilikukwaza. Jf haiwek kumbkumb nilipost saa ngap, ukute ilikuwa usiku nimeshanyimwa kitu. Lkn ujumbe ndo huo huo.
Neno faida ni la kimahesab zaid kutoa mtaji, matumizi, kodi/tozo na gharama nyingine.
 
Mkuu umenikumbusha RICHMOND. Ile kampuni ya kufua umeme. Milioni 152 kwa siku ilikua inapokea kutoka serikalini tena kwa miaka ile ya 2008.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Facebook inaingiza zaidi ya milioni 9 kwa sekunde Apple wanaingiza zaidi ya milioni 6 kwa sekunde! Inategemea na biashara yako,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…