Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!


• Tumegawanywa kisiasa tena siasa za ushabiki. Bado vijana wenzetu wengi wanaamini shilingi ina pande mbili. Katika siasa watafanya na kufikiri na kuyaona mambo yote kama 'daikotomi' fulani. Wanaowawakilisha wachache ili pengine waseme kwa niaba ya wengi kwa watu wenye maamuzi hawasemi, ama wanasiasa huingilia mchakato. Siasa za upande zinaaathiri sauti ya pamoja kama vijana. Wakiitishwa vijana waseme yanayowasibu wengi huja ki-UVCCM, ki-BAVICHA ama ki-NgomeYaVijana-ACT n.k, hoja za msingi haziguswi wanabaki kushindana. Hali hii inaanzia vyuoni mpaka huku. Tunashida!

• Uchumi wa kidigitali. Kuna mwanaJamii forum humu aliwahi kusema “kwa sasa tuna aina tatu za ulimwengu: 1. Kimwili 2. Kiintaneti na 3. Kiroho”. Ulimwengu wa kidigitali unachukuliwa poa, kama kianasa, haupewi uzito unaostahili. Ni taasisi na kada chache ambazo zimevuna kwa ufanisi nafasi ya intaneti katika kuhudumia watu wa eneo lao k.v michezo. Sheria, sera zetu zimekuwa 'reactive' badala ya kuwa 'active' ama 'proactive'.

Eneo lakidigiti linasemwa tu nahisi kunaweza kuwa na sababu nyingi; mimi nitaje mbili. Mosi, tuna kizazi kinachoongoza ambacho ni kigeni cha teknoloji ya kidigitali. Tuna viongozi wengi ambao baada ya shule huacha kujifunza, kwa namna dunia inavokimbia hawa wanakuwa wajinga kadri siku zinavyosonga. Unyumbulifu ni mdogo, na si wepesi kuchangamkia fursa. Tuna sheria za kukomesha na kudhibiti, kwa sababu wanaoshikilia makali wanakuwa wajinga kadri dunia inavyosonga mbele kiteknolojia wao huendelea kijitutumua na vyeti vyao ili hali dunia imeawaacha.

•Umaizi wa kidigitali upo chini sana. Viongozi wengi ni wageni katika ulimwengu huu wakigitali, hususani waliokwenye nafasi. Intaneti na mitandao ya kijamii inachukuliwa katika uhasi ama ustarehe. Vijana mashuleni haaafundishwi mamboa ya twiter, facebook wala jamii forum; wameachwa wajifundishe wenyewe (wanajilindaje) lakini serikali imekuja nashiria kadhaa ili kudhibiti matumizi (inajilinda).

Kama dhima ya elimu ni kuwemwezesha mtoto kupambana na mazingira yake basi ijulikane kwamba kuna mazingira ya kimabile, kigitali na kiroho. Kwa sababu vitu vyote humwathiri mtu kwa namna moja ama nyingine ujuzi katika hayo mambo unahitajika.

•Jambo usilolijua huwa ni kama upuuzi tu. Kuna kizazi hapa ambacho kwa kweli ndo kina kontro nchi suala la mazingira ya kidigitali na TEHAMA kwa ujumla ni vitu vya kidhahania sana, halitilii maanani. Shule na taasisi vinajengwa na mahitaji ya mawasiliano ya intaneti hayapewi uzito.

•Biashara za mtandaoni ni biashara zinazohitaji mazingira mazuri ya kisera na sheria. Kwa mfano, unaweza kujifunza chochote mtandaoni na ukawa gwiji lakini ukashindwa kupata tenda sehemu fulani, wakikutaka leseni. Bado teknolojia imepewa taswira ya 'umasihara' fulani.

Kufanya 'forex' na biashara zingine sio kulala na kuamka tajiri. Shamba utalima mwaka wa kwanza, kama jipya, linaweza lisitoea mazao mengi ila mwaka wapili na watatu likaanza kuchanganya, ndivyo ilivyo mtaandaoni. Mtu anaefanya biashara mtandaoni anachukuliwa kama mvivu ama mtu ambae hajitbui na anapenda hela za mteremko. Hata hivyo, uzuri wa teknolojia huwa inajipigania, ni ngumu kushindana nayo. Pamoja na hayo hasara huwa nikuchelewa kuanza.
0759 170 823
 
Nilikutana na mshikaji mmoja kazini akaniletea hizi stori. Ati Kaka yake anafanya onlone forex. Kwamba nikimpa milioni 3, nitakuwa napewa faida ya laki 5 kila mwezi na nitakapoamua kuchukua mtaji wangu nitapewa muda wowote. Akaongeza kwa kusema hata Mke wake kaacha kazi maana anaingiza karibu mil 1 kila mwezi so kaona vikazi vya lako tatu anajichosha tu.

Nikamwangalia mtu mwenyewe anayenishawishi na hali yake ya maisha nikampotezea. Baada ya miezi kama mitatu akanijia nimuuzie gari yangu ati kaipenda. Tukakubaliana bei. Aisee kumbe jamaa tapeli tu hana iasue ya maana mjini. Pesa iliyobaki kwenye mayzo ya gari 1.5M alinizungusha mwaka mzima.

Hizo online bussness ni kazi za wavivu.
 
Forex ni biashara nzuri tu kama biashara nyingine na inaweza kukuletea faida nzuri lakn kwa mda mrefu...wabongo tunajua fx unaingia tu pap unapiga hela..hakuna kitu Kama hicho et mtu unasoma mwez mmoja afu unategemea ulijue soko..never ..utapigwa na utasema fx Ni utapeli...invest kwny knowledge kwnz .. knowledge ile knowledge yenyewe uelewe kinagaubaga unafanya nn.. otherwise utakufa kwa stress....achana na haya cjui pyramid scheme cjui ponza cjui nn cjui smarthela...Utapeli tu
 
Taja online busines tofauti na nilizotaja hapo juu ....

Mkuu tafadhari naomba unitajia hizo online business tofauti na hayo makundi nimeyoweka hapo juuu ...
Samahani mkuu,unatumia broker/site gani kuuza na kununua hisa za U.S.A?
 
Kuna kazi online nyingi tu ila sio za kipuuzi kama ulizotaja. Zinataka profession na lazima upige kazi. Nitaweka mojawapo kwa wazee wa fursa:

 
NaombeniUafanuzi nini maana Ya Vloging
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…