Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Umetisha Sana,

Kuna siku nimeingia morning report wilaya ya ilala, MD na Clinical officers wakaanza kubishana kwa kumpa mgonjwa wrong dose.., mwisho kabisa

Mfamasia akaongea kwamba mgonjwa alitakiwa kupewa dose flani kwa kiwango flani, na sio Kama madaktari walivyoandika apewe.
Tanzania wengi wanakufa kwa style hiyo, kuna ndugu yetu ni marehemu kuna hospitali kubwa tu alikuwa anatibiwa, immunity zake zikawa zinashuka baadaye tulimpeleka Acha Khan akalazwa pale, kwenye Doctors discussion wakagunduwa Dawa alizokuwa anapewa ndio zinashusha immunity, walipombadirishia Dawa hali yake ikawa inaimarika.
 
Very interesting topic.
Lazima kuwe na connection kati ya mfamasia na tabibu. Ili wakutane mahali ni lazima kuna masomo wanasoma yanayowakutanisha mahali. At the end, wote lazima wajue kufanya diagnosis(mfamasia kwa kiwango kidogo na tabibu kwa kiwango kikubwa), wote lazima wajue kufanya prescription (mfamasia kwa kiwango kikubwa na tabibu kwa kiwango fulani).
Mfamasia kujua kufanya dianosis au kufanya prescription hiyo ni by interest or for fun tu, hawajibiki kwa hilo kwa mujibu wa taaluma yake. Hilo ni jukumu kamili la Daktari.

Na kisheria ni kosa la kitaaluma kwa mfamasia kufanya diagnosis or prescription for actual patient. Kwanini? Hakufunzwa kufanywa hivyo, hakupimwa ufahamu huo, hakuidhinishwa kufanya hivyo na mwisho hakuapishwa kufanya huo wajibu.


Karani wa mahakama kazi yake ni kuhudumia watumiaji wa mahakama kama kutunza kumbukumbu za mahakama, hapaswi kutoa hukumu hata kama ana ufahamu wa kiuzoefu katika hukumu za kimahakama.
 
Kingine hakuna Kurugenzi ya Famasi kule Wizarani inayohusiana na kada hii ...
Kiufupi hii kada imewekwa chini ya uangalizi wa madaktari wizarani ..

Hawajui kazi za wafamasia ni zipi...

Unakuta Zahanati sehemu ya dawa amekaa nurse ...ndie anatoa dawa ..

Kuna vitu vingi sana vya kubadilisha hii kada

Vitu gani mkuu zaidi ya kutaka kuongezewa wigo wa maeneo ya kugawa dawa,nilikua na iheshimu sana kozi ya famasi ila nilipigundua graduates wake mwisho wa siku wanakuja kugawa dawa niliona ni upuuzi mtupu haina faida kwa nchi hii.
 
Exactly, anayefanya kwenye viwanda na yule wa hospital wanakuwa na majukumu tofauti.
Ila Bongo kuna Wafamasia wanawazidi madaktari.

Yupo mmoja namfahamu ana famasi yake na laboratory hapo na anatibu wagonjwa hasa wanawake na Watoto, hilo Nyomi lake si la kitoto, anapiga sana pesa.

Jamaa anajuwa Dawa nadhani ndio siri ya mafanikio yake.
 
Kingine hakuna Kurugenzi ya Famasi kule Wizarani inayohusiana na kada hii ...
Kiufupi hii kada imewekwa chini ya uangalizi wa madaktari wizarani ..

Hawajui kazi za wafamasia ni zipi...

Unakuta Zahanati sehemu ya dawa amekaa nurse ...ndie anatoa dawa ..

Kuna vitu vingi sana vya kubadilisha hii kada
Sio kweli kwamba hilo ndilo tatizo.
Katika famasi nyingi nchini ambazo hazitegemei kurugenzi wizarani ,zina wauza dawa wengi wengine hawajasoma hata fani yoyote ya afya na wanauza dawa.
Wafamasia wenyewe mnawaajiri na wakati mwingine wapenzi wenu tu ama watoto wa mjomba walioishia form 4.

Kama ni ubabaishaji ni nyie ndio mnaufanya msilalamike hapa.
Fani kama za maabara huwezi kukuta house girl anapima maabara tofauti na famasi ambapo wanaruhusiwa tu kwa kisingizio eti wanafanya chini ya uangalizi!
Hebu nenda kafanye kazi ya uaskari usalama barabarani chini ya ujinga mnauita uangalizi kama itawezekana

JamiiForums mobile app
 
Umetisha Sana,

Kuna siku nimeingia morning report wilaya ya ilala, MD na Clinical officers wakaanza kubishana kwa kumpa mgonjwa wrong dose.., mwisho kabisa

Mfamasia akaongea kwamba mgonjwa alitakiwa kupewa dose flani kwa kiwango flani, na sio Kama madaktari walivyoandika apewe.
Vitu vya namna hii wangekuja waliosoma hizi course watoe maelezo yaliyoshiba zaidi.

Ila hata ukisikiliza zile morning reports zao, uliyetoa dawa ni LAZIMA useme aina ya dawa, na UJAZO na kwanini ujazo huo kwa muda uliosema(hapo interns jasho la meno linawatoka)
 
Back
Top Bottom