Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Tanzania wengi wanakufa kwa style hiyo, kuna ndugu yetu ni marehemu kuna hospitali kubwa tu alikuwa anatibiwa, immunity zake zikawa zinashuka baadaye tulimpeleka Acha Khan akalazwa pale, kwenye Doctors discussion wakagunduwa Dawa alizokuwa anapewa ndio zinashusha immunity, walipombadirishia Dawa hali yake ikawa inaimarika.
 
Mfamasia kujua kufanya dianosis au kufanya prescription hiyo ni by interest or for fun tu, hawajibiki kwa hilo kwa mujibu wa taaluma yake. Hilo ni jukumu kamili la Daktari.

Na kisheria ni kosa la kitaaluma kwa mfamasia kufanya diagnosis or prescription for actual patient. Kwanini? Hakufunzwa kufanywa hivyo, hakupimwa ufahamu huo, hakuidhinishwa kufanya hivyo na mwisho hakuapishwa kufanya huo wajibu.


Karani wa mahakama kazi yake ni kuhudumia watumiaji wa mahakama kama kutunza kumbukumbu za mahakama, hapaswi kutoa hukumu hata kama ana ufahamu wa kiuzoefu katika hukumu za kimahakama.
 

Vitu gani mkuu zaidi ya kutaka kuongezewa wigo wa maeneo ya kugawa dawa,nilikua na iheshimu sana kozi ya famasi ila nilipigundua graduates wake mwisho wa siku wanakuja kugawa dawa niliona ni upuuzi mtupu haina faida kwa nchi hii.
 
Exactly, anayefanya kwenye viwanda na yule wa hospital wanakuwa na majukumu tofauti.
Ila Bongo kuna Wafamasia wanawazidi madaktari.

Yupo mmoja namfahamu ana famasi yake na laboratory hapo na anatibu wagonjwa hasa wanawake na Watoto, hilo Nyomi lake si la kitoto, anapiga sana pesa.

Jamaa anajuwa Dawa nadhani ndio siri ya mafanikio yake.
 
Sio kweli kwamba hilo ndilo tatizo.
Katika famasi nyingi nchini ambazo hazitegemei kurugenzi wizarani ,zina wauza dawa wengi wengine hawajasoma hata fani yoyote ya afya na wanauza dawa.
Wafamasia wenyewe mnawaajiri na wakati mwingine wapenzi wenu tu ama watoto wa mjomba walioishia form 4.

Kama ni ubabaishaji ni nyie ndio mnaufanya msilalamike hapa.
Fani kama za maabara huwezi kukuta house girl anapima maabara tofauti na famasi ambapo wanaruhusiwa tu kwa kisingizio eti wanafanya chini ya uangalizi!
Hebu nenda kafanye kazi ya uaskari usalama barabarani chini ya ujinga mnauita uangalizi kama itawezekana

JamiiForums mobile app
 
Vitu vya namna hii wangekuja waliosoma hizi course watoe maelezo yaliyoshiba zaidi.

Ila hata ukisikiliza zile morning reports zao, uliyetoa dawa ni LAZIMA useme aina ya dawa, na UJAZO na kwanini ujazo huo kwa muda uliosema(hapo interns jasho la meno linawatoka)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…