Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Unaposema "Medical Officer ana Recommend Dawa Akiwa hana uzoefu"......

Ulikuwa unamaanisha nini au Unamaanisha nini pengine sijaelewa hivi
 
Hii Ishu naiona ikikuwa kama kipindi kile MA NO(Nurse Officer) walianza kufanya kazi za Daktri eti kisa Wanajiita Nurse Practitioner wakang'ang'ania wawe sawa kimajukumu na Daktari...
Kuna vitu hatukatai kweli Ni vigumu kuvitenganisha ila organogram Iheshimiwe tu...
 
Na huu ndo ukweli
 
Nimewahi kuwaza hili ingawa Mimi siko kwenye tasnia ya afya.
Anayeandika au kuamuru mgonjwa atumie dawa ipi ni doctor, anayeamua mgonjwa atumie vipi dawa ni doctor. Sasa rule ya pharmacist ni nini?
Pharmacist rule yake (Kwa hospitali) ni kuhakikisha Dawa iliyoandikwa na Daktari inatolewa kwa Uhakika na kwa Dose maalumu kama ilivyoandikwa..
Na kwa kiasi kile ambacho hakitaweza kumletea Shida Mgonjwa na Pia kuona njia nzuri ipi ni sahihi ya kutumia Dawa hizo kwa dozi gani ambayo haina tatizo na kulazimika kupanga utaratibu mzuri wa utumiaji kwa kushauriana na Daktari..
Pia ndo anayeHusika na Usalama wa Dawa zote..
 
na wabunge wengine ni darasa la saba[kama bwege],,,,,,,alaf dereva wake ni form six
 
Ndo maana anaweza kufanya reconstitution/reformulation ya dawa iendane na dozi au umri wa mgonjwa, sema ndo hivyo watu tunadharauliana sana kwenye hizi taaluma.........na haya mambo yanachangiwa na serikali yenyewe kutokuweka na kufuata miundo na majukumu ambayo yako clear kwa kila taaluma.​
 
Medical officer anajua dawa?
Dah Mkuu umesoma Chuo gani ambacho kinakushindwa kujua kuwa...
Wote Daktari na Mfamasia Husoma Pharmacy ila tu Daktari husoma kwa Kiasi kile kimachohusiana na Mgonjwa...

Daktari hubase katika pharmacokinetics na kidogo Pharmacodynamics na Pharmacognosy
na mfamasia hu base kwenye Pharmacodynamics sana na pharmacognosy sana kuliko Daktari...

na ndo Maana daktari hawezi kuelelezea Dawa Ya Amoxycilne imatengenezwaje kwa sababu Hakusoma Pharmacognosy ila Ukimuuliza Dawa inafanyaje kazi kwa Mwili wa Binadamu atakuelezea mpaka inapotolewa na hata madhara yale hutokea vipi...

kwahyo usipotoshe umma Kuwa Kwenye Dawa Daktari hajui...
Japo mfamasia hajui How we Prescribe dawa na Dose maintanance na Kujua Dx ,Hx na Mx..

unaweza ukajua Dawa DUNIA NZIMA ZINATENGENEZWAJE NA ZINAKUWAJE DAWA LAKINI UKASHINDWA KUJUA DAWA GANI INAFAA KWA MGONJWA..

NB: BAHATI MBAYA MGONJWA HATAKI KUJUA DAWA INATENGENEZWAJE NA WAPI NA IMETOKANA NA NINI ANAACHOTAKA NI KUPONA NA DAWA IMLETEE MATOKEO MAZURI
 
Sasa ulitaka wafanye kazi zipi hapo hospital boss. By the way, kwa nature ya kazi zilizopo Tanzania hiyo ndio kazi ya mfamasia.
 
Nyumisi shida kubwa inakuja Kuwa zaman Kipindi sisi Tunasoma na tunakua Hizi kazi zilikuwa zikifanywa na watu wanaopenda kazi zao na wana hekima..

Shida inapokuja Mtu alienda kusoma Pharmacy akiamini kwamba atakuwa kiongozi ndo shida inapoanziaga hpa..

Na kingine kama Nursing shida kubwa ilinza pale kulipoanza kuwepo na Manurse wa Kiume wengi Ndo wakaanza kujiona wao ni vidume lakini mbona zamani ilikuwa sawa tu ...ndo mnatakiwa mjiukize hilo
 
Daktari yeye anasoma pharmacology ambayo inamwezesha kujua aina za dawa, indications kwa magonjwa mbalimbali, dosage, pharmacokinetics, pharmacodynamics, drug excretion, side effects na hii ni kwa ajili ya kumsaidia kujua ni aina gani ya dawa na dozi ya kumpa mgonjwa bila kumletea madhara makubwa.

Pharmacists nafikiri yeye anasoma dawa in much details, hivyo huwezi kumlinganisha na daktari kwenye ujuzi wa madawa.​
 
Twende taratibu kidogo!
Vyote ulivyotaja vinaingia kwenye Hizo terms Mbili za Pharmacokinetics na Pharmacodynamics...
Na nakuongezea kuwa Daktari pia Anasoma Essential Pharmacy japo Ni basic..
Na kingine Kuhusu Dawa kwa Mgonjwa na Ingedients zake kwa mgonjwa Naomba nikutoe hofu kuwa Daktari pia anasoma..
Na ndo maana amaweza kujua allaergy ya ugonjwa (Urticaria) inayosababishwa na Dawa...

Najua kuwa mfamasia anamzidi Daktari kujua Dawa lakini kipande anachomzidia hakihitajiki kwa Wagonjwa ila kwenye viwanda na Makampuni ya chemical
 
Naam mkuu,tusaidie kuchambua na mchango wa Watu wa Maabara upoje katika tiba.
 
ila na mimi naona kama mtoa mada ana hoja,
ila kwanini Pharmacist wasipewe mchakato mzima wa kuanzia ku test dawa, kuotesha wadudu wa ugonjwa, kumimini solution ya dawa , ku test wadudu wamekufa wangapi, kupima ni moles ngapi za compound fulani zimeuwa wadudu wenye miligramu ngapi. kisha ku develop equation ya hiyo reaction. kisha wakafundishwa kwenye real world ni udongo gani ambao una tabia ambazo unaweza kuuchimba sehemu na kuu- subject kwenye equation hiyo zikazalisha dawa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…