DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
Ha ha ha....[emoji28]Lazaro alipiga kimya maana njemba zile za kifarisayo zilikuwa zinataka kumpoteza kwakuwa alisababisha wengi wamwamini Yesu kwamba ndiye Kristo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha ha ha....[emoji28]Lazaro alipiga kimya maana njemba zile za kifarisayo zilikuwa zinataka kumpoteza kwakuwa alisababisha wengi wamwamini Yesu kwamba ndiye Kristo.
Ha ha ha....Tunafanana aisee[emoji28]Mkuu kwa hii Kasi yako ya kuichunguza biblia, sioni kama utaendelea kuhudhuria kanisani. Mimi baada ya kuanza kujiuliza maswali kama yako, kwa sasa nimebaki mromani mstaafu. Naongea na Mungu direct sitaki tena hivyo vitabu.
Wale gio-devi umewasahau[emoji28]Wafia dini mjee
Haswa wale wa mwamposa vs kuhani musa
Kumekucha aisee[emoji28]Tumepewa akili na marifa ila kuhoji mambo haya ni kukufuru Mungu.
Leo hii nimesikio clip ya Mchungaji mmoja maarufu sana(Mchungaji Daniel Mgogo) ambae clip zake husambaa sana mitandaoni akisema, "waliodai Israeli ni Taifa teule,ni Manabii wa Kiyahudi".
Sasa hyu Mchungaji nae anahoji/anapingana na maandiko kama kina sisi?
Mambo mengi muda mchache.
Ukifa umekufa, kula maisha kijana[emoji4]Yaani eti mtu umeshakufa eti alafu uwe na maisha mengine kwenye ulimwengu mwingine huu ni uwongo!
Twambie Sasa maisha ya lazalo yalikua Ni yapi uko kuzimuKufufuka kwa Yesu kunathibitisha hilo; yapo maisha baada ya kifo.
Wazungu walitugeuza mazuzu Sana[emoji29]Wametuweza kwakweli hasa Waafrica.
Ngoja nimuite huyo muumini wa hicho kitabu FaizaFoxyHuwezi kufafanuliwa, yani hivi vitabu mfano wake ni sawa na Nyerere mwaka 1960 anazungumzia jinsi alivyokufa na msiba wake mwaka 1999.
Ni ngumu sana kwa mtu anayetumia akili na logic kuviamini vitabu hivi, hasa kile cha Quran ndio magumashi matupu.
Mmhh!Akiwa kuzimu sio akiwa amerud dunian. Halafu ukiwa unataka kuijua Biblia usisome mstari mmoja mmoja soma kwa muktadha mzima utaielewa. Maana Yesu mwenyewe anasema cc au nyie mmepata kupewa kuzijua Siri za Mungu wengine watasikia au kusoma hawataelewa ndio maana Biblia imeandikwa kwa mafumbo. Wako wakuielewa na wako watakaopotea.
Mungu mwenyewe hakutuambia kupitia maandiko yake matakatifu; pumbavu mimi ni nani nithubutu ku-question mamlaka ya Mwenye Enzi yote?Twambie Sasa maisha ya lazalo yalikua Ni yapi uko kuzimu
Kufananisha uzingizi na kifo ni kukosa maarifa TuJinsi
Ambavyo mtu aliyelala fofofo hajitambui ndivyo mtu aliyekufa hajitambui. Utasikia watu "Unafananisha kifo na usingizi?" Ukweli ni kuwa kifo na usingizi vinafanana mno.
Hivi kama ukweli ni kwamba mtu akifa hatakuwa anajua chochote kinachoendelea ilikuwaje Yesu akatoa mfano kama huu usio na uhalisia ambao unaonyesha kwamba wafu wanakuwa na maisha mengine huko kaburini, na ndugu, jamaa, marafiki na majirani wanaweza kukutana kupiga story kukumbushana ya duniani na hata kutumana? Na kingine, kwa nini kutokana na utata unaoletwa na maandiko haya ambapo yanapingana na mtazamo wa kwamba wafu hawajui chochote kinachoendelea, inalazimishwa (?) na wajuzi (?) wa kutafsiri biblia kwamba hicho kisa hakikuwa cha kweli bali Yesu alikisema kama mfano tu kwenye mafundisho yake? Yaani Yesu kabisa atoe mfano kwa jambo nyeti kama hilo kwa kutumis kisa kisicho na uhalisia wowote na wenye kuweza kupotosha wengi?Luka 16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
²⁰ Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
²¹ naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
²² Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
²³ Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
²⁴ Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
²⁵ Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
²⁶ Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
²⁷ Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
²⁸ kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
²⁹ Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
³⁰ Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
³¹ Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Hapa panaelezea mtu akifa nini hutokea.
Mtu akiwa hai na kupata usingizi tu wa kawaida kama hajaota ndoto, kuumwa na mbu au kuguswa na chochote kamwe hawezi kujua kinachoendelea duniani. Sasa akiwa kafa kabisa ndiyo atajuaje kinachoendelea au ku-experience maisha mengine?Yaani eti mtu umeshakufa eti alafu uwe na maisha mengine kwenye ulimwengu mwingine huu ni uwongo!
Yes, inawezekana kabisaUnaweza kutunga stori zako; ukaandika kitabu ukazisambaza watu wakaziamini kwa mamilioni Mkuu?
Hakuna record popote kwenye Biblia kama alisimulia chochote, lakini baadae alikuja kufa tena.Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.
Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?
Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?
Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?
Mwenye majibu tafadhali.
Kwenye biblia za orthodox kuna details.Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.
Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?
Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?
Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?
Mwenye majibu tafadhali.
Haya mambo rahisi sana....je? Petro alijuaje yule ni Musa na Eliya wakati Yesu akiomba?. Akashauri pajengwe vibanda 3?Umeniongezea maswali ndugu.
Hapa hakuna wa kukupa jibu.Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.
Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?
Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?
Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?
Mwenye majibu tafadhali.