Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Ni mifano tu alikuwa anatoa bwana Yesu...
Ila tukio la kufufuliwa lazaro kwa mujibu wa bibilia takatifu ni tukio ambalo lilitokea. Na lazaro aliyekufa na kufufuliwa na Yesu alikuwa rafiki yake Yesu.

Hivyo haya mambo mawili tofauti.
Huo mfano ulikuwa unaelezea uhalisia wa matukio mwanadamu anapokufa au ni just paukwa pakawa?
 
Mhubiri 9:5, 10​

Biblia Habari Njema (BHN)​

5. Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote. Hawana tuzo tena; hata kumbukumbu lao limesahauliwa kabisa

10. Kila unachotaka kufanya kifanye kwa nguvu zako zote, maana, hakuna kazi, wala wazo, wala maarifa, wala hekima huko kuzimu unakokwenda.
... ule mfano wa Yesu kuhusu maskini Lazaro kifuani pa Ibrahimu tunaona yule tajiri kule kuzimu akikumbuka ndugu zake aliowaacha duniani. Ufafanuzi tafadhali.
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.

Mkuu kuna mtu anaitwa DR Mambo AMP kuna vitabu aliniorodheshea nikavisome kuhusu the church history.

sijawahi kujuta kumfahamu huyu kiongozi ni anajua haya maswala mpaka anakera. Nipo nasoma kitabu kimoja kinaitwa “when Jesus become god” kiukweli wengi hatufahamu historia. Tusome mkuu historia
 
Mleta mada kweli katika wanaume wako wote uliowahi kuwa nao hakuna hata mmoja anayesoma na kuielewa biblia akusaidie swali lako?
Au mna date na wanaume ili mradi ana kende na dushe?
Ndio shida inapoanzia..))
 
Mkuu kwa hii Kasi yako ya kuichunguza biblia, sioni kama utaendelea kuhudhuria kanisani. Mimi baada ya kuanza kujiuliza maswali kama yako, kwa sasa nimebaki mromani mstaafu. Naongea na Mungu direct sitaki tena hivyo vitabu.
Willy Gamba enzi zake kikosi cha kisasi, au Allan quaterman na Umsolopagaz ukisoma vile vitabu unaona ni vitu halisi kabisa.

Sasa pata Picha ya magenious wa middle east jinsi walivyotunga hivi vitabu huchomoki.

North Korea walishapiga marufuku hivi vitabu vya middle east kitambo tu kwenye nchi yao.
 
... ule mfano wa Yesu kuhusu maskini Lazaro kifuani pa Ibrahimu tunaona yule tajiri kule kuzimu akikumbuka ndugu zake aliowaacha duniani. Ufafanuzi tafadhali.
Huwezi kufafanuliwa, yani hivi vitabu mfano wake ni sawa na Nyerere mwaka 1960 anazungumzia jinsi alivyokufa na msiba wake mwaka 1999.

Ni ngumu sana kwa mtu anayetumia akili na logic kuviamini vitabu hivi, hasa kile cha Quran ndio magumashi matupu.
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.
Mkuu usipende kuamini story za Biblia na Qur'an kwani zile ni hadithi tu za kuchanganya watu akili wa kuwatia hofu
 
Mimi sio msomaji mzuri wa Bibilia, ila nimesikia habari ya Lazoro kufa na baadae kufufuliwa na Yesu wakati Yesu bado yuko hapa duniani na tena tunaambiwa alikuwa anatoa harufu.

Swali ni je, Lazaro alihadithia nini kuhusu kifio au hakusema chochote?

Kwa mfano, wakati anakata roho, nini hasa kilitokea?

Na je, alikufa mara ya pili au ilikuwaje?

Mwenye majibu tafadhali.
Akili yako inakuwa kama memory card. Inaflashiwa unakuwa hukumbuki chochote
 
Ni mifano tu alikuwa anatoa bwana Yesu...
Ila tukio la kufufuliwa lazaro kwa mujibu wa bibilia takatifu ni tukio ambalo lilitokea. Na lazaro aliyekufa na kufufuliwa na Yesu alikuwa rafiki yake Yesu.

Hivyo haya mambo mawili tofauti.
²⁸ kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
²⁹ Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
³⁰ Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
³¹ Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Musa anayemzungumzia hapa ni yupi maana Musa alikufa kabla ya Yesu kuzaliwa
 
Luka 16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
²⁰ Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
²¹ naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
²² Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
²³ Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
²⁴ Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
²⁵ Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
²⁶ Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
²⁷ Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
²⁸ kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
²⁹ Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
³⁰ Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
³¹ Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Hapa panaelezea mtu akifa nini hutokea.
Simulizi hii ya Yesu inaonyesha hili ni jambo kamili lilitokea haikuwa hadithi ya kutungwa kama ile hadithi ya Msamaria mwema
 
Musa anayemzungumzia hapa ni yupi maana Musa alikufa kabla ya Yesu kuzaliwa
Inawezekana kutoa mfano wa kisa cha zamani kana kwamba kinatokea leo. Anaanza na neno; "palikuwa... "; happened in the past!

Hata leo tunaanzaga; hapo zamani za kale kujenga taswira ya kisa cha zamani kana kwamba kinatokea sasa.
 
Back
Top Bottom