Mkuu Nyani Gabu,
Ukiwa rational na logical thinker utajiuliza maswali kama hayo, lakini jamaa zetu hawana hilo! Si vyema kubeza dini ya mtu yoyote, lakini wakati mwingine unajiuliza mbona hawa jamaa wana twisted thinking, maana Israel lazima ingelipiza kisasi, furaha yao ilikua ya muda mfupi mno! na imewaachia madhara ya miaka mingi, na ile compromise ya "Two State Solution" sasa hivi haipo tena. Kwa kifupi wamejiletea NAKBA Nyingine, na mbaya zaidi kuliko ile ya 1948! Na ambayo imesababisha hata swaiba wao mkubwa Syria kuangushwa!
Nadhani walidanganywa na Iran, wakitegemea Iran itaingia kwenye vita kamili na Israel (total war) na Hezbollah itashambulia kutoka North! Hilo halikutokea! Lakini kwa mtu anayefuatilizia kwa makini, Iran haitaki vita vya moja kwa moja na Israel ! Kama ingetaka ingefanya hivyo muda mrefu sana! Hiyo ni kauli mbiu yao toka Khomeini alipomwondoa Shah 1978, na vita vya moja kwa moja na Israel vinaweza kufungulia mlango ndani ya Iran na kusababasha utawala wao kuanguka! Hilo lilikuwa kosa kubwa kwa Hamas.
Lakini vile vile Hamas hawakutegemea Israel itakuwa brutal kiasi hicho! Walijua ile mbinu ya kujificha ndani ya raia italipa! Ulimwengu utaipigia kelele Israel, na Israel itasimisha mapigano, hilo halikutokea, na vile vile walitegemea pigo la October 7 litaleta mgawanyiko mkubwa ndani ya Israel, lakini mgawanyiko hakuondoa uwezo wa IDF.
Kwa kifupi Hamas na Hezbollah hawana kabisa strategic thinking, walikuwa na plan ya October 7 tu! Sio zaidi ya hapo! Najua wengi hawatakubali, kijeshi, huwezi kulinganisha uwezo wa jeshi la Israel na Hamas, vita vya leo vinataka kutumia anga ( air power) vinataka mechanized infantry etc, mwenye kufikiri angeona wazi vita vikichukua muda mrefu Hamas ingekosa pumzi!
kama ulivyosema Gaza haitakuwa Gaza tena!