Nimekuwa nikijiuliza kwa muda sasa bila kupata majibu.
Kwa nini Hamas walianzisha chokochoko ambayo msukosuko wake hawawezi kuustahimili?
Wapalestina wa Gaza wanapaswa kuilaani kabisa Hamas na kuipinga kwa hali zote.
Ndiyo, Wapalestina hao wa Gaza walikuwa wanaishi kwenye mazingira magumu sana, kwa hisani ya Israel.
Lakini kabla ya Oktoba 7, hali haikuwa mbaya kama ilivyo hivi sasa.
Sasa hao Hamas wakijua kabisa uwezo wao pamoja na ule wa adui yao, kwa nini waanzishe songombingo ambayo walijua kabisa hawawezi kuimudu?
Labda walikuwa wakiichukulia poa Israel.
Viongozi wa Hamas ni wapumbavu sana. Gaza haitorudi kuwa Gaza tena.
Ndo matatizo ya kuongozwa na watu wapumbavu.
In the end, was it all worth it? I think not.
walijipanga kwa miaka mingi tu, trained mno, na mle ndani kulikuwa na wanajeshi hadi wa iran, wale walikosa vifaa tu ila walikuwa makomandoo wazuri mno kwa vita. Lengo lao ilikuwa kuvamia israel, kuanza kuua, vita ianze, hamas apige kutokea gaza, hezbollah awasaidie kutokea lebanon, na iran amalizie ili isrel ifutike.ndio maana adui wa Mungu ayatollah alikuwa anaongea wazi kitambo kwamba kuna siku mzayuni atafutika kwenye ramani pale. bahati mbaya, matokeo yakawa tofauti, myahudi ameuwa karibu magaidi wote wa hamas, kauwa makamanda wa kutosha wa iran, hezbollah aliyekuwa na malaki ya silaha akaingia, viongozi wake wakuu wote wameshauza sasaivi, ikabaki kutazamia ceasefire, iran kaenda kuwaambia waache vita wapokee ceasefire.
matokeo: majengo kadhaa ya israel yamebomoka na watu kadhaa wameuawa, ila upande wa gaza, haikaliki, imeteketezwa yote. hakuna sehemu gaza bom halijatua. na kwa hezb, majengo yote wanayomiliki yavunjwa, wamepata hasara ambayo hawakutegemea.
way forward: mzayuni anajiandaa tukio kama lile lisijetokea tena, anajenga silaha bora, na kununua zingine. Israel haitakuja kufutika milele. kwa sababu pale Yerusalem ndio mji wa Mungu.