Fredwash
JF-Expert Member
- Oct 27, 2009
- 1,400
- 2,010
Nami pia nina wasiwasi na hili, kuwa dola la kishia la Iran ndio liko nyuma ya mipango ya tukio lile. Hamas wako karibu mno na akina Khamenei. Matokeo yake mazayuni wamewageukia wapalestina wasio na nguvu na kuwaua na kuwaumiza kwa kuchupa mipaka na dhulma.
Na tukio lile ghafla limekuja wakati Saudia akiwa katika mchakato wa mazungumzo ya amani na mazayuni. Kuna watu walipinga lile kwa jazba, lakini kufanya amani na mazayuni haikuwa na maana wanawapenda mazayuni na wanaunga mkono mambo yao, bali kufanya vile ilikuwa ni kutengeneza mazingira ndugu zetu angalau wawe na amani na wapumzike na zipungue shida kwa sababu kwa wakati huo/huu hawakuwa na nguvu ya kupigana na mazayuni. Lakini ghafla linatokea tukio hilo...
Qaddara Allahu maa shaa fa'ala
Na hasa ndio approach iliiotakiwa.. mbona Jordan wanashare mipaka na israel hakuna migogoro.. tatizo palestina upande wa gaza wamekubali kutawaliwa na watu radicals ambao wanaamini katika dawa ya moto ni moto..
hamas wanataka israel ifutike kabisa kitu ambacho haiwezekani. Matokeo yake kwa kadiri wanavyojaribu ndio wanaIdi kupoteza.. na tatizo wanatumika na waraabu wenzao .. kungekuwa na nia ya dhati ya waarabu kuwapa utaifa palestina ingeshatokea zamani sana
We fikiria sudan tu hapo walipoanza kuchapana kwa misingi ya dini .. mara likatolewa wazo.. dunia ikalisimamia sudani ikagawanywa.. kwa nini ishindikane kwa palestina kuwa na utaifa
Jibu ni kuwa Israel hakubali kwa sababu anajua nia ya Hamas wao wanataka kufuta taifa la israel same to Iran. Maana yake ikiwa palestina itakuwa taifa.. italindwa na soverignity laws.. inaweza hata ikamruhusu iran akaweka silaha kali pale waka cordinate na Lebanon .. waka attack israel na kuifuta maana hilo
Ndio lengo mama .. hata vitabu vyao vya dini vinataka iwe hivyo.. na kijiografia Israel ni ndogo sana..
Ndio maana netanyau alisema palestina kuwa na utaifa its a death sentence kwa Israel
sasa hivi dunia imebadilika.. ili kumuwin Israel wangeleta approach ambayo israel wangeona kuwa hawa jamaa sio Threat kisha wakaja na proposal ambayo wangewekeana mipaka basi Palestina ikawa nchi kamili
Wakaanza kupata wawekezaji na misaada.
Hapo Hata Israel wangeona aibu.. na dunia nzima ingekuwa upande wa Palestina kama ingetokea Israel kafanya ndivyo Sivyo.. lakini toka enzi na enzi approach ya wa palestina imekuwa ni jino kwa jino..
Arafat alijaribu kutafuta suluhu ya mezani hadi wakaingia mkataba na israel.. ila hamas wakagoma
Ndio chanzo cha Mgawanyiko na alipokufa gaza ikabaki kwa Hamas. Kule west babk wakabaki Fatah chama ambacho kinaongozwa na Abbas..